Umakini unahitajita sana unapotaka kuanzisha biashara ili kuepuka kuchoma pesa zako

Kipondo Cha ugoko

JF-Expert Member
Apr 12, 2023
655
1,042
Wana jukwaa habari zenu!
Leo ningependa kushare nanyi kitu ambacho nimekiona ktk ka utafiti kangu kadogo kuhusu biashara nyingi za maduka ya nguo na saloon ama za kiume au za kike kufa kifo Cha mende.(hasa kwa maeneo ambayo yapo pembezoni mwa mji)

Nimekuja kugundua watanzania walio wengi hawana/hatuna Elimu nzuri wa biashara na hapo ndipo wengi wanaoshindwa hizo biashara nilizozitaja huanzia. kushindwa kwa hizo biashara Huanzia kwenye kuchagua LOCATION,KODI ZA FLEMU NA BEI YA KUUZA BIDHAA.

1. LOCATION. unajua Kuna watu wanafungua biashara mahali mpaka unajiuliza hivi huyu huku anamuuzia nani? Unakuta mtu kufugua duka eti la nguo mitaani ndani ndani huko, mtu akipita ni baada ya lisaa lingine ndo utaona mtu mwingine anapita Tena! Sasa wewe huko hizo nguo unamuuzia nani? Kama sio kuchoma pesa ni Nini sasa(utasikia nauzia mtandaon) nyoooooh!!!

Alafu ooh! Biashara ngumu! Ooh Kuna watu wanachezea biashara yangu na blaa blaa kibao kumbe ujinga ni wako mwenyewe. Utachoma sana mtaji🤣

Kuna mahali nilipita maeneo ya tegeta ndani ndani huko nikakata Kuna mwamba kafungua bonge la barber shop ambalo kwa makadilio ya haraka haraka jamaa kawekeza kama 15ml+
Kajaza ferniture za dhamani kweli kweli lkn sasa wateja hakuna ameajiri vinyozi na wadada wapo pale mda wote wanapiga miayo tu.
Sasa wewe hiyo saloon ya ghalama huko vichochoroni ya Nini kama sio kutafuta watu maneno? Mbona mnapenda kuchoma pesa zenu kwa biashara hewa? Haya kwa Tsh5000 utampata nani huko uswekeni? Mbona mambo mengine ni madogo ya kujiongeza tu mpaka ushauriwe kweli wakati unaona Hali halisi?

2. KODI ZA FLEMU. Hapa sasa ndio wengi huingia Cha kike, kwa mfano unachukua flemu ya 500k/mwezi kwa maeneo kama GOBA( Bora Bora iwe pale center) lkn sio center kabisa! Then unatumia ghalama kuuubwaaa kutengeneza vi-ferniture na shelfu
Mzigo unaoukuta dukani sasa ndo kichekesho🤣 kama ni nguo ni chache mpaka zinahesabika! Bei yake sasa haaaa! Utakimbia bila kuangalia nyuma.
Yaani unagusa nguo ya kawaida kbs utasikia hiyo 150k,ile pale laki2 sasa kwa goba my friend utamuuzia nani nguo laki2? Na hiyo yote najua ni kujaribu kuballance ujinga ulioufanya kwenye kukurupukia flemu ya laki5. Nakuhakikishia utaifunga tu hiyo biashara Yako! Hamna namna utaweza toboa labda kama hilo duka ni zunga tu lkn unabiashara zako nyingine unafanya.

Haya mwingine anasuka style ya twende msibani kwa 50k kisa kapalamia flemu isiyoendana na uhalisia, sasa makosa Yako unataka wateja ndio wagharamie, unasahau kwamba huku goba hakuna kina wema sepetu, Aunt Ezekiel Wala maslay queen, huku Kuna akina mwajuma kamswekeni, hao washua unaowaona wanapita na magari mambo yote wanayamalizia mjini.
Lkn pia nao hawana pesa ya kufidia mikulupuko Yako. Utaifunga tu hiyo saloon Yako labda kama unakabiashara kengine hapo.

Aaah! Nishachoka kuandika jamani naomba niishie hapa lkn kikubwa ninacho washauri wapambanaji wenzangu kuweni makini sana mnapo taka kuanzisha biashara. Inauma sana kwenda kuchoma pesa Yako ambayo umeipata kwa tabu sana ( wengine wamebeba mikopo nyumba iko mbele) wengine wameuza maeneo Yao ya urithi ili wakajaribu biashara lkn mwisho wanafanya makosa makubwa ya kuwekeza sehemu isiyofaa, kukurupukia flemu za bei mbaya kisa umeziona zinang'aa.

Haya Nisha wasanua kazi kwenu japo mwandiko na mpangilio mbovu ila ujumbe umefika.
 
Goba kuna fremu za 500k kwa mwezi?
Fremu town ukibugi Ndio msiba unaanzia hapo, usiombee Mtaji nao Umekopa,
 
Hivi Hawa wenye umiliki wa frem wanatuchukuliaje wapangaji yani akilala akiamka anakuja na ukurasa mpya mpk 500K mibiashara ulivyokua migumu saivi watatuua kwa mawazo😂😂
 
Back
Top Bottom