Vigezo. . .

Dr Lizzy

Platinum Member
May 25, 2009
30,778
59,133
Tofauti na zamani siku hizi vigezo vya mwanamke kumkubali mwanaume ili awe mume na baba watoto wake vimeongezeka maana wadada wanajanjaruka siku hadi siku. Zamani muhimu ilikua 1. Anatoka kwenye familia nzuri. 2. Hawana matatizo ya akili/magonjwa ya kurithi 3. Ana kashamba kake kama sio kanyumba hata ka udongo na mengine yangejiset baadae.

Siku hizi bana vigezo vinatofautiana kuendana na aina fulani ya wanawake.

a) Miss dependent
1. Uwe 'mwanaume' hata kama ni kwa muonekano tu.
2. Uwe na pesa.
3. Uwe tayari ku-act kama mzazi wake maana anakuhitaji kwa kila kitu.

b) Miss independent (Miss Jeuri. .sio mjeuri). . .maana sio tegemezi kifedha, kihisia wala kifikra.
1. Uwe mwanaume kamili. . .hataki tabu.
2. Kichwani kuwe na kitu cha maana. . .
3. Muonekano wa kumridhisha (yaweza kuwa vyovyote) . . .
4. Uwe na heshima kwake. . .
5. Usiwe mgomvi
6. Uwe mwaminifu
7. Uwe tayari kukosolewa/kuwekwa sawa.
8. Uwe na maisha yanayoeleweka.
9. Uwe mwelewa.
10. Uwe safi kitandani.
11. Uwe msikilizaji mzuri.

c) Miss Erotica (Erotica haki zimehifadhiwa mwaya)
1. Be good in bed. . .
Mengine mbele kwa mbele.

d) Miss Desperate.
1. Mwambie "NTAKUO/NATAKA KUKUOA".
2. Kuwa na kanyumba ka kumweka hata kama ni cha kupanga.
3. Ongelea maswala ya kumpa mimba.

e) Miss Certificate
1. Kuwa na degree
2.Kuwa na PhD. . .
3. Itwa Dr. , Eng. , Prof. Fulani
4. Kuwa na vijisenti kidogo
5. Ongea kiingereza

f) Miss 'Born again'
1. Uwe mkristo.
2. Ujiite mlokole.
3. Upende maongezi yamhusuyo Mungu.
4.Upende kwenda kanisani na shida/mapungufu yako yote yataonekana ni 'mpango wa Mungu'.

JB WISER. . .there you go . . .
 
Last edited by a moderator:
Lizzy Pamoja na Category B kuwa na requirements nyingi, lakini that is my option& selection. katika hiyo Category B kipengere cha 7 na cha 11 kama vikikushinda then hata sifa nyingine hautokuwa nazo, kwani hivyo vipengere ndio Basic Human need.
 
Basi wapenda kuchinja wala sio kunyonga.
 
Last edited by a moderator:
Miss desperate for life!

Ila Lizzy ndo maana unamwagiwa tindikali, ukorofi huu.
Hahahaha. . .wifi hongera kwakujitambua mwaya. . .lolz
Ila ukorofi mi sina bana. . muulize hata kakako.

Ohhh na lile somo langu vipi?
 
Ndoaaa, ndoaaa!

Hii imedoda mama, ijazie jazie mwenyewe kwa kujibu kila post. Jibu na hii yangu tujibishane mara 10 zitafika angalau 35
 
Basi wapenda kuchinja wala sio kunyonga.
Hata wale jamaa wa Middle Eat Nyama wanayoikubali ni lazima iandikwe Halaal Food ndio mpango mzima yaani imechinjwa na siyo kunyongwa, Mwanaume kamili leo nimeamka na hasira kweli naona online Debt correct Wabongo Kiswahili mingi naingia mwenyewe Front. I will join u here in evening.
Good day.
 
Mpalestina at work.....Lol!! Kaazi kweli kweli.... itabidi na sie tuannalyse tunayoyategemea toka kwako....
 
Ndo maana sisi wengine kuoa inakuwa kazi ngoja nifuate ushauri wa bibi yangu nikabebe mzigo kijijini
 
Hahahaha. . .kweli mwanaume kamili hali haram.
Laters.
 
Mpalestina at work.....Lol!! Kaazi kweli kweli.... itabidi na sie tuannalyse tunayoyategemea toka kwako....

Mkirua nani ndie Mpalestina?
Kama unaniongelea mimi wakati bado hujajua nipo kwenye kundi gani ukijua je?
 
Last edited by a moderator:
Ndo maana sisi wengine kuoa inakuwa kazi ngoja nifuate ushauri wa bibi yangu nikabebe mzigo kijijini

Fidel80 labda umwache huko huko kijijini. Ukimleta mjini nae atabadilika awe kama aliowakuta. . .
 
Last edited by a moderator:
Fidel80 labda umwache huko huko kijijini. Ukimleta mjini nae atabadilika awe kama aliowakuta. . .

Hapo njia ni moja tu nikupiga mimba kila wkt hawezi badilika anakuwa busy na kulea kila baada ya mwaka mmoja na nusu napiga mimba ingine lengo kumfanya busy na kulea hata saloon atakuwa anasahau kwenda
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom