Vigogo wagawana viwanja vya Gezaulole

Vigogo wagawana viwanja vya Gezaulole

Mimi nawashangaa watu wanavyokimbilia manispaa kuweka booking ya viwanja ambavyo hawana uhakika wa kuvipata wakati manispaa hiyo hiyo imeshazipa idhini kampuni binafsi zifanye hiyo kazi ya upimaji na uuzaji viwanja kwa niaba ya manispaa hizo. Mfano Temeke hivi majuzi tena baada ya hivi viwanja vya gezaulole; kupitia kampuni ya Ardhi Plan wameuza viwanja vingine huko huko kigamboni, vimeunzwa kiustaarabu hadi raha, mtu unapata nafasi ya kuona ramani ya eneo, unachagua kiwanja unapelekwa eneo kiwanja kilipo unaliona eneo physically then unafanya maamuzi ya kununua au la. na bei ni hizo hizo za manispaa.
 
poleni sana.
namkumbuka yule meneja wa viwanja 20,000 aliyefariki.mradi wake ulitubeba tusio nacho bila hata kumjua mtu nakumbuka nililipa kwa instalment 3 kiwanja cha shillingi 780,000.00 lakini nakumbuka watu wakati tunanunua huko walikuwa wanatucheka tunanunua kwa waswahili na vilikaa wazi zaidi ya miaka 3 sasa leo kumeshabadilika na wakati ule hata ukitaka kumi unapewa bila mizengwe wala rushwa.kilichotakiwa ni kwenda ofisi ya temeke au ilala.
nakumbuka kuna wakili mmoja nilimshawishi mimi kwenda na umuhimu wa kiwanja ndo akatoka na baada ya masaa machache akaniambia kapata.
maskini tujipange kwa maeneo mapya lakin kigamboni si kwenu tena vinginevyo tafuta 20mill
 
Hayo ndio matokeo ya serikali kandamizi; Pesa zilizopatikana (360,000,000/-) zilitosha kabisa kuwapimia viwanja watu wote walioomba!,....
Hebu tujiulize maswali yafuatayo alafu utaelewa ninayosema;

1. Kupima kiwanja kimoja inagharimu kiasi gani?
2. Je hakuna watu waliojariwa kwa ajiri ya kazi hiyo na kila mwezi wanalipwa mshahara?
3. Kwa nini mtanzania maskini analipishwa fomu ya kiwanja kwa shilingi elfu thelasini, alafu mwishop wa siku ananyimwa kiwanja?
4. Je viwanja vyote vimeisha pimwa na kujaa huko kigambon?

Me nadhani watanzania tunapuuzia sana mambo, hivi kweli tunauziwa prited fomu kwa shilingi 30,000/- alafu mwisho wa siku hatupati chochote kutokana na hiyo fomu!!!, huu si wizi wa mchana mchana jamani!..... I think we have to be more serious!
 
Muhimu waliopata viwanja wajenge nyumba siyo kuvigeuza mapori. Kuna viwanja walipewa mawaziri na wabunge kule Bunju. Mpaka sasa ni machaka,waliojenga ni wachache sana. Naamini baadhi yao ni hawa wamepewa tena vya Gezaulole.
 
Ndio maana wanakuwa wakali wanachi wa Kigamboni wakitaka fidia kwa bei ya soko wao wameshajipatia.....:nerd:
 
Kimbunga, Naona siku hizi kuuza form za viwanja imekuwa ni njia moja wapo ya source ya revenue kwa manispaa zetu. Wanashindwa kubuni njia mbadala za kujipatia kipato. Nakumbuka vya Kinyerezi mpaka leo sijui kinachoendelea. najutia kwanini niliapply. Kuhusu idadi ya fomu, kumbuka pia kama zingetolewa form chache watu wangelalamika. Cha muhimu hao wagawaji wawe fair kwenye ugawaji.

Mkuu nina machungu kwa kuwa hata Kinyerezi walinilamba!
 
Viwanja vya Kinyerezi walikula hela yangu , this time nikasoma mchezo nikasema hawanipati NG'O

Mkuu Kinyerezi walinilamba, ikaja Gezaulole phase 1 wakanilamba. Jamaa mmoja wa pale manispaa akaniambia phase 1 walikuja wabunge, madiwani, nk. wakachukua viwanja sasa phase 2 vingekuwa vingi na sisi walalahoi tungepata; basi nikajitosa kichwakichwa, hawakunionea huruma wamelamba tena! Uchungu kweli inakuwa kama bahati na sibu.
 
You are right GREED, Uchoyo, Uroho, Ufisi.
Watemi wale wa kale,
walitamani shanga na nguo,
Ardhi kwa shanga za ulanga.

Leo Kikwete Lowassa Chenge,
nao pia watamani shanga,
Shangingi suti pande tatu,
Ardhi kwa shangingi na gagulo,
Elimu haijawatoa tongo,
historia mfukoni swekani.

Historia yajirudia tena na tena na tena,
ujinga ule ule matamanio ya umauti.


greedy!!!!!!!!!
 
Si wewe pekee yako,
WaTanzania ote tumepanga,
foleni ya matumaini,
Wao wanaiba leo,
sisi tutaiba kesho.

Tuko ujingani, twajidanganya mchana kweusi.
Dawa ni kuwapandia huko huko.
Kwa nini tusikusanya hati zetu, tukaziweka online?
kwa nini tusiweka picha na majina ya watendaji wote online?
kwanini tusiwarekodi na kuweka ujinga wao online?

Tuna Internet tuitumie kwa manufaa yetu.

Mkuu Kinyerezi walinilamba, ikaja Gezaulole phase 1 wakanilamba. Jamaa mmoja wa pale manispaa akaniambia phase 1 walikuja wabunge, madiwani, nk. wakachukua viwanja sasa phase 2 vingekuwa vingi na sisi walalahoi tungepata; basi nikajitosa kichwakichwa, hawakunionea huruma wamelamba tena! Uchungu kweli inakuwa kama bahati na sibu.
 
Back
Top Bottom