Vifo vilivyoniumiza JF

Pole sana Mkuu.

Hiyo namba 4. Acha tu! Siku nikipata muda nitaleta story hapa.

Lakini pia umemsahau Dena, sikumbuki ID yake vizuri but she was a good friend to many
 

Kila nafasi itaonja umauti kwa wakati wake muafaka, bila kuwahi wala kuchelewa. Ni vizuri kujiandaa kikamilifu kwa safari hiyo isiyokwepeka.

R.I.P kwa wote waliotangulia wanapostahili 🤭
 
R.I.P Mpauko,
huyu member amenifanya nijue mwanaume hadi jamii ijue kuwa ulikuwa unayapitia ni hadi pale hilo tatizo litakupeleka either kaburini.
Hakuna anaye jali mapito ya mwanaume ambaye hana uhakika wa kula kesho.
Huyu jamaa nilikuwa karibu nae sana na kifo chake kilinitikisa. Ni miaka mitano sasa nadhani imepita

Wengine sijui hata kama tukifariki kuna wa kuleta taarifa au na sisi tutaishia kama IDs ambazo zinapotea pasipo watu kujua shida ni nini.
 
Daah! Inauma sana, maisha yetu hapa duniani ni mafupi sana, leo upo kesho haupo, ni huzuni kubwa kwa kweli, sijui nitakufa kifo cha aina gani? Nawaza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…