Vifo Vinavyotokana na Magonjwa ya Mafua vs Ugonjwa wa Corona Ulaya & Marekani

bizplan

JF-Expert Member
Jun 28, 2013
575
547
Najua kuna watu wanafatilia sana na kushtuka na idadi ya watu wanaokufa huko Italy kutokana na ugonjwa wa korona. Vifo hivi vimeleta hofu kubwa kiasi kwamba watu kusitisha shughuli zote ili kuzuia maaambukizi.

Kwa muktadha huo nimependa watu hasa wa dunia ya tatu kufahamu magonjwa ya mafua na yenye kuathiri mfumo wa upumuaji yamekuwa yakisababisha vifo vingi sana sana. Simaanishi kuhafifisha kinachotokea sasa hasa vifo vya korona natoa picha kuwa ipo hofu ya ziada iliyotokea.

Katika utafiti uliofanywa na Rosano et al (2019) huko Italy wenye kichwa kinachosema ‘Investigating the impact of influenza on excess mortality in all ages in Italy (2013/14 – 2016/17)’ inaonyesha kati ya mwaka 2013/14 hadi mwaka 2016/17 huko Italy idadi ya watu waliokufa kutokana na magonjwa yahusianayo na mafua ni zaidi ya watu 68,000.

Mchanganuo wake ni 13/14 – 7,027, 14/15 – 20,259, 15/16 – 15,801 , 16/17 – 24,981. Utafiti huu unasema watu wengi wanaokufa ni wazee na Italia vifo vitokanavyo na mafua ni vingi sana kulinganisha na nchi nyingine Ulaya. Kwa utafiti huu na ukichukua namba kubwa Zaidi ya vifo ya mwaka 16/17, ni wastani wa vifo 2081 kila mwezi kwa mwaka mzima, na au 4163 kwa mwezi ndani ya miezi sita ambapo ni karibu ya wastani wa muda wa mlipuko wa mgonjwa haya ya mafua kila mwaka.

Sasa linganisha idadi hiyo kwa Italy ambapo hadi tarehe ya leo ni watu karibia 11,591 wamepoteza Maisha tangu vifo vya mwanzo kutangazwa tarehe 22 Feb 2020.

Je, idadi hiyo itafikia au kuzidi idadi ya watu walio kufa kwa magonjwa yahusianayo na mafua mwaka 16/17 ambayo ni 24,981?

Kwa upande wa nchi ya marekani angalia katika website ya www.cdc.gov/flue ‘burden of Influenza’, inaonyesha idadi ya vifo vinavyotokea huko America kila mwaka vinavyotokana na jamii ya mafua ambapo kwa wastani kati ya watu 12,000 hadi 61,000 hufa kwa magojwa ya jamii ya mafua kila mwaka. Hii ni wastani wa vifo 10,166 kwa mwezi ndani ya miezi sita au 5083 kwa mwezi ndani yam waka mzima.

Mchanganuo wake hadi 2017 ni;

2010-11: 37,000 , 2011-12: 12,000, 2012-13: 43,000 , 2013-14: 38,000, 2014-15: 51,000, 2015-16: 23,000, 2016-17: 38,000.

Hapo idadi kubwa Zaidi ya vifo ni watu 51,000 wa mwaka 14/15. Linganisha na idadi ya sasa takribani watu 2854 wamefariki huko Marekani kwa ugonjwa wa korona.

Kwa duniani, WHO wanasema kuwa kila mwaka hadi watu 650,000 hufa kila mwaka kwa magonjwa ya kupumua yanayohusiana na mafua kila mwaka. Angalia www.who.int/news up to 650,000 die of respiratory diseases linked to seasonal flue each year.

Hadi sasa kwa dunia nzima inakadiriwa kuwa na vifo 35,035 vitokanavyo na korona tangu mwezi disemba mwaka jana. Linganisha idadi hiyo na vifo vitokanavyo na influenza vya dunia nzima, hii kulingana na mtandao wa www.worldometers.info.

Kutoka katika website ya John Hopkins medicine www.hopkinsmedicine.org inaeleza kwa urefu tofauti kati ya ugonjwa wa korona na ugonjwa wa mafua (influenza). Kwa kifupi magonjwa haya yanafanana sana kwa dalili zake kwamba yanasababisha homa, kikohozi, kutapika n ahata kuharisha. Namna yanavyosambazwa inafanana tofauti ni (INAWEZEKANA) korona ikasambaa kupitia hewa (airborne route) na mwisho hata namna za kuzuia zinafanana mfano kuosha mikono, kukaa nyumbani n.k. Muhimu kuliko yote tunaambiwa watu wanapona kwa magonjwa yote haya.

