Vigogo wagawana viwanja vya Gezaulole

Hawa jamaa wa manispaa hovyo kabisa. Wanatuuzia form tena unapanga foleni kuanzia saa kumi usiku lakini kiwanja hupati. Huu ni wizi wa mchana kweuupe. Sipendi
Pole sana mkuu. Haikuwa bahati yako. Mimi nimebahatisha kimoja tu though niliwajazia fomu na wanangu wote. Ayway, usiwe na wasiwasi hop kwenye waiting list na jina lako litakuwepo.
 
mukama-top2.jpg

WALALA HOI WALALAMIKA, WALITOA SH30,000 ZA MAOMBI ‘ZIMEENDA NA MAJI’

Patricia Kimelemeta
MANISPAA ya Temeke imetoa orodha ya majina ya wananchi waliopewa viwanja katika manispaa hiyo, ambayo inaonyesha kuwamo kwa vigogo wanaojumuisha mawaziri, wabunge, watendaji wakuu wa Serikali pamoja na baadhi ya watoto wa vigogo hao.Katika orodha hiyo, jumla ya watu 1,800 walipatiwa viwanja hivyo, huku majina hayo ya vigogo yakiwa ni zaidi ya 50, ambao baadhi wamejiandikisha wenyewe, wengine wake zao, ndugu na watoto wao.

Majina hayo ambayo gazeti hili iliyaona jana, yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo wa manispaa hiyo, ili wananchi walioomba viwanja hivyo waweze kuangalia kama wamo katika orodha ya waliopatiwa viwanja hivyo.

Baadhi ya wananchi waliofika kusoma majina hayo walisikika wakilalamikia hali hiyo, huku wakisema kuwa kinachoonekana ni vigogo kupendelewa na kuwanyima wananchi wa kawaida.

Katika orodha hiyo, majina yanayosomeka ni pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama; Naibu Spika, Job Ndugai; Waziri wa Mawasiliano, Sanyansi na Teknolojia, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima.

Kwa upande wa Makatibu Wakuu wa Wizara wapo, Dk Florence Turuka (Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Ramadhan Kijjah; Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Omary Chambo na Dk Idris Rashid ambaye ni Gavana wa Zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Pia wamo Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk Didas Masaburi, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa; Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam, Suleinan Kova.

Wengine ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Haruna Masebu; Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh na Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH),Marina Njelekela.

Kwa upande wa wabunge wamo Dk Augustine Mrema (Vunjo - TLP), Mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe; Mbunge wa Kibaha Mjini (CCM), Sylvester Koka; Mbunge wa Kinondoni (CCM), Idd Azzan; Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), Dk Cyril Chami na Mbunge wa Singida Kusini (CCM), Mohamed Misanga.

Wengine ni Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila; Mbunge wa Igunga (CCM), Dk Peter Kafumu na Mbunge wa Bukene (CCM), Seleman Zedi.

Wabunge wa Viti Maalumu (Chadema), Maulida Komu na Suzan Lyimo, Viti Maalumu CCM, Dk Mary Mwanjelwa na Zakhia Meghji ambaye ni mbunge wa kuteuliwa.

Orodha hiyo pia inaonyesha majina ya ukoo yanayofanana na majina ya baadhi ya viongozi ambao ni Miraji Kikwete, Khalfan Kikwete, Juanita Mramba, Suzan Mkapa, Zainab Mkomwa, George Rupia, Maimuna Mfutakamba, Mary Membe, Pharles Ngeleja, Judith Kahama na Wilfred Mwanri.

Mkurugenzi apatwa kigugumizi
Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Magreth Nyalile alipoulizwa kuhusu orodha hiyo alisema kuwa, majina hayo hajayaona na kwamba waliobandika wamefanya uamuzi huo bila ya yeye kuupitia.

“Majina yenyewe sijayaona, hivyo basi siwezi kujua ni kina nani waliopewa viwanja hivyo, kwa sababu wako zaidi ya 1,000, jambo ambalo litakuwa vigumu kwangu kubaini tatizo hilo,” alisema Nyalile.

Aliongeza kuwa, kutokana na hali hiyo hawezi kusema lolote kwa sababu yuko nje ya ofisi kwa ajili ya shughuli nyingine za ujenzi wa taifa.

Hata hivyo, Nyalile alisema mchakato wa ugawaji wa viwanja hivyo ulifuata taratibu za kisheria na kwamba hakuna mtu au kiongozi yeyote aliyependelewa, jambo ambalo linaweza kusababisha mgongano wa hapa na pale.

Nyalile alisema kuwa kama kuna viongozi walipewa kwa njia zisizo sahihi, au kwa rushwa wakati wa uwasilishaji wa majina hayo, walipaswa kutoa taarifa kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Wananchi walalama

Baadhi ya wananchi walikuwa wakiangalia majina hayo katika ubao huo walidai kuwa, baadhi ya maofisa wa halmashauri hiyo wamedaiwa kupewa rushwa wakati wa ugawaji wa viwanja hivyo.

