Vigogo wagawana viwanja vya Gezaulole

Vigogo wagawana viwanja vya Gezaulole

Mimi nacholalamika ni kuwa kwa vile manispaa imeshaona mahitaji basi ipime viwanja vingi wale wanaokoswa wawe kwenye waiting list ya vinavyofuata. Kama wanavyofanya national housing. Mbona mradi ulipoanza hatukuwa na hili tatizo? Ni kwa vile walipima vingi na kuuza kwa wakati mmoja. Ila viongozi ni raia wana haki ya kupata viwanja kwa utaratibu wa haki kwa raia wote
 
the listener,

mita moja ya mraba iliuzwa kwa kama sh 8000 sasa kama unataka sqm 400 manake hapo ni 3,200,000, sasa hapa kweli mlalahoi amezingatiwa?

ndugu maundumula mimi nakubaliana na wewe kabisa kwamba mwananchi wa kawaida hakuzingatiwa kabisa. Bado hiki kiasi ni kikubwa kwake na wala hakiwezekaniki
 
Acheni kupiga kelele kuhusu viwanja vya gezaulole.

Utaratibu uliofutwa ni kutoa kipaumbele kwa yule aliyeonyesha uwezo mkubwa wa kununua kiwanja; katika fomu za maombi kulikuwa na kipengele cha kuonyesha WEWE UKO TAYARI KUNUNUA KIWANJA KWA KIASI GANI??
Hivyo mwenye kuweka KIWANGO KIKUBWA KAPEWA KIPAUMBELE, katika hali ya kawaida KATIBU MKUU HAZINA hawezi kuweka dau ndogo!!! Kwa hiyo usishangae Bw. Khija Kupata kipaumbele

Aisee.. mkuu hicho kipengele kweli kiboko! inaonyesha walitaka watu fulani fulani tu
 
Viwanja vilikuwa vingapi? .Hapo huu waliotajwa ni 39 tu Ina maana viwanja vilikuwa hivyo tu au gazeti limeamua kuorodhesha vigogo tu? Nao si watanzania na hivyo wanastahili kupata viwanja hivyo? Tafadhali tupate na walalahoi waliopata ili kuona uwiano uliopo ndipo tuweze kutoa maoni yetu.

soma habari tena na uache uvivu wa kusoma
 
Mimi nacholalamika ni kuwa kwa vile manispaa imeshaona mahitaji basi ipime viwanja vingi wale wanaokoswa wawe kwenye waiting list ya vinavyofuata. Kama wanavyofanya national housing. Mbona mradi ulipoanza hatukuwa na hili tatizo? Ni kwa vile walipima vingi na kuuza kwa wakati mmoja. Ila viongozi ni raia wana haki ya kupata viwanja kwa utaratibu wa haki kwa raia wote

mAJINA YAO YAMEKUWA YAKIJIRUDIA RUDIA KILA MGAO UNAPOTOKEA NA HAPO NDIPO WATANGANYIKA WANAPOLALAMIKIA. SUALA LA WAITING LIST HAPA KWETU TANGANYIKA LINAHITAJI DISCLIPINE YA HALI YA JUU KWANI WATU WANANUNUA HATA HIYO 'FOLENI' ILI WATOKE KWANZA WAO KABLA YA WALIOWAHI. KUNA SUALA MOJA KUBWA LILILO NYUMA YA PAZIA JUU YA UPIMAJI WA VIWANJA VINGI KWA WAKTI MMOJA. KULIPA FIDIA NI MOJA KATI YA ELEMENTS ZA MRADI WOWOTE UNAOHUSIANA NA UPIMAJI WA VIWANJA. HAPA NDO HUWA PANA TATIZO KUBWA KWANI ZAIDI YA NUSU YA PESA YOTE YA VIWANJA HUWA NI KWA AJILI YA KULIPA FIDIA. VIONGOZI WANAPASWA KUWA NA NIA YA DHATI KUFANYA MAAMUZI SAHIHI JUU YA KAZI HII. NAKUMBUKA WIZARA YA ARDHI ILIWEZA MIAKA YA MWANZONI MWA 2000 KATIKA MTRADI WAO WA VIWANJA 20,000 NA NAKUMBUKA VILIKUWA VINAUZWA KWA BEI RAHISI SANA HADI KATIKA MAONYESHO YA SABASABA LAKINI WATANGANYIKA HATUKUVINUNUA AMA KWA UWEZO MDOGO KIFEDHA AU KUTOJUA THAMANI YA ARDHI ILIYOPIMWA. HALMASHAURI LEO HII ZINAONEKANA KUSHINDWA KUFANYA KAZI HII NA KIMSINGI KAZI HII NI YA HALMASHAURI.
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]
[/TD]
[TD="class: buttonheading, align: right"]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"]Wednesday, 25 July 2012 21:03[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]

​

​
WALALA HOI WALALAMIKA, WALITOA SH30,000 ZA MAOMBI ‘ZIMEENDA NA MAJI'

Patricia Kimelemeta

MANISPAA ya Temeke imetoa orodha ya majina ya wananchi waliopewa viwanja katika manispaa hiyo, ambayo inaonyesha kuwamo kwa vigogo wanaojumuisha mawaziri, wabunge, watendaji wakuu wa Serikali pamoja na baadhi ya watoto wa vigogo hao.Katika orodha hiyo, jumla ya watu 1,800 walipatiwa viwanja hivyo, huku majina hayo ya vigogo yakiwa ni zaidi ya 50, ambao baadhi wamejiandikisha wenyewe, wengine wake zao, ndugu na watoto wao.

Majina hayo ambayo gazeti hili iliyaona jana, yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo wa manispaa hiyo, ili wananchi walioomba viwanja hivyo waweze kuangalia kama wamo katika orodha ya waliopatiwa viwanja hivyo.

Baadhi ya wananchi waliofika kusoma majina hayo walisikika wakilalamikia hali hiyo, huku wakisema kuwa kinachoonekana ni vigogo kupendelewa na kuwanyima wananchi wa kawaida.

Katika orodha hiyo, majina yanayosomeka ni pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama; Naibu Spika, Job Ndugai; Waziri wa Mawasiliano, Sanyansi na Teknolojia, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima.

Kwa upande wa Makatibu Wakuu wa Wizara wapo, Dk Florence Turuka (Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Ramadhan Kijjah; Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Omary Chambo na Dk Idris Rashid ambaye ni Gavana wa Zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Pia wamo Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk Didas Masaburi, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa; Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam, Suleinan Kova.

Wengine ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Haruna Masebu; Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh na Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH),Marina Njelekela.

Kwa upande wa wabunge wamo Dk Augustine Mrema (Vunjo - TLP), Mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe; Mbunge wa Kibaha Mjini (CCM), Sylvester Koka; Mbunge wa Kinondoni (CCM), Idd Azzan; Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), Dk Cyril Chami na Mbunge wa Singida Kusini (CCM), Mohamed Misanga.

Wengine ni Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila; Mbunge wa Igunga (CCM), Dk Peter Kafumu na Mbunge wa Bukene (CCM), Seleman Zedi.

Wabunge wa Viti Maalumu (Chadema), Maulida Komu na Suzan Lyimo, Viti Maalumu CCM, Dk Mary Mwanjelwa na Zakhia Meghji ambaye ni mbunge wa kuteuliwa.

Orodha hiyo pia inaonyesha majina ya ukoo yanayofanana na majina ya baadhi ya viongozi ambao ni Miraji Kikwete, Khalfan Kikwete, Juanita Mramba, Suzan Mkapa, Zainab Mkomwa, George Rupia, Maimuna Mfutakamba, Mary Membe, Pharles Ngeleja, Judith Kahama na Wilfred Mwanri.

Mkurugenzi apatwa kigugumizi
Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Magreth Nyalile alipoulizwa kuhusu orodha hiyo alisema kuwa, majina hayo hajayaona na kwamba waliobandika wamefanya uamuzi huo bila ya yeye kuupitia.

"Majina yenyewe sijayaona, hivyo basi siwezi kujua ni kina nani waliopewa viwanja hivyo, kwa sababu wako zaidi ya 1,000, jambo ambalo litakuwa vigumu kwangu kubaini tatizo hilo," alisema Nyalile.

Aliongeza kuwa, kutokana na hali hiyo hawezi kusema lolote kwa sababu yuko nje ya ofisi kwa ajili ya shughuli nyingine za ujenzi wa taifa.

Hata hivyo, Nyalile alisema mchakato wa ugawaji wa viwanja hivyo ulifuata taratibu za kisheria na kwamba hakuna mtu au kiongozi yeyote aliyependelewa, jambo ambalo linaweza kusababisha mgongano wa hapa na pale.

Nyalile alisema kuwa kama kuna viongozi walipewa kwa njia zisizo sahihi, au kwa rushwa wakati wa uwasilishaji wa majina hayo, walipaswa kutoa taarifa kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Wananchi walalama
Baadhi ya wananchi walikuwa wakiangalia majina hayo katika ubao huo walidai kuwa, baadhi ya maofisa wa halmashauri hiyo wamedaiwa kupewa rushwa wakati wa ugawaji wa viwanja hivyo.

"Walitangaza kama kiini macho, lakini tayari walikuwa na majina yao ili waweze kuwapatia na jambo ambalo limejionyesha wazi kwenye majina ya watu waliopewa viwanja hivyo," alisema mwananchi mmoja (jina tunalihifadhi) na kuongeza:

"Kutokana na hali hii, hatuna imani na viongozi wowote wa Serikali kwa sababu inaonyesha wazi kuwa, kila mmoja anaangalia masilahi yake na si wananchi wasio na kipato".

Aliongeza kuwa, wananchi hawana imani na viongozi wao, hivyo Serikali inapaswa kuingilia kati kwa sababu hali hiyo inaweza kusababisha matatizo.

Mwananchi mwingine aliyekuwa akifuatilia jina lake alisema: "Wewe unachokiona ni nini hapo kama siyo yaleyale ya ubinafsi! Wewe unaamini kabisa kwamba kweli hawa viongozi wetu hawana nyumba au hawana viwanja hapa Dar es Salaam.

Aliongeza: "Kama manispaa walitangaza viwanja ili wajiuzie wangesema tu badala ya kuchukua fedha zetu Sh30,000 halafu viwanja wakajigawia wenyewe."

Mgawo wa Viwanja
Mapema mwezi Juni mwaka huu, Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ilitangaza kwamba imepima viwanja 1,800 katika eneo la Gezaulole ikiwa ni mwendelezo wa utekelezaji wa Mradi wa Upimaji Viwanja.

Fomu za maombi ya kununua viwanja hivyo zilianza kutolewa Juni 11 na kila mwombaji alipaswa kulipia ada ya maombi ya kiasi cha Sh30,000 katika ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke iliyopo mkabala na Uwanja Taifa jijini Dar es Salaam.

"Fedha hizo hazitarejeshwa na mwombaji atajaza nakala mbili za fomu ya maombi na kuzirejesha zikiwa zimebandikwa picha 3 za ukubwa wa pasipoti. Mwisho wa kurudisha fomu hizo ni tarehe 18.06.2012 saa 8 mchana," linasomeka tangazo rasmi la manispaa hiyo.

Wakazi wenye nyumba na mashamba ndani ya eneo la mradi ambao walikuwa wametambuliwa kabla ya zoezi la upimaji kuanza, pia walitakiwa kununua fomu za maombi kwa utaratibu uleule.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Wamepewa viwanja watu 1,000 na kati yao wangapi (au % ngapi) ni vigogo au ndugu wa vigogo. Naona vilevile wamo waheshimiwa wabunge wa upinzani, je tuseme viongozi hawakustahili kupewa viwanja?
 
Jamani nilishawaambia, sasa ni kila mtu lwake. Anayedhani kuna atakayehangaika kumsaidia, basi aka asubiri hiyo serikali na hao waliojaa tamaa. Hata hawa wenzetu (upinzani) wanaojifanya wana uchungu na nchi hii na maisha ya watanzania ni walaghai na wanafiki wakubwa tena wachumia tumbo na wapenda sifa ambazo hawastahili. Njaa tu na tamaa zinawasumbua. Kila mtu apambane kivyake jamani, pata potea kupata kuna Mungu. Napita lkn nitarudi.
 
Haya Ni Makosa ya Uongozi; ni kwanini Viongozi wa Nchi yetu imewageuzia Mgongo wananchi?

Yaani ina Maana Vyama Vyote Sasa sio vya SIASA YA KUWAJALI WANANCHI? Hata kama Chadema wana wabunge 2

Ambao ni wa kuteuliwa Samaki Mmoja akioza wote wameoza...?

Hapo ndio inaonyesha ndio sababu ya kusainisha MIKATABA mibaya; kila mtu anajali chake tu cha kula...

Na Mrema kaupata U-DR.? Uhhh???
 
Nadhani waziri wa ardhi amelala usingizi mnono, naye kanogewa na utamu wa siasa. Siku hizi kimyaaaaaa! Utadhani hasikii wala haoni. Ukipata ulaji, weacha tu.
 
Naomba mwenye orodha ya watu waliopata viwanja Gezaulole tafadhari atuwekee.
 
1. Someone Kikwete
2. Someone Kikwete
3. Someone Kikwete
4.
5. Watakujakukujazia waliona majina mengine
 
Watu wanashindwa kuelewa kuwa, hata kama waliopata ni 39 Tu kati ya 1000, kwa nini kila viwanja vinapopimwa wanapata wao tu? Sisi wanyonmge tunaishia kujenga katika makazi yasiyopimwa? Tamaa ni kitu kibaya sana, mtu ana viwanja 20 kidogo, bado anapewa tu. Huu ni udharimu wa hali ya juu sana. Siku zenu zinakaribia!
 
Naomba mwenye orodha ya watu waliopata viwanja Gezaulole tafadhari atuwekee.
Katika orodha hiyo, majina yanayosomeka ni pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama; Naibu Spika, Job Ndugai; Waziri wa Mawasiliano, Sanyansi na Teknolojia, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima.

Kwa upande wa Makatibu Wakuu wa Wizara wapo, Dk Florence Turuka (Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Ramadhan Kijjah; Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Omary Chambo na Dk Idris Rashid ambaye ni Gavana wa Zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Pia wamo Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk Didas Masaburi, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa; Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam, Suleinan Kova.

Wengine ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Haruna Masebu; Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh na Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH),Marina Njelekela.

Kwa upande wa wabunge wamo Dk Augustine Mrema (Vunjo - TLP), Mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe; Mbunge wa Kibaha Mjini (CCM), Sylvester Koka; Mbunge wa Kinondoni (CCM), Idd Azzan; Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), Dk Cyril Chami na Mbunge wa Singida Kusini (CCM), Mohamed Misanga.

Wengine ni Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila; Mbunge wa Igunga (CCM), Dk Peter Kafumu na Mbunge wa Bukene (CCM), Seleman Zedi.

Wabunge wa Viti Maalumu (Chadema), Maulida Komu na Suzan Lyimo, Viti Maalumu CCM, Dk Mary Mwanjelwa na Zakhia Meghji ambaye ni mbunge wa kuteuliwa.

Orodha hiyo pia inaonyesha majina ya ukoo yanayofanana na majina ya baadhi ya viongozi ambao ni Miraji Kikwete, Khalfan Kikwete, Juanita Mramba, Suzan Mkapa, Zainab Mkomwa, George Rupia, Maimuna Mfutakamba, Mary Membe, Pharles Ngeleja, Judith Kahama na Wilfred Mwanri.
 
ndug freema agyeman: Huu ni uongo ulio wazi mkuu. Mita moja ya mrabaa kwa viwanja vya makazi ilikuwa ikiuzwa kwa shilingi 6000 na kiwanja kidogo kabisa walau kilikuwa na size ya mita 400 za mraba ambazo ni sawa na shilingi 2,400,000/= . Sasa wewe ni nani amekudanganya mabo haya. Kama huna uhakika au hujui ni vyeam ukawasikiliza wenye kuelewa masuala hayo la sivyo waweza ingia katika matatizo ya uchochezi. Cha msingi cha kusema ni kwamba pamoja na hayo bado bei ni kubwa

Na form nilichuku, KILICHONISHINDA ni bei baba. Low density 12 m na high density ni 3 m. Walichojitetea ni kwamba manispaa imekopa benki kuwezesha huo upimaji na ndio maana gharama ya ununuzi imekuwa kubwa kuwezesha kulipa mkopo.

Anyway kama nimekuwa mwongo, samahanini kwa kuwadanganya na inawezekana na mimi nimedanganywa?
 
nooo agyeman ni namna ulivoleta taarifa mwanzo ila sasa nimekuelewa kwamba bei ya 12m ilikuwa ni kwa low density plots. Pole mkuu i didnt mean to say u a liar
 
loooh!hakuna jina la masikini hapo,inauma jamani nyie
 
Katika orodha hiyo, majina yanayosomeka ni pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama; Naibu Spika, Job Ndugai; Waziri wa Mawasiliano, Sanyansi na Teknolojia, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima.

Kwa upande wa Makatibu Wakuu wa Wizara wapo, Dk Florence Turuka (Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Ramadhan Kijjah; Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Omary Chambo na Dk Idris Rashid ambaye ni Gavana wa Zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Pia wamo Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk Didas Masaburi, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa; Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam, Suleinan Kova.

Wengine ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Haruna Masebu; Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh na Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH),Marina Njelekela.

Kwa upande wa wabunge wamo Dk Augustine Mrema (Vunjo - TLP), Mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe; Mbunge wa Kibaha Mjini (CCM), Sylvester Koka; Mbunge wa Kinondoni (CCM), Idd Azzan; Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), Dk Cyril Chami na Mbunge wa Singida Kusini (CCM), Mohamed Misanga.

Wengine ni Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila; Mbunge wa Igunga (CCM), Dk Peter Kafumu na Mbunge wa Bukene (CCM), Seleman Zedi.

Wabunge wa Viti Maalumu (Chadema), Maulida Komu na Suzan Lyimo, Viti Maalumu CCM, Dk Mary Mwanjelwa na Zakhia Meghji ambaye ni mbunge wa kuteuliwa.

Orodha hiyo pia inaonyesha majina ya ukoo yanayofanana na majina ya baadhi ya viongozi ambao ni Miraji Kikwete, Khalfan Kikwete, Juanita Mramba, Suzan Mkapa, Zainab Mkomwa, George Rupia, Maimuna Mfutakamba, Mary Membe, Pharles Ngeleja, Judith Kahama na Wilfred Mwanri.

Mkuu,
Unaweza kutuwekea orodha yote? Ahsante
 
Hawa jamaa wa manispaa hovyo kabisa. Wanatuuzia form tena unapanga foleni kuanzia saa kumi usiku lakini kiwanja hupati. Huu ni wizi wa mchana kweuupe. Sipendi
 
Back
Top Bottom