Vifaa kama BVR vyanaswa vikiandikisha Dar

Vifaa kama BVR vyanaswa vikiandikisha Dar

Kuna habari kuwa BVR machines zimekamatwa maeneo ya Mwenge ITV karibu au ndani ya viwanda vya MM Steel vikiendelea na zoezi la kuandikisha wapiga kura.

Mwenye taarifa zaidi atujuze ilikuwaje.
Eti kuna habari...Vilaza utawajua tuu..
 
Hatari hii. Uongozi wa aina gani kipindi kama hiki unafanya zoezi hatari kama hiyo?

Kuna harufu mbaya hapo tena wa kiwango cha juu. Kuna thread iliwekwa jana kuhusiana na namna ya kutumia false information kudanganya mfumo wa NEC kwa kutumia data au taarifa kama hizo.
 
NEC mwaka msipokuwa makini mtaingiza nchi yetu kwenye vita hizi mashine za BVR zimetoka wapi?wahusika akina nani?wametumwa na nani?kwa lengo gani?mwaka huu kuibeba ccm haiwezekani tena
 
Hofu ilitanda jana katika kiwanda cha MM Steel cha jijini Dar es Salaam, baada ya kuwapo kwa taarifa kuwa mashine ya kusajili wapigakura kwa mfumo wa elektroniki (BVR) inatumika kuandikisha wafanyakazi katika kiwanda hicho.

Kutokana na hofu hiyo, baadhi ya maofisa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakiongozwa na Mwanasheria wa chama hicho, John Mallya, Polisi na Tume Taifa ya Uchaguzi (Nec), walifika kiwandani humo na kufanya upekuzi ikiwamo kuondoka na baadhi ya vifaa vilivyokuwa vinatumika.

Baada ya kukubaliana pande zote, vifaa hivyo ambavyo ni vya kuchukua alama za mikono, macho, scanner na kompyuta mpakato, vilichukuliwa na Polisi ili baadaye vikakabidhiwe Nec.
Polisi, Chadema na Tume, walielezwa na Meneja Mawasiliano wa kampuni hiyo, Abubakari Mlawa, kuwa kampuni hiyo imeamua kuandikisha wafanyakazi wake kutokana na kukithiri kwa vitendo vya wizi katika viwanda saba walivyonavyo na kushindwa kuwatambua wafanyakazi.

“Tunaendesha zoezi la kuweka ‘data base’ kwa ajili ya wafanyakazi wetu wote kwa maana ya kupiga picha na kuandika taarifa zake zote; amezaliwa wapi, amesoma wapi na ameanza kazi lini, wakati tunaendelea na zoezi letu walikuja watu wakajitambulisha kuwa ni polisi wakawaweka chini ya ulinzi watu wanaofanya zoezi hilo. Tulipowauliza ni kina nani, walisema wanatoka Chadema na wamepewa taarifa kuwa tunatoa vitambulisho vya kupigiakura,” alisema na kuongeza:
"Ili tujiridhishe, tuliamua kuwaita Nec na polisi kuthibitisha wamechukua mashine kwenda kujiridhisha. Tunafanya zoezi hili wiki nzima na tumeandikisha wafanyakazi zaidi ya 100 na tuna zaidi ya wafanyakazi 900.”

Hata hivyo, wakati anahojiwa na Polisi na Chadema kama kifaa cha alama za vidole wametoa wapi, Meneja huyo alisema walitoa zabuni kwa kampuni ambayo hakuitaja na alipotakiwa kuitaja hakufanya hivyo.
Afisa wa ICT wa Nec, Amosi Madaha, akizungumza mara baada ya kufika na kulinganisha mashine ya alama za vidole ya Nec na yao, alisema ni mapema sana kueleza kama vifaa hivyo ni sehemu ya vifaa vya BVR hadi watakapokwenda kuvichunguza zaidi.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango wa Nec, Salvisius Mkwera, alisema walipata taarifa kuna uandikishaji wa wapigakura unafanyika ndani ya kiwanda hicho na walipofika walikuta baadhi ya vifaa ambavyo ni ngumu kusema.
“Tulichokiona ni baadhi ya vifaa ambavyo vinafanana na vifaa vya Tume, lakini hatuwezi kuhakikisha kama ni vyetu au siyo, tulichokubaliana na polisi ni kuchukua vifaa hivyo vifanyiwe uchunguzi zaidi tujiridhishe na vifaa tulivyonavyo,” alisema.
Alitaja kifaa kinachofanana na cha Nec kuwa ni `finger print machine,' lakini wamechukua na vifaa vingine kama kompyuta mpakato na scanner.