“Walitangaza kama kiini macho, lakini tayari walikuwa na majina yao ili waweze kuwapatia na jambo ambalo limejionyesha wazi kwenye majina ya watu waliopewa viwanja hivyo,” alisema mwananchi mmoja (jina tunalihifadhi) na kuongeza:

“Kutokana na hali hii, hatuna imani na viongozi wowote wa Serikali kwa sababu inaonyesha wazi kuwa, kila mmoja anaangalia masilahi yake na si wananchi wasio na kipato”.

Aliongeza kuwa, wananchi hawana imani na viongozi wao, hivyo Serikali inapaswa kuingilia kati kwa sababu hali hiyo inaweza kusababisha matatizo.

Mwananchi mwingine aliyekuwa akifuatilia jina lake alisema: “Wewe unachokiona ni nini hapo kama siyo yaleyale ya ubinafsi! Wewe unaamini kabisa kwamba kweli hawa viongozi wetu hawana nyumba au hawana viwanja hapa Dar es Salaam.

Aliongeza: ”Kama manispaa walitangaza viwanja ili wajiuzie wangesema tu badala ya kuchukua fedha zetu Sh30,000 halafu viwanja wakajigawia wenyewe.”

Mgawo wa Viwanja

Mapema mwezi Juni mwaka huu, Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ilitangaza kwamba imepima viwanja 1,800 katika eneo la Gezaulole ikiwa ni mwendelezo wa utekelezaji wa Mradi wa Upimaji Viwanja.

Fomu za maombi ya kununua viwanja hivyo zilianza kutolewa Juni 11 na kila mwombaji alipaswa kulipia ada ya maombi ya kiasi cha Sh30,000 katika ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke iliyopo mkabala na Uwanja Taifa jijini Dar es Salaam.

“Fedha hizo hazitarejeshwa na mwombaji atajaza nakala mbili za fomu ya maombi na kuzirejesha zikiwa zimebandikwa picha 3 za ukubwa wa pasipoti. Mwisho wa kurudisha fomu hizo ni tarehe 18.06.2012 saa 8 mchana,” linasomeka tangazo rasmi la manispaa hiyo.

Wakazi wenye nyumba na mashamba ndani ya eneo la mradi ambao walikuwa wametambuliwa kabla ya zoezi la upimaji kuanza, pia walitakiwa kununua fomu za maombi kwa utaratibu uleule.

Vigogo wagawiwa viwanja Dar
 
Pole sana mkuu. Haikuwa bahati yako. Mimi nimebahatisha kimoja tu though niliwajazia fomu na wanangu wote. Ayway, usiwe na wasiwasi hop kwenye waiting list na jina lako litakuwepo.

Mkuu Rejao hii ni mara ya tatu naliwa vihela vyangu; ilala mara moja na temeke mara mbili. Nilikuwa nikiamka usiku na kwenda kupanga foleni lakini wapi wanakuja kupata watu ambao hawakuwepo kwenye foleni! Mkuu hapa kuna wizi wa mchana. Kama wanajua viwanja ni vichache kwa nini wauze maform lukuki? Viwanja havitakiwa kuwa issue ila.wao wanafanya supply iwe scarce ili demand iwe juu na wao kujipatia chochote.
 
Last edited by a moderator:
Jamani viwanja 1800, viwanja vya wanaolalamikiwa ni viwanja havizidi 50 inamana 1750 wamepewa walalahoi sasa malalamiko ya nini? mbona tumegeuka kama wale jamaa wanaolalamikia kilakitu? mi ningekuwa mojawapo ya wanaolalamika kama wangechukua viwanja 500.

wapo waliokosa kabisa ambao hata kiwanja kimoja hawana....wht are u talkinng..talk sense...kinachopimwa hapa ni tamaa. hakuna tamaa nusu...tamaaa ni tamaa tu....kama una viwanja 20; nyumba ya serikali umeuziwa tena kwa bei ya kutupa; vyeo mnagawana; kazi za umma mnagawana; makampuni ya umma mnauziana; bado mnakuja huku uswahili kwetu kugombania viota.......huu ni unyang'au
 
Viwanja 1800 vimeuzwa kwa wananchi. Kati yao, kuna viongozi wa kada mbali mbali, na kuna ndugu zao ama watoto wao. Majina yaliyoorodheshwa ya "wanene" hao ni kama 50.

1800-50= 1750. Tufikirie tu kwamba "walala hoi" 1,750 au hata 1500 wamepata viwanja, na vigogo 300 wamepata pia. Tunalalamika vigogo wamegawana viwanja!

Katika vigogo hao, wana watoto wakubwa tu...namfahamu Juanita Mramba, anafanya kazi benki moja jijini. Naye amenunua kiwanja. Tunalalamika mtoto wa kigogo kauziwa kiwanja? Hivi, wao hawapaswi kuwa na kiwanja simply because baba yake (tu assume tu) ni kigogo na ana viwanja vingine? Kweli hili ni taifa la walalamishi tu...hata tufanyeje.

Ninadhani pengine kama wamekiuka sheria, kwamba vigogo hawakustahili kuuziwa hata mmoja, na kwamba iwe ni kinyume cha sheria kumiliki kiwanja zaidi ya kimoja Tanzania, basi hawa wangekuwa wana makosa. Wengi wetu tumekuwa tunawekeza mno kwenye kulalamika kuliko kutoa maoni ya namna bora ya kuendesha mambo.

Go back to school ujifunze kufikiri...hata kwa umri huu bado huwezi kutambua hata jambo dogo kama hili....kaa soma kati kati ya mistari ili ugundue malalamiko ya wananchi ni nn,

Je malalamiko yao yanajikita kulalamikia idadi yao hao wanaolalamikiwa au tabia yao? Wewe unakomaa na idadi yao tunaofikiri nje ya box tunaichambua tabia na hulka za hawa wanaolalamikiwa........jiulize Nyerere mpaka anakufa alikuwa na viwanja vingapi mbona huyu mzee hakuwa na tamaa ya kiwango hiki?? kw taarifa yako wapo wanaotamani kuimiliki nchi nzima iwe yao....na hao si tofauti na hao unaowatetea ni hao hao.si ajabu ukawa sehemu au miongoni mwao...ndg yangu ukitaka kujua uchungu wa mwarobaini onja...

Huwezi kujua uchungu wa kuishi kwenye skwata wakati unaishi masaki; oysterbay; mikocheni au upanga.............cku ya wanyonge kurudisha nchi mikononi mwao inakaribia...wapo waliotamba na kuwatukana wananchi wao wanyonge kiasi cha kuwaita panya.lakn mwisho wao ukawa wa aibu kubwa rejea ya Ghadaf dk chache kabla ya kutangulia mbele ya haki.......rejea ya Gbagbo siku alipovuliwa ujuha na ghafla kuwa sisimizi.....

Gbagbo hakwenda na wala hajaambana na nyumba wala mali zake kule the Hague kama ambavyo ghadafi hakuondoka na Bahari Beach Hotel kwenda nayo mbinguni..hakuna atakayekumbuka kukimbia na kiwanja wala nyumba pindu wenye nchi watakapoamua kuirejesha nchi mikononi mwao...na nyakati hizi zikiwadia Mfalme huwa Mtwana huku mtwana akikalua kiti cha enzi, mtawala akigeuka kuwa mtawaluwa, kizazi cha mateso kikitamalaki dhidi ya majuha, mabwana wakigeuka kuwa kabwela , waliokuwa wakibebwa wakigeuka kuwa wachimba kokoto, waliokuwa juu wakishuka na kuwa rafiki wa tope...

Waliodhani wanaishi EDEN wakilia na kusaga meno..huku GOLLIATI akiwa kesha salimu amri mbrle ya Daudi...cku si nyingi haya tatatimia...tukutane tena hapa kukumbushana haya cku ya ahadi itakapotimia..tuombe uhai ....kumbuka "THE SOVEREIGN ARE THE PEOPLE" and always shall reign no matter how long it might take but eventually We shall TRIUMPH
 
go back to school ujifunze kufikiri...hata kwa umri huu bado huwezi kutambua hata jambo dogo kama hili....kaa soma kati kati ya mistari ili ugundue malalamiko ya wananchi ni nn, je malalamiko yao yanajikita kulalamikia idadi yao hao wanaolalamikiwa au tabia yao? wewe unakomaa na idadi yao tunaofikiri nje ya box tunaichambua tabia na hulka za hawa wanaolalamikiwa..........
mwabakuki you've said it all, Godbless you
 
[h=6]VIGOGO NA FAMILIA ZAO WAGAWIANA VIWANJA DAR- ORODHA HII HAPA.

WALALA HOI WALALAMIKA, WALITOA SH30,000 ZA MAOMBI ‘ZIMEENDA NA MAJI’

Patricia Kimelemeta

MANISPAA ya Temeke imetoa orodha ya majina ya wananchi waliopewa viwanja katika manispaa hiyo, ambayo inaonyesha kuwamo kwa vigogo wanaojumuisha mawaziri, wabunge, watendaji wakuu wa Serikali pamoja na baadhi ya watoto wa vigogo hao.Katika orodha hiyo, jumla ya watu 1,800 walipatiwa viwanja hivyo, huku majina hayo ya vigogo yakiwa ni zaidi ya 50, ambao baadhi wamejiandikisha wenyewe, wengine wake zao, ndugu na watoto wao.
Orodha hiyo ni pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama; Naibu Spika, Job Ndugai; Waziri wa Mawasiliano, Sanyansi na Teknolojia, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima.

Kwa upande wa Makatibu Wakuu wa Wizara wapo, Dk Florence Turuka (Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Ramadhan Kijjah; Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Omary Chambo na Dk Idris Rashid ambaye ni Gavana wa Zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Pia wamo Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk Didas Masaburi, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa; Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam, Suleinan Kova.

Wengine ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Haruna Masebu; Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh na Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH),Marina Njelekela.

Kwa upande wa wabunge wamo Dk Augustine Mrema (Vunjo - TLP), Mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe; Mbunge wa Kibaha Mjini (CCM), Sylvester Koka; Mbunge wa Kinondoni (CCM), Idd Azzan; Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), Dk Cyril Chami na Mbunge wa Singida Kusini (CCM), Mohamed Misanga.

Wengine ni Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila; Mbunge wa Igunga (CCM), Dk Peter Kafumu na Mbunge wa Bukene (CCM), Seleman Zedi.

Wabunge wa Viti Maalumu (Chadema), Maulida Komu na Suzan Lyimo, Viti Maalumu CCM, Dk Mary Mwanjelwa na Zakhia Meghji ambaye ni mbunge wa kuteuliwa.

Orodha hiyo pia inaonyesha majina ya ukoo yanayofanana na majina ya baadhi ya viongozi ambao ni Miraji Kikwete, Khalfan Kikwete, Juanita Mramba, Suzan Mkapa, Zainab Mkomwa, George Rupia, Maimuna Mfutakamba, Mary Membe, Pharles Ngeleja, Judith Kahama na Wilfred Mwanri.
[/h]
 
Kinachoitafuna Tanzania ni UNAFIKI. Watanzania wote wanakula kwa kamba zao. Kila mtu alipo anajipa upendeleo kadri awezavyo. Mpaka airport kwenye kupokea wageni mtu anaweza kuamua ndugu zake wakapokelewe kwenye mlango wa ndege kabisa!!! Huwezi kuona kitu kama hicho Heathrow.
Watu wakiona jambo halijafanyika in their favour ndio wanapiga kelele, sio kwa sababu wanadhani upendeleo haufai, ila kwa sababu wanaona upendeleo huo haujawafaa wao. Hatuwezi kuleta mabadiliko kwa kubadilisha jina la mtafuna nchi. Inabidi tujenge tabia ya kuchukia ubadhilifu katika ngazi zote. Kuanzia kwenye foleni ya kuchota maji kwenye bomba la kijij la kijiji, upendeleo wa kuovertake foleni za huduma benki, hospitali na kwingineko.
Haya majina yaliyotajwa kwenye hili gazeti ni kwasababu kuna walioshindwa kwenye hiyo vuta nikuvute sasa roho zinawauma, lakini katika Tanzania yetu tusidanganyane kuwa upendeleo uko kwenye viwanja vya gezaulole tu. Tanzania imejaa upendeleo kuanzia ngazi ya kijiji, mtaa, kata, mpaka taifa!!!
 
Viwanja 1800 vimeuzwa kwa wananchi. Kati yao, kuna viongozi wa kada mbali mbali, na kuna ndugu zao ama watoto wao. Majina yaliyoorodheshwa ya "wanene" hao ni kama 50.

1800-50= 1750. Tufikirie tu kwamba "walala hoi" 1,750 au hata 1500 wamepata viwanja, na vigogo 300 wamepata pia. Tunalalamika vigogo wamegawana viwanja!

Katika vigogo hao, wana watoto wakubwa tu...namfahamu Juanita Mramba, anafanya kazi benki moja jijini. Naye amenunua kiwanja. Tunalalamika mtoto wa kigogo kauziwa kiwanja? Hivi, wao hawapaswi kuwa na kiwanja simply because baba yake (tu assume tu) ni kigogo na ana viwanja vingine? Kweli hili ni taifa la walalamishi tu...hata tufanyeje.

Ninadhani pengine kama wamekiuka sheria, kwamba vigogo hawakustahili kuuziwa hata mmoja, na kwamba iwe ni kinyume cha sheria kumiliki kiwanja zaidi ya kimoja Tanzania, basi hawa wangekuwa wana makosa. Wengi wetu tumekuwa tunawekeza mno kwenye kulalamika kuliko kutoa maoni ya namna bora ya kuendesha mambo.

Mkuu Mbalamwezi, ukweli usemwe. Upendeleo umefanyika na mchakato haujakuwa wa haki. Hayo majina yaliyotajwa ni baadhi tu na ni kwa wale waliotambuliwa kwa majina yao. Tutoe mfano dada yake Magreth Sitta akiwemo kwenye hiyo list unaweza kumtambua kwa jina lake??? Upendeleo umefanyika na mgao haujawa wa haki hata kidogo, na kinachoudhi zaidi ni kwamba walalahoi wameliwa pesa zao kimagumashi.
Tatizo langu mimi ni pale kizazi cha watanzania kinapokuwa interested na kufuatilia mambo ya kitaifa wakati pale wanapoishi kila siku kwenye mtaa au kijiji kwao pia kuna tabia hizohizo za upendeleo. Hawa viongozi wa kitaifa kuna siku walikuwa viongozi wa wilaya, wakaachwa kujifanyia upendeleo, tabia ikaendelea na sasa imeota mizizi. Ni wajibu wetu sote, kama kweli tunachukia upendeleo na kukosekana kwa uadilifu, kupiga vita ubadhilifu katika ngazi zote, siyo ngazi ya taifa tu na tusisubiri mpaka kitu kiandikwe kwenye gazeti ndio tuanze kukijadili!
 
kuna mambo mawili matatu ambayo wachangiaji wanaogopa kusema:
Jambo la kwanza kuuza fomu 12000 wakati manispaa ikijua ina viwanja takribani 1000 ni wizi wa kimfumo yaani hapa kuna Mamlaka ya Manispaa ambayo imeshindwa kubuni vyanzo vya mapato wakatangaza viwanja wakijua vitagombaniwa na watauza fomu hewa,Manispaa ya Ilala ilitumia mbinu hiyo huko Kinyerezi Kifuru na matokeo eneo lenyewe lina kesi na ada ya fomu ukishailipa hairudishwi.Kwa kujua wana vichache wangeuza Fomu 2000 tu hata kwa shilingi laki moja wangepata fedha na mnunuzi angejua kuwa kama haki inatendeka yamkini ya 1/2 =0.5ya kupata kiwanja ingekuwepo.Yamkini ya 1/12=0.083 ni ndogo mno na hii ni kwa sababu walishakuwa na preferred list!MSINGI WA UKWELI ULIVUNJWA HAPA
Jambo la pili bei ya sh 6000 hadi 12,000 kwa mita ya mraba ya ardhi ni kubwa kwa mtu wa kima cha kati na cha chini anayetaka kumilikishwa ardhi.MSINGI WA USAWA HAPA HAUPO
Jambo la tatu vigezo vya kupata/kukosa ardhi katika inyang'anyiro hiki ni vipi?
Kukosekana kwa vigezo kunatoa mamlaka yasiyohojika kwa wagawaji wa ardhi.Kama vigezo vingetajwa waziwazi ni dhahiri baadhi ya walalamikaji wangeiokoa 30000 zao.UWAZI UMEKIUKWA HAPA
JAMBO la nne kuna kaharufu ka shinikizo la kuwapa viongozi na watu wenye majina fulani fulani ardhi kama mtu akisoma hiyo orodha.HAYA NI MATUMIZI HARAMU YA MADARAKA!
Niwaombe wale wanaoona hakuna tatizo kwenye mazingira haya kama hawajaelewa wanisamehe maana hata wanaotumia miwani kuonea mbali/karibu wana SIZE tofauti za lensi za kusaidia kuonea na mimi hii ni lensi yangu ya kuonea tatizo ,bila hata kuzama sana kwenye utafiti
 
Vigogo waliopata mgawo Viwanja Dar waongezeka
Thursday, 26 July 2012 20:36

Patricia Kimelemeta
Mwananchi

MLOLONGO mrefu zaidi wa majina ya vigogo umebainika kugawiwa viwanja katika eneo la Gezaulole, jijini Dar es Salaam, ambapo safari hii imo familia ya Rais mstaafu wa Awamu ya Pili Ali Hassani Mwinyi.

Jana, gazeti hili lilichapisha katika ukurasa wa mbele habari iliyoonyesha baadhi ya majina ya vigogo waliogawiwa viwanja na kufanya wananchi wa kawaida kulalamika.

Katika uchunguzi zaidi, imebainika kuna orodha ndefu ya majina ya vigogo waliopewa viwanja katika mradi huo wa Gezaulole ambayo inahusisha mawaziri, wabunge, wakuu wa taasisi za Serikali na familia za baadhi ya watu maarufu.

Kwa upande wa familia maarufu, imo ya mzee Mwinyi ambaye pia amegawiwa eneo, wengine wana majina ya ukoo yanayofana na ya kwake ambao ni, Asina Mwinyi, Maimuna Mwinyi, Salama Mwinyi na Steven Ali Mwinyi, huku kutoka katika familia yenye jina la Kikwete yumo Ali J. Kikwete.

Viongozi wengine maarufu waliogawiwa viwanja hivyo ni Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman na Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage, Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emanuel Nchimbi, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Manejimenti ya Utumishi wa Umma), Celina Kombani na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam Malima.

Kwa upande wa watendaji wa taasisi za dola, yumo Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilila, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema, Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Polisi, Clodwig Mtweve, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Misime, Balozi wa Tanzani nchini Afrika Kusini, Radhia Msuya, SACP Hamdan Makame, ACP John Gudaba, ACP Saada Juma Haji na ACP Mohamed Usi.

