Vigogo wahusishwa na kufyatua Noti bandia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vigogo wahusishwa na kufyatua Noti bandia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ben Saanane, Mar 14, 2010.

 1. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #1
  Mar 14, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  • Wamo wafanyabiashara wakubwa, wanasiasa

  na Mwandishi Wetu
  Tanzania Daima


  BAADHI ya wafanyabiashara maarufu hapa nchini na makada wa chama kimoja kikubwa cha siasa wanahusishwa katika kashfa ya kutengeneza noti bandia ambazo zimepenyezwa katika mzunguko wa fedha hapa nchini kwa muda mrefu sasa.

  Habari ambazo Tanzania Daima Jumapili, imezipata kutoka vyanzo vya kuaminika zinabainisha kuwa wafanyabiashara hao wamekuwa wakijihusisha kufadhili na kudhamini shughuli mbalimbali kwenye jamii kiasi cha kujizolea umaarufu.

  Fedha hizo zinachapishwa na makampuni ambayo yanamilikiwa na baadhi ya wafanyabiashara matajiri (tycoons), ambao faida yake wamekuwa wakiitumia kwa wanasiasa, viongozi wa dini na watendaji wa serikali kila wapatapo nafasi ya kujumuika na makundi hayo.

  Chanzo hicho kilidokeza kuwa noti zinazotengenezwa na wafanyabiashara hao ni zile za sh 5,000 na sh 10,000, ambazo zimekuwa na viwango vya hali ya juu, kiasi cha kumfanya mtumiaji asiweze kubaini kuwa ni bandia.

  Kwa mujibu wa chanzo kimoja cha habari, mzunguko wa fedha hizo ni mkubwa kiasi cha taasisi zinazojishughulisha na fedha kujikuta zikishindwa kuzizuia, kwa hofu ya kuingia hasara kubwa.
  Noti hizo ambazo baadhi yake Tanzania Daima Jumapili imeziona, zinashabihiana kwa kiasi kikubwa na hata baadhi ya wafanyakazi wa benki wamejikuta wakizitumia.

  Vituo vya mafuta na mabasi ya abiria ni miongoni mwa sehemu ambazo gazeti hili limebaini kuwa fedha hizo chafu zinatumika kwa kiwango kikubwa, ambapo huchanganywa na nyingine ambazo ni halali.

  Tanzania Daima Jumapili imedokezwa kuwa baadhi ya vigogo wanaotengeneza fedha hizo wamekuwa wakizitawanya sehemu mbalimbali hapa nchini, huku wakiwapa ‘kamisheni' mawakala wao wanaozisambaza fedha hizo.

  Ili kuzuia matumizi ya fedha hizo kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imeamua kuchapisha noti za sh 500, 1,000, 5,000 na 10,000 ikizitumia kampuni za kimataifa za utengenezaji wa fedha hizo.

  Oktoba mwaka jana, Gavana wa Benki Kuu, Profesa Benno Ndulu, akiwa katika Ofisi Ndogo ya Bunge, jijini Dar es Salaam aliwaambia wanahabari kuwa tayari serikali imeshatoa zabuni ya kuchapisha noti hizo.

  Katika mchakato wa kuchuja na kupata kampuni itakayokidhi haja hiyo, Cren Currency ya nchini Sweden ilishinda na kupatiwa zabuni ya kuchapa noti za sh 500, 2,000, 5,000 na 10,000, wakati noti za sh 1,000 pekee zitachapwa na Kampuni ya De-rarue ya nchini Uingereza.

  Hadi sasa BoT haijawa tayari kutoa taarifa kuwa ni kiasi gani kitatumika mpaka zoezi hilo litakapofikia kikomo.

  Tanzania Daima Jumapili iliwasiliana na kitengo cha mawasiliano cha BoT, juu ya mbinu zinazotumika kudhibiti fedha bandia, ambapo kitengo hicho kimesema utengenezaji wa noti mpya utazingatia alama za usalama (Security features) zitakazoendana na teknolojia ya kisasa.

  Ofisa wa kitengo hicho, John Kimaro, alisema wamezingatia zaidi teknolojia ya kisasa ili kuwepo na tofauti kubwa kati ya noti halali na bandia, kwa lengo la kumuwezesha mtu kuzitambua kwa urahisi zaidi.

  "Tumezingatia maendeleo ya teknolojia zinazotumiwa na watu wanaotoa noti bandia, sisi tutakuwa juu zaidi na tuna uhakika noti zitakazokuja zitakuwa za viwango vya hali ya juu kiasi cha watu kushindwa kuzitengeneza zinazofanana nazo," alisema ofisa huyo.

  Pamoja na baadhi ya watu wanaomiliki mitambo kukamatwa na Jeshi la Polisi, BoT imesema kuwa haina taarifa ya kuwapo baadhi ya wafanyabiashara wanaomiliki teknolojia hiyo ya kuchapa noti bandia na kutaka taarifa zitolewe haraka kwenye vyombo vya habari.

  BoT imeongeza kuwa ipo tayari kushirikiana na vyombo vya dola na wananchi kuwashughulikia wale wote wanaozitengeneza noti bandia kwa kuwa wanahujumu uchumi wa taifa.

  Tatizo la uwepo wa noti bandia hivi sasa linaonekana kuwa kubwa zaidi, ambapo Septemba mwaka jana, mkoani Dar es Salaam msikiti mmoja uliopo Mburahati ulipewa msaada wa kiasi cha sh milioni mbili na mfanyabiashara mmoja (jina tunalihifadhi), ambazo baadaye zilibainika kuwa ni bandia.

  Katika sakata hilo, mfanyabiashara huyo alidai kuwa fedha hizo alizichukua dukani kwake kwa lengo la kutoa msaada katika msikiti wakati wa kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

  Uwepo wa noti hizo mara kwa mara umekuwa ukiwafanya baadhi ya wafanyabiashara hasa ndogo ndogo kupata hasa mara wabainipo kuwa hawana fedha halali.

  "Kwenye maduka huwa naona sh 5,000 na 10,000 zikiwa zimebandikwa na hazitumiki, nikiuliza naambiwa ni feki, wafanyabiashara ndogo wengi hawazijui na inawakata mitaji wajasiriamali ambao mitaji yao ni midogo," alisema Mwanaidi Hamis, mkazi wa Dar es Salaam.

  Kutokana na hali hiyo, nguvu za Jeshi la Polisi zimekuwa zikigonga mwamba kwani pamoja na misako inayoendelea ya mara kwa mara ikihusisha mbinu shirikishi, bado tatizo hilo linaendelea.
  Aprili mwaka jana, mkoani Ruvuma, Abel Mgaya (26), mkazi wa Iringa alikamatwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kukutwa na noti bandia zenye thamani ya sh 520,000.

  Mei, mwaka jana, jeshi hilo lilimshikilia Marko Sayi (26), mkazi wa Nyahanga, wilayani Kahama kwa kukutwa na vifaa mbalimbali vya kutengenezea noti bandia.

  Shaibu Ibrahim alitaja vifaa hivyo kuwa ni karatasi zilizokatwa ili kutengenezea fedha bandia, wino na pamba. Katika sakata hilo ilidaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa amewapa watu mbalimbali kiasi cha sh milioni 2.5, ambazo ni bandia ili wazitumie kununulia mazao na mifugo kutoka kwa wananchi. Hayo yamekuwa ni baadhi ya matukio yanayotoa picha halisi ya namna ambavyo biashara hii inavyoshamiri siku hata siku, licha ya jeshi hilo kujitapa kuwa linadhibiti hali hiyo na BoT ikitoa matamshi ya kukabiliana na matukio ya namna hiyo.


  My Take:
  If this is true,then we are doomed! Hii ni grave damage ktk uchumi wetu.Nowonder pia sarafu yetu inazidi kudidimia,yaaani jamani uzalendo umekosekana namna hii?hizi ni mbinu chafu ambazo kimsingi zinatumiwa na maadui wa nchi nje ya mipaka,but sasa watanzania tena vigogo wamehusika?mbinu hizi zinatumiwa na mataifa hasimu kwani wanajua ni madhara kiasi gani yanasababishwa na mbinu hizo kiuchumi.Mfano Pakistan wanatuhumiwa kuifanyia umafia huu India,Bangladesh na Thailand


  Pia,kila zinapotoka noti mpya BOT wamekuwa wakitoa matumaini kwamba itakua ngumu kwa watu kughushi

  Kwa kumalizia,Waandishi wa habari nao sijui ni kwa nini hawatoi taarifa kwa vyombo vya usalama maanke inaonekana wanakuwa na dataz.Hili si jambo la mzaha,mwananchi wa kawaida ndiye anaumia zaidi jamani!
   
 2. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #2
  Mar 14, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Obvious watakuwa wanahusika tu maana wao ndio wameikamata nchi.
   
 3. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2010
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Usalama wa Taifa my ass.. What are they doing? Inflation imefika 12%...This govt has really EFFD up.
   
 4. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #4
  Mar 14, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  -It's like we are incompetent in every department buddy!
   
 5. D

  DoubleOSeven JF-Expert Member

  #5
  Mar 14, 2010
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 661
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0


  ...nchi imekamatwa na wabongo wasiotaka maendeleo. kila chaguzi wanajazwa ubwabwa na kiwachagua wapishi wale wale! that ubwabwa must taste heavens!
   
 6. D

  DoubleOSeven JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2010
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 661
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0


  WEE! ...usalama wa taifa na inflation wapi na wapi. wewe as an individual umeifanyia NINI Tanzania yako?
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Mar 14, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,412
  Likes Received: 81,450
  Trophy Points: 280
  Hakuna kitu kinachoitwa usalama wa Taifa Tanzania bali tuna usalama wa Mafisadi na ndiyo maana mafisadi wote wamekuwa na kiburi cha hali ya juu na kufanya lolote lile walitakalo maana wanajua hakuna wa kugusa. Wamegundua pia wanaweza kuprint mabilioni ya shilingi na kuendeleza madudu yao ya kuifisadi Tanzania.
   
 8. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #8
  Mar 14, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,174
  Trophy Points: 280
  Nas anakwambia "What is made by man, can be taken apart". They were faking the big head $ 100 as son as the government printed them.
   
 9. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #9
  Mar 14, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Ulivyomjibu huyo jamaa hapo juu,hivi kweli huoni connection kati ya ela bandia na inflation?Ingwa fake currency kusababisha inflation wakati mwingine inaonekana kwamba namba ni ndogo,lakini kama kuna hela nyingi sana zimeingizwa ktk mzunguko basi mfumuko wa (Inlation) hutokea.Consequence zake ni kubwa sana kwa the middle class(tabaka la kati) na tabaka la chini

  Pia,ni wajibu wa usalama wa taifa kwani kama zinaingizwa kutoka nje na au kama mashine za kuchapishwa zinaagizwa nje kwa nini wasiwe responsible?

  Also it's a threat for our national security
   
 10. Black Jesus

  Black Jesus JF-Expert Member

  #10
  Mar 14, 2010
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nainukuu Kauli ya Mzee yusufu Makamba alikuwa na kamsemo wake huu ufuatao, Mfanya Biasha akitaka Biasha yake yende vizuri ajiunge na CCM ,ameuwacha msemo huu nbaada ya matokeo ya mambo ya Ufisadi kuwa mjada la kwa Taifa zima.
   
 11. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #11
  Mar 14, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,192
  Likes Received: 997
  Trophy Points: 280
  It's very sad, but we have to think twece. Hii issue haiwezi kuwa mbinu za chama tawala kutengeneza hofu ili wahalalishiwe kufyatua pesa mpya kuweza kupiga bao la pesa ya uchaguzi kirahisi?
  Mimi nashauri utengenezaji wa noti mpya ufanywe baada ya uchaguzi kama kweli kuna nyingi za bandia kwenye mzunguko.
   
