Vigogo wagawana viwanja vya Gezaulole | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vigogo wagawana viwanja vya Gezaulole

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ihs, Jul 26, 2012.

 1. ihs

  ihs Member

  #1
  Jul 26, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana Jamii,

  Tumekua tukiona mwenendo mzima wa ugawaji wa viwanja hapa nchini hususan hapa Dar, umejaa utapeli, unafiki, uzandiki na wizi wa waziwazi. Tunatumika kukusanya hela za wananchi wadogo na wanaopewa viwanja kwa kutumia hizo hela za walalhoi ni watu ambao wana majumba zaidi ya manne, na wengine hawajui hata sebule za nyumba zao nyingine zikoje.

  Huu ni udhalimu dhidi ya wananchi wadogo, na hakuna wa kututetea - lazima tukae tukubaliane na tuseme imetosha, la sivyo wajukuu zetu kama si wattoto wetu wote wataishia kua ma houseboy na mahousegirl wa rulling elite.

  The rulling elite ya hapa kwetu is trhe most corrupt elite katika africa nzima, ila woga wa wananchi umefanya tuonekane tuna afadhali lakini ni uanfiki mtupu.

  Watu wana miliki viwanja mpaka 20 wengine 30, wanaviuza milion 15 mpaka milion 20. Wao hawajalipia chochote, wanafanya biashara ya kuuza watu. Wanatuuza sisi na watoto wetu na wajukuu zetu.

  Ingekua sio unafiki wetu, tungewaruhusu wao wakubwa wapimiwe vyakwao kwanza wakishachukua watuachie na sisi wadogo tupate, lakini huu unafiki wa kutuchanganya nao - eti kwa kete ya usawa wa binadamu, utatutafuna mpaka tunaingia kaburini.

  The rulling elite are evils, they are not human being like us and they have no empathy at all.

  tukusubiri watuonee huruma, utashangaa watatuchinja na damu yetu watoe kafara baharini au kwa baphomet ili wapate kuendelea na mamlaka ya hapa duniani mpaka mwanga wa juu utakavyotuwakia tena.

  Wananchi, kama tukishindwa kupambana na huu udhalimu - basi angalau tuanze kuchonga majeneza yetu. Tusifikirie tutazikwa wapi, kiwanja cha kuzikiwa hutopata. Anyway, it doesn,t matter at all.

  Illuminati never lies, they rely on great deception and we are the one who perceives it to be the reality. Whose to blame?

  The Great and brutal fascism state and colonialisim in this country is yet to come. The rulling elite are not yet big eneough to burst.

  Aluta Continua!
   
 2. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Ni wizi wa hali ya juuu, nadhani kwa isu ya temeke lazima tuwape wabunge wa upinzani hii hoja... kwa mpano wamekusanya fedha za form 12,000 ambapo kila moja waliuza 30,000/= hapo wanapata zaidi ya 360,000,000/=. wamegawa viwanja 1,040 tu na tu fanye assuption ya kuwa vyote vimeuzwa kwa bei ya chini kabisa ambay ilikiwa Tsh 4,800,000 wanepata 4,992,000,000 sasa hii nidhuruma kabisa
   
 3. Zinedine

  Zinedine JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,189
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Weka Orodha kwanza ya wote waliopata ili tujue ikiwa ni wakubwa watupu au akina "maimuna' pia wapo waliopata!
   
 4. M

  Madcheda JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2012
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 416
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Tuache utani 30,000 yangu INANIUMA SANA!Tanzania imekua pango la wanyang'anyi yani viwanja vyote vya geza ulople wamewapa makatibu wakuu,wabunge,watoto wa maraisi,mawaziri na vigogo wengine wengi! Kweli aliyenacho ataongezewa msemo huu umetimia Tanzania ya Nyerere!

  Kifupi viwanja wamepata wakina CAG,ndugai, miraji kikwete,kijja etc
   
 5. Zinedine

  Zinedine JF-Expert Member

  #5
  Jul 26, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,189
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ungeliweka orodha ya wote waliopata ingekuwa vema sana
   
 6. saragossa

  saragossa JF-Expert Member

  #6
  Jul 26, 2012
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 2,141
  Likes Received: 147
  Trophy Points: 160
  Wapo akina meghji, mary mwanjelwa,wilson mukama, na wengine wengi. Nimeisikia listi kwenye power breakfast Clouds asubuhi hii. Balaa!
   
 7. Kabembe

  Kabembe JF-Expert Member

  #7
  Jul 26, 2012
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 2,236
  Likes Received: 928
  Trophy Points: 280
  Katika miradi yote ya upimaji viwanja wilaya ya Temeke kuna majina ya waliopata yanajirudia kila allocations zinapofanyika,yaani wanapata wao tu! I just don't get it!
   