Alisema pia wataingia kwenye data base ya kampuni hiyo ili kujiridhisha na taarifa zilizoingizwa.
Alisema pia wamechukua orodha ya wafanyakazi waliorodheshwa kwenye karatasi ili kuangalia kwenye daftari la kudumu la wapigakura kama kuna uwiano wowote.

“Tutatoa taarifa mapema na kwa wakati ili kuondoa wingu lililotanda kwa sasa, tunataka pande zote zijiridhishe hivyo tutafanya kwa uwazi kueleza kama hizi ni mashine zetu,” alisema.
Baadhi ya wafanyakazi ambao hawakutaka kutajwa majina yao, walisema wameshtushwa na uandikishaji huyo kwa kuwa unafanana na BVR hasa kwenye uchukuaji wa alama na kuamua kutoa taarifa.

SOURCE: NIPASHE
 
Kwa hali ya kawaida database ya wafanyakazi inajumlisha majina ,picha , namba na scan ya kitambulisho.Msitufanye wajinga eye scan na fingerprint scan zote za nini? Mandalizi ya kuchakachua tu hamna jengine. I mean,what's the point.You know,i mean,is it me or what? Don't take us fool's.
 
Kila kitu kwenu ni siasa. MM Steel walikua na Biometric Machine kwa ajili ya kuweka kumbukumbu za wafanyakazi wao na sio Biometric Voters Register kwa vile mna mihemko ya kisiasa na hamjiamini ndo maaa mkisikia Biometric mnajua tu ni lazima BVR.
Acheni kujitoa akili.
Kawadanganye wenzio
 
Yaani hata iwe vp, mwaka huu ccm huenda tukapata matokeo mabaya kutokana na kutokaa sawa ndani ya chama
 
INTERNATIONS OBSERVER MUST OBSERVE THIS!!
A bad sign of UNFAIR ELECTIONS!!

Hizo madhine ziko sehemu nyingi tu.Hutumiwa mambo ya ndani,mabenki mengi tu,makampuni kibao tu hata ya Tanzania ambayo hutumia dole gumba kufungua milango badala ya funguo unapoingia kazini au ofisi moja kwenda ingine n.k.Hata nyumbani kwako kampuni za ulinzi zaweza tengeneza kitu kama hicho milango ukawa unafungua kwa dole.Lengo la kufanya hivyo ni kuzuia mfanyakazi kuingia chumba ofisini asichohusika.Au ukitokea wizi waweza jua wote walioingia hapo siku hiyo.

Hizi machine ziko tofauti na za BVR na huuzwa madukani kama njugu tu
 
Magumashi tu hayo
zisije kuwa mashine za mafundo
mchundo wa SIDO au FTC..
 
Ccm hawataachia nchi kirahisi. Utasikia hao maafisa wa tume na polisi waliokamata wanakula kibano
 
Angalia screen vizuri, hizo nembo za nani????
Aisee.?????? NEC Huu mchezo mnaiangamiza Tanzania yetu nzuri.Jamani,Madaraka kweli yasababishe tuchinjane? Mzee Judge Lubuva huwa nakupigia kinanda pale St.Peter's kwenye misa zetu,I served you in the Holy Requiem Mass of Your Beloved Wife,Please,take this seriously. Ni heri ujiuzulu kama unaona huna kauli tena ndani ya management ya NEC. Heshima yako kwa watanzania na Mbele ya Mungu wetu itaishi milele.
This thing is genuine BVR!
Huu ni mchezo wa CCM na Idara ya nyeti (corrupt and rotten system)
 
Hizo madhine ziko sehemu nyingi tu.Hutumiwa mambo ya ndani,mabenki mengi tu,makampuni kibao tu hata ya Tanzania ambayo hutumia dole gumba kufungua milango badala ya funguo unapoingia kazini au ofisi moja kwenda ingine n.k.Hata nyumbani kwako kampuni za ulinzi zaweza tengeneza kitu kama hicho milango ukawa unafungua kwa dole.Lengo la kufanya hivyo ni kuzuia mfanyakazi kuingia chumba ofisini asichohusika.Au ukitokea wizi waweza jua wote walioingia hapo siku hiyo.

Hizi machine ziko tofauti na za BVR na huuzwa madukani kama njugu tu

Granted fingerprint scan is for access control what's the purpose of eye scan?
 
Back
Top Bottom