 12. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #12
  Mar 14, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  nadhani mwaka hautaishaia bila kuwa na noti mpya ya 20,000. But thanks God watanzania tumejaliwa amani na utulivu. Tunahitaji nini zaidi?
   
 13. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #13
  Mar 15, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Wewe nafikiri ndiyo hujui maana ya usalama wa taifa unafikiri kazi yao ni kukimbizana na wauza unga tu
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Mar 15, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Watanzania watu wa ajabu kweli; hivi mnafikiri fedha bandia zinazotengezwa zaidi Tanzania ni hizo za madafu? Wengine tukisema hapa tutaambiwa hatuitakii nchi mema. Na jinsi watu wanavyopenda "greenback"..mtakoma wenyewe..
   
 15. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #15
  Mar 15, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Inflation is there already, and if that is true this may have well be condoned by those who have power. Tatizo ni kuwa sasa hivi ni kama nchi haina mwenyewe. Unaweza kuibiwa ukaenda polisi na ukaamibwa mwizi ni polisi mwenyewe.
   
 16. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #16
  Mar 15, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Hali ya mgonjwa aitwaye Tanzania inazidi kuwa mbaya, kila siku anaambukizwa magonjwa mapya kwa makusudi kabisa pamoja na kwamba bado yupo ICU.

  Kaaz kwelikweli
   
 17. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #17
  Mar 15, 2010
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,211
  Likes Received: 312
  Trophy Points: 180
  Tuliwaambieni haya mara baada ya moshi mweupe kuonekana kule Dodoma 2005. Tulisema JK alipokea nchi yenye mfumuko wa bei wa 4.9% lakini tukaonya kwamba kabla hajamaliza kipindi chake cha kwanza atakuwa ameachia mfumuko huo uwe zaidi ya 10%. Na tukabashiri kwamba akipata kipindi cha pili basi atakimalizia tukiwa na kasi ya mfumuko wa bei ya 30% au zaidi. Hiyo ni sawa na ilivyokuwa wakati BWM anaanza kipindi chake.

  We made our bed; we must sleep on it.

  Kwa wale wanaofikiria kuirudisha tena CCM Ikulu, niwaambie hivi: You ain’t seen nothing yet!
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Mar 15, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280

  kweli mwalimu na hivi walipoingiza hizi trilioni moja nyingine katika stimulus package yao tuliwahoji hapa.. sasa tunavuna tunashangaa mabua?
   
 19. H

  Hekima Ufunuo JF-Expert Member

  #19
  Mar 15, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 220
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Kwa watanzania hili kulikumbuka ni kubwa sana kwenye memory yao. Ukiamua kuweka utabiri ulioufanya hapa, utashangaa wengi watakuwa hawakumbuki.

  Hiki ni kipindi cha miaka kumi cha kurudi nyuma kama ilivyokuwa kwa Mzee Mwinyi, yeye ndiye alienda Zanzibar na kuliua Azimio la Arusha na kuanzia siku ile ni ufisadi kwa kwenda mbele. IPTL ilizaliwa wakati wake Mwinyi. Inflation ilifika 30% kwenye nchi ambayo ina amani na haina vikwazo vya kiuchumi.

  Miaka Mitano Tuko 12% hivi mpaka uchaguzi uishe tutafika ngapi? Je miaka minne baada ya uchaguzi tutafika ngapi?

  Mungu kiokoe kizazi hiki
   
 20. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #20
  Mar 15, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Hii ndiyo bongo, ukitaka kuishi vizuri, nyumba nzuri, gari zuri nk lazima utumie Bongo. watu wake wana akili kama cherehani. hata wakileta za plastiki haitachukuwa muda mrefu wabongo watadurufu
   
Loading...