Video ya Mh. Tundu Lissu akiomba idhini ya Spika kuahirisha bunge kujadili Ajali ya meli

Brakelyn

JF-Expert Member
Oct 6, 2009
1,181
517
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania ameonyesha udhaifu mkubwa kwa kukataa hoja ya Mh. Tundu Lissu ya kuomba idhini ya Spika kutoa hoja kuahirisha shughuli za Bunge ili kujadili jambo la dharura kuhusiana na ajali ya meli iliyotokea...hii inaonyesha wazi kwamba hakuna umakini ndani ya serikali katika kushughulikia majanga kama hayo. Swala muhimu kama hilo linapaswa lijadiliwe kwa umakini ili kuokoa maisha ya waTanzania wasio na hatia.

majibu ya naibu spika kwa hoja ya mh. Lissu

Last edited by a moderator:
"Chanzo cha ajali kimefunguliwa kesi mahaamani hivyo si busara kuingilia majukumu ya muhili mwingine wa dola" Supika!
 
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania ameonyesha udhaifu mkubwa kwa kukataa hoja ya Mh. Tundu Lissu ya kuomba idhini ya Spika kutoa hoja kuahirisha shughuli za Bunge ili kujadili jambo la dharura kuhusiana na ajali ya meli iliyotokea...
Mkuu Brakelyn hii clip imekuwa fupi sana iongeze nasisi ambao hatukuangalia bunge tufaidi
 
Hivi kuna mtu anaweza kunieleza Mtundu Lisu alikuwa anaomba Bunge lijadili nini katika hili 'jambo la dharura?'. What exactly MP have to discuss on this issue? Serikali ina kazi gani? waache ujinga sasa, wameshakuwa wakubwa
 
Serikali inayoongozwa na imani za ki-freemason lazima iendelee kutoa kafara, kujadili ishu kama hiyo ni kwenda kinyume na makubaliano kati yao na freemason.wakinunua meli mpya hawatapata damu
 
Hivi kuna mtu anaweza kunieleza Mtundu Lisu alikuwa anaomba Bunge lijadili nini katika hili 'jambo la dharura?'. What exactly MP have to discuss on this issue? Serikali ina kazi gani? waache ujinga sasa, wameshakuwa wakubwa
hivi wewe polisi ni punguani kiasi hiki usione cha kujadili hapa? upolisi ni kweli ni kimbilio la waliofeli? washindwe kuona cha kujadili kuzama kwa meli mbili katika kipindi kisichozidi mwaka? hivi kweli polisi huoni bunge lina la kujadili nchi inaposhindwa kuokoa abilia mia mbili hamsini baharini tena karibu na ufukwe ianawapoteza nusu yake je ingekuwa na meli kama ile iliyozama italy yenye abiria elfu tatu(3000) tena imezama deep sea ilipoteza kumi na moja tu huoni wewe koplo cha bunge letu kujadili hapa? kweli yaani umefikiri vizuri na kutoa hiyo hoja dhaifu kiasi hiko aaha wapi mr policeman bunge lazima lijdili hili, mifumo ya usafirishaji majini mibovu cha kujadili kiipo
 
baada ya Lissu kumaliza kutoa hoja yake, naibu spika angetakiwa kuwahoji wabunge kama wanakubaliana na hoja hiyo ili iweze kujadiliwa na sio kumkaribisha wenje kutoa utaratibu..Naibu spika umechemka hapo!
 
Naomba walio na clip yenye kauli inayosema "Kuwa na nywele sio kuwa na uwezo wa kufikiri"
 
hivi wewe polisi ni punguani kiasi hiki usione cha kujadili hapa? Upolisi ni kweli ni kimbilio la waliofeli? Washindwe kuona cha kujadili kuzama kwa meli mbili katika kipindi kisichozidi mwaka? Hivi kweli polisi huoni bunge lina la kujadili nchi inaposhindwa kuokoa abilia mia mbili hamsini baharini tena karibu na ufukwe ianawapoteza nusu yake je ingekuwa na meli kama ile iliyozama italy yenye abiria elfu tatu(3000) tena imezama deep sea ilipoteza kumi na moja tu huoni wewe koplo cha bunge letu kujadili hapa? Kweli yaani umefikiri vizuri na kutoa hiyo hoja dhaifu kiasi hiko aaha wapi mr policeman bunge lazima lijdili hili, mifumo ya usafirishaji majini mibovu cha kujadili kiipo

mkuu siamini kama uwezo wa polisi wetu wa kufikiri mdogo kiasi hiki!
 