Mlolongo huo pia unaonyesha majina ya baadhi ya wabunge ambao ni Murtaza Mangungu wa Kilwa Kaskazini (CCM), Mohamed Misanga, (Singida Kusini CCM), Jenister Mhagama (Peramiho CCM), Kheri Ameir (Matemwe, CCM), Kaika Telele (Ngorongoro, CCM), Amina Clement (Koani, CCM) na Ali Hamis Seif (Mkoani, CUF)

Pia kuna orodha ya wabunge wa Viti Maalum CCM ambao ni Subira Mgalu, Alshaiymaa Kweygir, Elizabeth Batenga, Josephine Genzabuke, Betty Machangu, Lediana Mng’ong’o na Mwanakhamis Kassim Said.

Wabunge wengine wa Viti Maalum CCM ni Mariam Mfaki, Mariam Kasembe, Agnes Hokororo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa pamoja na Suzan Kiwanga ambaye ni mbunge wa Viti Maalum, Chadema na Ania Said Chaurembo ambaye ni mbunge mstaafu.

Majina mengine ambayo koo zake ni za watu maarufu ni pamoja na Ahmed Dau, David Kandoro, Asila Ditopile, Alice Koka, Gemini Suchak, Fidelis Owenya, Filoteus Msigwa, Evelyne Manumba, Fatma Ismail Rage, Jamhuri Kihwelo, Issack Mwang’onda, Hijjal Makamba, Joseph Nyambibo, Mbwana Samata, Mohamed Mzimba na Mohamed Mtonga.

Wengine ni pamoja na Masanja Manumba, Mariam Mkama, Mansour Al-Maamry, Onesmo Mtasiwa, Musa Chagonja, Omary Shein, Shimbo Shimbo, Sikitu Kijazi, Solomon Kivuyo, Thomas Nyalile na Aisha Sululu (diwani Jangwani, CCM).

Pia wamo maofisa watatu wa Bunge ambao ni Herman Berege, Anslem Mrema na Theonest Ruhilabake pamoja na mmoja wa maofisa waandamizi ndani ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Boniface Njombe.

Wananchi waja juu
Baadhi ya maofisa wa Manispaa ya Temeke walisema fomu zilizochukuliwa ni zaidi ya 20,000 na kwamba kila fomu ilikuwa ikiuzwa Sh30,000, hivyo kufanya fedha zilizokusanywa kuwa zaidi ya Sh600 milioni.

Tayari mlolongo huo wa majina ya vigogo umesababisha baadhi ya wananchi waliokuwa wakisoma majina hayo kulalamikia mchakato wa utoaji viwanja hivyo, huku wengine wakidai kuwa, warejeshewe fedha zao.

“Tumelipa Sh20,000 kila fomu ya kuombea kiwanja na wananchi tuliojitokeza ni karibu 30,000, lakini majina yanaonyesha kuwa asilimia kubwa ya waliopata ni vigogo ambao tunaamini wana viwanja mahali pengine,” alisema mwananchi mmoja(jina limehifadhiwa).

Mwananchi huyo alisema kuwa, hakukuwa na umuhimu wa kutangaza zabuni hiyo kwa sababu tayari walikuwa na majina yao, hivyo walitakiwa kuwakabidhi viwanja vyao badala ya kuwasumbua na kuwatoza fedha.

“Hali hii inaonyesha kuwa Serikali ipo kwa ajili ya watu wachache, wenye fedha na si wananchi wa kawaida,” aliongeza.

Mwananchi mwingine (jina tunalo), alisema idadi kubwa ya watu waliokabidhiwa viwanja hivyo ni watoto wa vigogo na wabunge.

Aliongeza kuwa hali hiyo inaonyesha wazi kuwa, hakuna kiongozi atakayewatetea wananchi, kwa vile kila mmoja wao yupo kwa ajili ya kupigania maslahi yake.

“Wabunge ambao tuliwategemea kutetea maslahi ya wananchi ndio wanaoongoza kwenye orodha ya kujichukulia viwanja, hii inaonyesha wazi kuwa hakuna kiongozi atakayeacha shughuli zake ili kutetea maslahi ya wananchi,” alisema.

Vyanzo vya habari kutoka ndani ya Manispaa hiyo vinaonyesha kuwa, halmashauri hiyo imeingiza zaidi ya Sh600 milioni kutokana na uuzaji wa viwanja hivyo.
 
Wananchi Tumeanza tambua haki zetu, lakini bado hatujaanza kupambana,
Mjenzi mkuu wa Kigamboni, ni Serikali ya Marekani,

Atajenga Kituo kukubwa, cha Kijeshi chenye, Bandari kubwa, Uwaja mkubwa wa ndege,
Hospitali kubwa, na nyumba za kuishi askari zaidi ya 200,000.

Trilion 16?!! Serikali ya CCM itazinya wapi?? Ili safari ya Mzee Kichaka rais wa Marekani, na zawadi ya vyandarua sijui vya $ M5,
faida yake ni kumegewa kipande cha ardhi, mtakoma na bakuli lenu la umataonya.

Lakini kuna mshiko mkubwa wa karibu $1000,000,000.00 kila mwaka, zitalipwa kama ada ya kunajisi ardhi yetu,
Kuna watu account zao USWIZI zitafura kishenzi.

Mmepigwa sementi ya macho safari hii si changa tena.

Hapo nilipoweka red colour, tumuulize nani atuhakikishie kama masuala hayo ni kweli ndivyo yalivyo??? Wabunge wetu basi wajaribu kuuliza huko bungeni wakati huu wa bunge la bajeti, au kiongozi mkuu wa upinzani amuulize Mhe Waziri Mkuu wakati wa maswali ya papo kwa papo
 
Hakuna wakumwuliza,
Zaidi ya Kikwete,
Kama huamini,
Subiri mpaka wajenge.
Mama wa Liberia aliomba wajenge kwake,
Wakamwambia wana interest na Indian Ocean siyo Atlantic.

One thing hwa jamaa wakisha ingia hawatoki.

Source; Very Skinny BioMosquito

Hapo nilipoweka red colour, tumuulize nani atuhakikishie kama masuala hayo ni kweli ndivyo yalivyo??? Wabunge wetu basi wajaribu kuuliza huko bungeni wakati huu wa bunge la bajeti, au kiongozi mkuu wa upinzani amuulize Mhe Waziri Mkuu wakati wa maswali ya papo kwa papo
 
Mkuu Rejao hii ni mara ya tatu naliwa vihela vyangu; ilala mara moja na temeke mara mbili. Nilikuwa nikiamka usiku na kwenda kupanga foleni lakini wapi wanakuja kupata watu ambao hawakuwepo kwenye foleni! Mkuu hapa kuna wizi wa mchana. Kama wanajua viwanja ni vichache kwa nini wauze maform lukuki? Viwanja havitakiwa kuwa issue ila.wao wanafanya supply iwe scarce ili demand iwe juu na wao kujipatia chochote.
Kimbunga, Naona siku hizi kuuza form za viwanja imekuwa ni njia moja wapo ya source ya revenue kwa manispaa zetu. Wanashindwa kubuni njia mbadala za kujipatia kipato. Nakumbuka vya Kinyerezi mpaka leo sijui kinachoendelea. najutia kwanini niliapply. Kuhusu idadi ya fomu, kumbuka pia kama zingetolewa form chache watu wangelalamika. Cha muhimu hao wagawaji wawe fair kwenye ugawaji.
 
Last edited by a moderator:
Hakuna wakumwuliza,
Zaidi ya Kikwete,
Kama huamini,
Subiri mpaka wajenge.
Mama wa Liberia aliomba wajenge kwake,
Wakamwambia wana interest na Indian Ocean siyo Atlantic.

One thing hwa jamaa wakisha ingia hawatoki.

Source; Very Skinny BioMosquito

During the Sept. 12, 2011, Republican presidential debate in Tampa, Rep. Ron Paul, R-Texas -- a staunch advocate of limited government and a more modest military footprint -- offered a surprising statistic about the reach of the U.S. armed forces. "We're under great threat, because we occupy so many countries," Paul said. "We're in 130 countries. We have 900 bases around the world. We're going broke. The purpose of al-Qaida was to attack us, invite us over there, where they can target us. And they have been doing it. They have more attacks against us and the American interests per month than occurred in all the years before 9/11, but we're there occupying their land. And if we think that we can do that and not have retaliation, we're kidding ourselves. We have to be honest with ourselves. What would we do if another country, say, China, did to us what we do to all those countries over there?" Wakijenga hapa kwetu tutakuwa moja kati ya nchi nyingi wanakosema wana makambi!!!!

Source: PolitiFact | Ron Paul says U.S. has military personnel in 130 nations and 900 overseas bases
 
Vigogo waliopata mgawo Viwanja Dar waongezeka

Thursday, 26 July 2012

MLOLONGO mrefu zaidi wa majina ya vigogo umebainika kugawiwa viwanja katika eneo la Gezaulole, jijini Dar es Salaam, ambapo safari hii imo familia ya Rais mstaafu wa Awamu ya Pili Ali Hassani Mwinyi.

Jana, gazeti hili lilichapisha katika ukurasa wa mbele habari iliyoonyesha baadhi ya majina ya vigogo waliogawiwa viwanja na kufanya wananchi wa kawaida kulalamika.

Katika uchunguzi zaidi, imebainika kuna orodha ndefu ya majina ya vigogo waliopewa viwanja katika mradi huo wa Gezaulole ambayo inahusisha mawaziri, wabunge, wakuu wa taasisi za Serikali na familia za baadhi ya watu maarufu.

Kwa upande wa familia maarufu, imo ya mzee Mwinyi ambaye pia amegawiwa eneo, wengine wana majina ya ukoo yanayofana na ya kwake ambao ni, Asina Mwinyi, Maimuna Mwinyi, Salama Mwinyi na Steven Ali Mwinyi, huku kutoka katika familia yenye jina la Kikwete yumo Ali J. Kikwete.

