Vijana 97 Wapewa eka 500 mradi wa BBT Dodoma

Vijana 97 Wapewa eka 500 mradi wa BBT Dodoma

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
83,852
Reaction score
90,359
My Take
-Programu ya BBT inaendelea
-Programu ya kuchimbia wakulima wadogo visima vya Bure inaendelea
-Programu ya mbolea ya ruzuku inaendelea

Vijana, wanawake 97 wakabidhiwa mashamba ya BBT-II BahiVijana na wanawake 97 kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma wamekabidhiwa ekari 500 za mashamba kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT-II).


Akizungumza Novemba 5, 2026, Mkuu wa Idara ya Kilimo wa halmashauri hiyo, Siwajibu Selemani, amesema awali wanufaika waliofaulu usaili walikuwa 99, lakini wawili wamefariki dunia kabla ya uzinduzi wa mradi.

Ameomba Serikali kuboresha miundombinu ya maji, barabara za ndani, makazi na maghala ya kuhifadhia mazao.

Mbunge wa Bahi, Kenneth Nollo, amewataka wanufaika kutumia fursa hiyo kuzalisha kwa ajili ya biashara na chakula, huku wanufaika Maria Mahona na Juma Hassan wakisema mradi huo utawasaidia kujikwamua kiuchumi na kuongeza uzalishaji wa mazao nchini.
 
Back
Top Bottom