 8. w

  wikolo JF-Expert Member

  #8
  Jul 26, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 801
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Vigogo wagawiwa viwanja Dar
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Wednesday, 25 July 2012
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  WALALA HOI WALALAMIKA, WALITOA SH30,000 ZA MAOMBI ‘ZIMEENDA NA MAJI'

  MANISPAA ya Temeke imetoa orodha ya majina ya wananchi waliopewa viwanja katika manispaa hiyo, ambayo inaonyesha kuwamo kwa vigogo wanaojumuisha mawaziri, wabunge, watendaji wakuu wa Serikali pamoja na baadhi ya watoto wa vigogo hao.Katika orodha hiyo, jumla ya watu 1,800 walipatiwa viwanja hivyo, huku majina hayo ya vigogo yakiwa ni zaidi ya 50, ambao baadhi wamejiandikisha wenyewe, wengine wake zao, ndugu na watoto wao.

  Majina hayo ambayo gazeti hili iliyaona jana, yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo wa manispaa hiyo, ili wananchi walioomba viwanja hivyo waweze kuangalia kama wamo katika orodha ya waliopatiwa viwanja hivyo.

  Baadhi ya wananchi waliofika kusoma majina hayo walisikika wakilalamikia hali hiyo, huku wakisema kuwa kinachoonekana ni vigogo kupendelewa na kuwanyima wananchi wa kawaida.

  Katika orodha hiyo, majina yanayosomeka ni pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama; Naibu Spika, Job Ndugai; Waziri wa Mawasiliano, Sanyansi na Teknolojia, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima.

  Kwa upande wa Makatibu Wakuu wa Wizara wapo, Dk Florence Turuka (Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Ramadhan Kijjah; Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Omary Chambo na Dk Idris Rashid ambaye ni Gavana wa Zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

  Pia wamo Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk Didas Masaburi, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa; Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam, Suleinan Kova.

  Wengine ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Haruna Masebu; Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh na Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH),Marina Njelekela.

  Kwa upande wa wabunge wamo Dk Augustine Mrema (Vunjo - TLP), Mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe; Mbunge wa Kibaha Mjini (CCM), Sylvester Koka; Mbunge wa Kinondoni (CCM), Idd Azzan; Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), Dk Cyril Chami na Mbunge wa Singida Kusini (CCM), Mohamed Misanga.

  Wengine ni Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila; Mbunge wa Igunga (CCM), Dk Peter Kafumu na Mbunge wa Bukene (CCM), Seleman Zedi.

  Wabunge wa Viti Maalumu (Chadema), Maulida Komu na Suzan Lyimo, Viti Maalumu CCM, Dk Mary Mwanjelwa na Zakhia Meghji ambaye ni mbunge wa kuteuliwa.

  Orodha hiyo pia inaonyesha majina ya ukoo yanayofanana na majina ya baadhi ya viongozi ambao ni Miraji Kikwete, Khalfan Kikwete, Juanita Mramba, Suzan Mkapa, Zainab Mkomwa, George Rupia, Maimuna Mfutakamba, Mary Membe, Pharles Ngeleja, Judith Kahama na Wilfred Mwanri.

  Mkurugenzi apatwa kigugumizi
  Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Magreth Nyalile alipoulizwa kuhusu orodha hiyo alisema kuwa, majina hayo hajayaona na kwamba waliobandika wamefanya uamuzi huo bila ya yeye kuupitia.

  "Majina yenyewe sijayaona, hivyo basi siwezi kujua ni kina nani waliopewa viwanja hivyo, kwa sababu wako zaidi ya 1,000, jambo ambalo litakuwa vigumu kwangu kubaini tatizo hilo," alisema Nyalile.

  Aliongeza kuwa, kutokana na hali hiyo hawezi kusema lolote kwa sababu yuko nje ya ofisi kwa ajili ya shughuli nyingine za ujenzi wa taifa.

  Hata hivyo, Nyalile alisema mchakato wa ugawaji wa viwanja hivyo ulifuata taratibu za kisheria na kwamba hakuna mtu au kiongozi yeyote aliyependelewa, jambo ambalo linaweza kusababisha mgongano wa hapa na pale.

  Nyalile alisema kuwa kama kuna viongozi walipewa kwa njia zisizo sahihi, au kwa rushwa wakati wa uwasilishaji wa majina hayo, walipaswa kutoa taarifa kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

  Wananchi walalama

  Baadhi ya wananchi walikuwa wakiangalia majina hayo katika ubao huo walidai kuwa, baadhi ya maofisa wa halmashauri hiyo wamedaiwa kupewa rushwa wakati wa ugawaji wa viwanja hivyo.

  "Walitangaza kama kiini macho, lakini tayari walikuwa na majina yao ili waweze kuwapatia na jambo ambalo limejionyesha wazi kwenye majina ya watu waliopewa viwanja hivyo," alisema mwananchi mmoja (jina tunalihifadhi) na kuongeza:

  "Kutokana na hali hii, hatuna imani na viongozi wowote wa Serikali kwa sababu inaonyesha wazi kuwa, kila mmoja anaangalia masilahi yake na si wananchi wasio na kipato".

  Aliongeza kuwa, wananchi hawana imani na viongozi wao, hivyo Serikali inapaswa kuingilia kati kwa sababu hali hiyo inaweza kusababisha matatizo.

  Mwananchi mwingine aliyekuwa akifuatilia jina lake alisema: "Wewe unachokiona ni nini hapo kama siyo yaleyale ya ubinafsi! Wewe unaamini kabisa kwamba kweli hawa viongozi wetu hawana nyumba au hawana viwanja hapa Dar es Salaam.

  Aliongeza: "Kama manispaa walitangaza viwanja ili wajiuzie wangesema tu badala ya kuchukua fedha zetu Sh30,000 halafu viwanja wakajigawia wenyewe."

  Mgawo wa Viwanja

  Mapema mwezi Juni mwaka huu, Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ilitangaza kwamba imepima viwanja 1,800 katika eneo la Gezaulole ikiwa ni mwendelezo wa utekelezaji wa Mradi wa Upimaji Viwanja.

  Fomu za maombi ya kununua viwanja hivyo zilianza kutolewa Juni 11 na kila mwombaji alipaswa kulipia ada ya maombi ya kiasi cha Sh30,000 katika ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke iliyopo mkabala na Uwanja Taifa jijini Dar es Salaam.

  "Fedha hizo hazitarejeshwa na mwombaji atajaza nakala mbili za fomu ya maombi na kuzirejesha zikiwa zimebandikwa picha 3 za ukubwa wa pasipoti. Mwisho wa kurudisha fomu hizo ni tarehe 18.06.2012 saa 8 mchana," linasomeka tangazo rasmi la manispaa hiyo.

  Wakazi wenye nyumba na mashamba ndani ya eneo la mradi ambao walikuwa wametambuliwa kabla ya zoezi la upimaji kuanza, pia walitakiwa kununua fomu za maombi kwa utaratibu uleule.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Source: Mwananchi

  My Take: Ina maana hawa viongozi waliopatiwa hivyo viwanja hawana makazi kwa sasa au wanachukua kama ziada tu?
   
 9. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #9
  Jul 26, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Kama wamefuata masharti na ni watanzania, sioni tatizo.
   
 10. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #10
  Jul 26, 2012
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  pia kuna waheshimiwa wabunge wa vyama pendwa kama NCCR....TLP.....CHADEMA. na CCM
   
 11. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #11
  Jul 26, 2012
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  AZIMIO LA ARUSHA ambalo tulilipiga teke kwa nderemo na vifijo bado linahitajika
   
 12. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #12
  Jul 26, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,282
  Likes Received: 1,432
  Trophy Points: 280
  Sishangai kabisa kuona hayo majina. Bei ya hivyo viwanja ilikuwa ni Tshs 12,000,000/=, mwananchi gani wa kawaida angemudu hiyo bei?
   
 13. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #13
  Jul 26, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Hii nchi hii! Ipo siku.
   
 14. k

  kafundi Member

  #14
  Jul 26, 2012
  Joined: Jun 2, 2012
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi kwani wao hawana haki ya kuomba na kupewa viwanja?
   
 15. Kabembe

  Kabembe JF-Expert Member

  #15
  Jul 26, 2012
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 2,236
  Likes Received: 928
  Trophy Points: 280
  Ubinafsi unaliangamiza taifa hili,hao wanaotumia surname ya Kikwete wameappear Katika kila mradi uliofanyika Temeke tangu walipoanza kupima viwanja Kigamboni.
   
 16. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #16
  Jul 26, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Ndio bei yake ilikuwa hivyo? Kweli akina siye tusingeweza.....
   
 17. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #17
  Jul 26, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Viwanja vilikuwa vingapi? Hapo huu waliotajwa ni 39 tu. Ina maana viwanja vilikuwa hivyo tu au gazeti limeamua kuorodhesha vigogo tu? Nao si watanzania na hivyo wanastahili kupata viwanja hivyo? Tafadhali tupate na walalahoi waliopata ili kuona uwiano uliopo ndipo tuweze kutoa maoni yetu.
   
 18. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #18
  Jul 26, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Wana haki lakini pale inapotokea miradi ya viwanja inapotokea yanakuwepo majina yaleyale lazima tuwe na mashaka.
   
 19. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #19
  Jul 26, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280  hii hapa
   
 20. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #20
  Jul 26, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Nani wa kulirudisha?
   
Loading...