Viongozi wengine maarufu waliogawiwa viwanja hivyo ni Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman na Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage, Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emanuel Nchimbi, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Manejimenti ya Utumishi wa Umma), Celina Kombani na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam Malima.

Kwa upande wa watendaji wa taasisi za dola, yumo Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilila, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema, Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Polisi, Clodwig Mtweve, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Misime, Balozi wa Tanzani nchini Afrika Kusini, Radhia Msuya, SACP Hamdan Makame, ACP John Gudaba, ACP Saada Juma Haji na ACP Mohamed Usi.

Mlolongo huo pia unaonyesha majina ya baadhi ya wabunge ambao ni Murtaza Mangungu wa Kilwa Kaskazini (CCM), Mohamed Misanga, (Singida Kusini CCM), Jenister Mhagama (Peramiho CCM), Kheri Ameir (Matemwe, CCM), Kaika Telele (Ngorongoro, CCM), Amina Clement (Koani, CCM) na Ali Hamis Seif (Mkoani, CUF)

Pia kuna orodha ya wabunge wa Viti Maalum CCM ambao ni Subira Mgalu, Alshaiymaa Kweygir, Elizabeth Batenga, Josephine Genzabuke, Betty Machangu, Lediana Mng’ong’o na Mwanakhamis Kassim Said.

Wabunge wengine wa Viti Maalum CCM ni Mariam Mfaki, Mariam Kasembe, Agnes Hokororo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa pamoja na Suzan Kiwanga ambaye ni mbunge wa Viti Maalum, Chadema na Ania Said Chaurembo ambaye ni mbunge mstaafu.

Majina mengine ambayo koo zake ni za watu maarufu ni pamoja na Ahmed Dau, David Kandoro, Asila Ditopile, Alice Koka, Gemini Suchak, Fidelis Owenya, Filoteus Msigwa, Evelyne Manumba, Fatma Ismail Rage, Jamhuri Kihwelo, Issack Mwang’onda, Hijjal Makamba, Joseph Nyambibo, Mbwana Samata, Mohamed Mzimba na Mohamed Mtonga.

Wengine ni pamoja na Masanja Manumba, Mariam Mkama, Mansour Al-Maamry, Onesmo Mtasiwa, Musa Chagonja, Omary Shein, Shimbo Shimbo, Sikitu Kijazi, Solomon Kivuyo, Thomas Nyalile na Aisha Sululu (diwani Jangwani, CCM).

Pia wamo maofisa watatu wa Bunge ambao ni Herman Berege, Anslem Mrema na Theonest Ruhilabake pamoja na mmoja wa maofisa waandamizi ndani ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Boniface Njombe.

Wananchi waja juu
Baadhi ya maofisa wa Manispaa ya Temeke walisema fomu zilizochukuliwa ni zaidi ya 20,000 na kwamba kila fomu ilikuwa ikiuzwa Sh30,000, hivyo kufanya fedha zilizokusanywa kuwa zaidi ya Sh600 milioni.

Tayari mlolongo huo wa majina ya vigogo umesababisha baadhi ya wananchi waliokuwa wakisoma majina hayo kulalamikia mchakato wa utoaji viwanja hivyo, huku wengine wakidai kuwa, warejeshewe fedha zao.

“Tumelipa Sh20,000 kila fomu ya kuombea kiwanja na wananchi tuliojitokeza ni karibu 30,000, lakini majina yanaonyesha kuwa asilimia kubwa ya waliopata ni vigogo ambao tunaamini wana viwanja mahali pengine,” alisema mwananchi mmoja(jina limehifadhiwa).

Mwananchi huyo alisema kuwa, hakukuwa na umuhimu wa kutangaza zabuni hiyo kwa sababu tayari walikuwa na majina yao, hivyo walitakiwa kuwakabidhi viwanja vyao badala ya kuwasumbua na kuwatoza fedha.

“Hali hii inaonyesha kuwa Serikali ipo kwa ajili ya watu wachache, wenye fedha na si wananchi wa kawaida,” aliongeza.

Mwananchi mwingine (jina tunalo), alisema idadi kubwa ya watu waliokabidhiwa viwanja hivyo ni watoto wa vigogo na wabunge.

Aliongeza kuwa hali hiyo inaonyesha wazi kuwa, hakuna kiongozi atakayewatetea wananchi, kwa vile kila mmoja wao yupo kwa ajili ya kupigania maslahi yake.

“Wabunge ambao tuliwategemea kutetea maslahi ya wananchi ndio wanaoongoza kwenye orodha ya kujichukulia viwanja, hii inaonyesha wazi kuwa hakuna kiongozi atakayeacha shughuli zake ili kutetea maslahi ya wananchi,” alisema.

Vyanzo vya habari kutoka ndani ya Manispaa hiyo vinaonyesha kuwa, halmashauri hiyo imeingiza zaidi ya Sh600 milioni kutokana na uuzaji wa viwanja hivyo.

Source: Mwananchi
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom