Vigogo wagawana viwanja vya Gezaulole

Rais mstaafu, tunamlipa mihela yote kumtunza, bado ananyang'anyana viwanja na sisi makapuku? Mbona hawa mafisi watatumaliza!
 
Kimbunga, Naona siku hizi kuuza form za viwanja imekuwa ni njia moja wapo ya source ya revenue kwa manispaa zetu. Wanashindwa kubuni njia mbadala za kujipatia kipato. Nakumbuka vya Kinyerezi mpaka leo sijui kinachoendelea. najutia kwanini niliapply. Kuhusu idadi ya fomu, kumbuka pia kama zingetolewa form chache watu wangelalamika. Cha muhimu hao wagawaji wawe fair kwenye ugawaji.
Kinyerezi Ilala wamekwama kwa sababu,walilileta mradi kihuni bila kupatana na wenye maeneo yao,hivyo wakawapeleka mahakamani,na mahakama kuu ikawapiga stop manispaa ya ilala kukanyaga Kinyerezi na kusimamisha zoezi lote la
upimaji na uuzaji viwanja.
 
And Temeke is still ngome imara ya magamba. Sijui tuwasaidieje?
 
is this an apology or a comment


DO YOU REAL KNOW THE DIFFERENCE BETWEEN THE TWO?

Apology is an admission for being guilty or a request for forgiveness
Comment a remark, observation, or criticism

THEN CHOOSE FOR URSELF. MIMI NI9 EXPERT KATIKA ENEO HILI LA MASUALA YA ARDHI. SASA KAMA UNADHANI KUELEWESHWA NI KUWA GUILTY THEN ITS AN APOLOGY OTHERWISE I WAS GIVING SOME CRITIQUES ON UR STATEMENT. NEXT TIME MAKE IT CLEAR BEFORE U PROVIDE ANY PIECE OF INFORMATION
 
wapo waliokosa kabisa ambao hata kiwanja kimoja hawana....wht are u talkinng..talk sense...kinachopimwa hapa ni tamaa. hakuna tamaa nusu...tamaaa ni tamaa tu....kama una viwanja 20; nyumba ya serikali umeuziwa tena kwa bei ya kutupa; vyeo mnagawana; kazi za umma mnagawana; makampuni ya umma mnauziana; bado mnakuja huku uswahili kwetu kugombania viota.......huu ni unyang'au
Mkuu hasira hizi, toa somo kwa mama zetu na wazee wetu vijiji wape somo la umuhimu wa uchaguzi sahihi. Majina hayo ni machache kuna kina angela kizigha na shyrose banji wa bunge la afr mash. Wapo madiwani na familia zao, watendaji wakuu wa manispaa, familia na rafiki wa vigogo wa serikali. Hasira kali inatia kichefuchefu
 
Wabunge wetu ambao ndiyo tunawategemea watutetee sisi wananchi hao hao ndiyo wanagawana viwanja pamoja na familia zao.
 
Hawa jamaa wa manispaa hovyo kabisa. Wanatuuzia form tena unapanga foleni kuanzia saa kumi usiku lakini kiwanja hupati. Huu ni wizi wa mchana kweuupe. Sipendi

Viwanja vya Kinyerezi walikula hela yangu , this time nikasoma mchezo nikasema hawanipati NG'O
 
DO YOU REAL KNOW THE DIFFERENCE BETWEEN THE TWO?

Apology is an admission for being guilty or a request for forgiveness
Comment a remark, observation, or criticism

THEN CHOOSE FOR URSELF. MIMI NI9 EXPERT KATIKA ENEO HILI LA MASUALA YA ARDHI. SASA KAMA UNADHANI KUELEWESHWA NI KUWA GUILTY THEN ITS AN APOLOGY OTHERWISE I WAS GIVING SOME CRITIQUES ON UR STATEMENT. NEXT TIME MAKE IT CLEAR BEFORE U PROVIDE ANY PIECE OF INFORMATION

Expert can not criticize something unclear to him/her. He does that after proving beyond doubt that the issue at hand needs to be critisised. At least am am an expert in nothing and therefore I can not differentiate the two.
 
Mie wamekula pesa yangu ya majina matano sina hamu hata nisikie kuna viwanja vya kulipia 5000 sitaki.

duh!we ni halali kuliwa kabisa!
Yaani ulikuwa unataka viwanja vitano!duhhhh!kumbe ufisadi upo hata kwa wananchi!!!
Eh!ukistaaajab ya kundule utayaona ya nyani!....
 
Hili gazeti limepotoshwa umma; Vigogo waliopata viwanja ni 39 ama 2.16% ya watu 1,800 waliopata viwanja. Wasio vigogo ni wengi kuliko vigogo. Watz msiwe na kasumba ya kubwabwaja pasipo kuingia ndani kwa hoja

Angalia from a different angle. Kama priority ilikuwa ni kwa wasio na viwanja kabisa hapa Dar, Je kati ya hao vigogo ni yupi unaweza kusema hana kiwanja(kama sio viwanja) hapa Dar. Kwa upande mwingine ni wangapi wasio na viwanja kabisa wamekosa!!!
 
kinachopingwa ni utaratibu usiojulikana. Kama vipi maombi yote yangeingizwa kapuni halafu tuchezeshe bahati nasibu tena live. Kwa vile vigezo havijulikani kwa nini mtu amepata ndio chanzo cha malalamiko. tulisikia mapema watu wakiambiwa watoe mil 5 ili wapate viwanja. Kwa hiyo kuna baadhi ya watu ambao majina hayajulikani ila wametoa kitu kidogo.
 
well said
Kumbuka kuwa hao vigogo walipeleka na majina ya watoto/ndugu/rafiki zao na pia kuna viwanja cilivyochukuliwa na mashika mbalimbali kwa mfano TBA(Tanzania building agency), benki iliyoikopesha manispaa, wizara mbalimbali, Ikulu n.k. Viwanja vilivyobaki kwa wananchi wa kawaida ni vichache sana. Kama unaweza kujiuliza katika zaidi ya watu 30,000 walioomba iweje majina hayo ya vigogo yaonekane zaidi wakati kuna wananchi wenye uwezo wa kulipa.
 
Back
Top Bottom