Hivi kuna mtu anaweza kunieleza Mtundu Lisu alikuwa anaomba Bunge lijadili nini katika hili 'jambo la dharura?'. What exactly MP have to discuss on this issue? Serikali ina kazi gani? waache ujinga sasa, wameshakuwa wakubwa

kama hujui ambacho kilikuwa kijadiliwe sasa unyamaze kimya!

Ni kuulize
1. Kwanini kila siku ajali za meli zinatokea na ni ukanda huohuo
2. Je unadhani kuna umakini katika ukaguzi wa meli hizi kabla ya kuaza safari?
3. Tume zinazo undwa zinatusaidia nini?
 
Hivi kuna mtu anaweza kunieleza Mtundu Lisu alikuwa anaomba Bunge lijadili nini katika hili 'jambo la dharura?'. What exactly MP have to discuss on this issue? Serikali ina kazi gani? waache ujinga sasa, wameshakuwa wakubwa

we kweli ndo sifuri kabisa.huoni ambacho bunge lingejadili?.. usiwe na akilikama za Kova polisi mwenzio
 
uccm unamsumbua ndugai

ndugai pumbaaafuuuuuuuuuu sana tena sana. Wewe ni n/spika aslahi na wa kuchonga anayetea ccm kwa gharama yoyote!
Kwa mara nyingine ccm wamedhihirisha kuwa hawana utu hata mamia ta watanzania wanapoteketea kwa ajali!!!!!!!!!!!!!!
 
hivi wewe polisi ni punguani kiasi hiki usione cha kujadili hapa? upolisi ni kweli ni kimbilio la waliofeli? washindwe kuona cha kujadili kuzama kwa meli mbili katika kipindi kisichozidi mwaka? hivi kweli polisi huoni bunge lina la kujadili nchi inaposhindwa kuokoa abilia mia mbili hamsini baharini tena karibu na ufukwe ianawapoteza nusu yake je ingekuwa na meli kama ile iliyozama italy yenye abiria elfu tatu(3000) tena imezama deep sea ilipoteza kumi na moja tu huoni wewe koplo cha bunge letu kujadili hapa? kweli yaani umefikiri vizuri na kutoa hiyo hoja dhaifu kiasi hiko aaha wapi mr policeman bunge lazima lijdili hili, mifumo ya usafirishaji majini mibovu cha kujadili kiipo

..umempa somo zuri...yamkini sasa ameelewa kilichotakiwa kujadiliwa!
 
ndugai pumbaaafuuuuuuuuuu sana tena sana. Wewe ni n/spika aslahi na wa kuchonga anayetea ccm kwa gharama yoyote!
Kwa mara nyingine ccm wamedhihirisha kuwa hawana utu hata mamia ta watanzania wanapoteketea kwa ajali!!!!!!!!!!!!!!

hao zenji wenyewe weny ndugu zao hawajal kila m2 na mambo yake wengnd ndo hao wanapigwa mabom ya machoz cc 2nang'ang'ana kuhairish bunge
 
Hivi kuna mtu anaweza kunieleza Mtundu Lisu alikuwa anaomba Bunge lijadili nini katika hili 'jambo la dharura?'. What exactly MP have to discuss on this issue? Serikali ina kazi gani? waache ujinga sasa, wameshakuwa wakubwa
Bunge sii ndio linatunga sheria? sii ndio wao wanapitisha bajeti ya matumizi..Sasa ulitaka wajadili nini zaidi kama huoni tofauti ya kujadili na kazi za serikali..
 
Back
Top Bottom