Mwisho, wakati habari za vifo vingi zikitangazwa kila siku zimeongeza hofu. Yawezekana ni kwa sababu ya mitandao ya kijamii na vile habari zinasambaa kwa haraka tofauti na zamani. Nani ajuaye?? Yawezekana watu wengi hasa wazee ambao kinga zao zimeshuka pia wakiwa na misongo mingi wanakufa kwa sababu ya taarifa mbaya wanazosikia kila wakati. Kama mwandishi Jeff Wise wa Psychology today anavyosema katika Makala yake ya Aprili 2010 kuwa ndio hofu inaweza kukuua ‘Yes, Fear Can Kill You’

Rai: Viongozi wetu, muda wa zile siku 30 zikiisha tufungue shule na shughuli zote wakati tukiendelea kuchukua tahadhari nyingine zilizopo sasa.

Tusisambaze hofu….
 
Rai: Viongozi wetu, muda wa zile siku 30 zikiisha tufungue shule na shughuli zote wakati tukiendelea kuchukua tahadhari nyingine zilizopo sasa.

Tusisambaze hofu….


Hapa nimeelewa vema

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani mkuu watu wafanye kazi sababu kinachoujia ulimwengu katika suala la anguko la uchumi wa dunia si dogo
 
bizplan,
hayo ni mafua tu hii ya sasa ni korona mkuu ogoba sana nchi zipo lockdown sasa imagine maisha yao yangekuwa yaendelea km kawaida hali ingekuwaje tuchukue tahadhari corona ni habari nyingine.
 
Kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO), asilimia 80 ya watu wenye virusi vya Covid 19 ambao unasababishwa na virusi vya Corona wanapona bila ya matibabu ya hospitali.
 
hayo ni mafua tu hii ya sasa ni korona mkuu ogoba sana nchi zipo lockdown sasa imagine maisha yao yangekuwa yaendelea km kawaida hali ingekuwaje tuchukue tahadhari corona ni habari nyingine.
Mkuu, lockdown huku kwetu haisaidii na ni ngumu kuitekeleza. Nimeonyesha hapo mfanano wa covid na influenza. Na hiyo influenza sio just kusema ni mafua tu, inakuwaga kali haswa. Haya yanatokea kila mwaka. Kweli korona ni hatari lakini si sahihi kufanya lockdown.
 
Wakiumwa ndugu zao ndio watajua joto ya korona, bafo wanamzaha
Mkuu hizo ni data. Influenza kwa kulinganisha na data za hadi sasa ni hatari kwa maana imeua au inaua watu wengi kuliko covid 19. Angalia hapo mwenyewe. Kama ni measures kali wangechukua basi miaka ya nyuma na kutangaza influenza pia ni janga.

Sina hakika kama vifo vya ugonjwa wa korona vinaweza fikia vifo vya influenza katika level ya dunia. Angalia data hapo nilizoweka.
 
Kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO), asilimia 80 ya watu wenye virusi vya Covid 19 ambao unasababishwa na virusi vya Corona wanapona bila ya matibabu ya hospitali.

Sasa ndio angalia maajabu hayo, ugonjwa ambao 80% wanapona bila matibabu kwa nini kuwaweka watu lockdown na kusimamisha maisha?
 
Mkuu umeandika kisomi sana, una PHD ngapi?

Unapaswa kuwa mshauri na mchambuzi mzuri.

Hizi ndizo post za kitafiti na kisomi zinavotakiwa.

Watu tufanye kazi. Saivi watu wameanza kumsikiliza WHO, DW, BBC, CNN, Reuters, RFI, kuliko wanavomsikiliza Mungu aliyewaumba.

Asante kwa compliments mkuu. Na tena hizo media ndio zimewajaza watu hofu sana. Pata picha mzee wa watu kachoka, umri umeenda na ana shida nyingi tu za kiafya, kumjaza hofu tu ni kumuua. Na hiyo hofu inaua hata kijana. Ukishakuwa na hofu kubwa kinga inashuka sana na unakufa kirahisi.
 
Mkuu, lockdown huku kwetu haisaidii na ni ngumu kuitekeleza. Nimeonyesha hapo mfanano wa covid na influenza. Na hiyo influenza sio just kusema ni mafua tu, inakuwaga kali haswa. Haya yanatokea kila mwaka. Kweli korona ni hatari lakini si sahihi kufanya lockdown.
tema mate chini kwa hali zao huko acha tu wakae lockdown mpaka hali itakapokuwa shwari.
 
hayo ni mafua tu hii ya sasa ni korona mkuu ogoba sana nchi zipo lockdown sasa imagine maisha yao yangekuwa yaendelea km kawaida hali ingekuwaje tuchukue tahadhari corona ni habari nyingine.
takwimu zinakataa kusema corona ni hatari vyombo vya habari vina kuza hofu kupita kiasi ambapo inalazimu watu kuamini kuwa corona ni zaidi ya ugojwa

Sent from my CPH1903 using JamiiForums mobile app
 
Wakiumwa ndugu zao ndio watajua joto ya korona, bafo wanamzaha
hapatanzania wamesha umwa watu zaidi ya 13 na leo wote ni wazima na wengine hata hawakutetereka kabisa tujaribu kulichukulia jambo kwa uzito wake tusiwe watu wakulishwa fikira na imani zilizo tofauti na uhalisia wito tujifunze kuwa wadadisi dunia inamambo

Sent from my CPH1903 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom