Video: Si kuibiwa ni kuzidiwa!

Video: Si kuibiwa ni kuzidiwa!

Status
Not open for further replies.

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
34,103
Reaction score
43,350

Haya ndiyo hapo sasa.

Wengine wametaka maneno:

Nipe kalamu nishike, hoja zangu niandike,
Nipe nami nisikikike, walimwengu wapilike,
Mnipe niliandike, na hili lifahamike,
Mke kukimbia nyumba, si wizi ni kuzidiwa!!!

Kapigwa mtu kikumbo, mke kaachia nyumba
Kalia bwana Mahimbo, kwa jaji kenda kuomba
Akatungia na wimbo, kamshinda hata Komba,
Mke kukimbia nyumba, si wizi ni kuzidiwa!!!

Kaja dada Josephina, kamuaga kwa kuzira
Mumewe akamnuna, na kusema kwa hasira,
Huyo mama akanena, pamekuwa na ukora,
Mke kukimbia nyumba, si wizi ni kuzidiwa!!!

Kibanda nakuachia, baba nanii naondoka,
Huku mama analia, na mizigo ameshika,
Kwangu nakukimbilia, kwako hapa nimechoka,
Mke kukimbia nyumba, si wizi ni kuzidiwa!!

Kaenda alikokwenda, maisha kuyaanzia,
Akataka pa kupenda, na moyo kutulizia,
Kampata wake nyonda, zilipendwa kaachia,
Mke kukimbia nyumba, si wizi ni kuzidiwa!!

Mtu kumwacha mwenziwe, huyo anayo sababu,
Kulazimisha isiwe, ni mwanzo kupata tabu,
Kamwe mgonjwa usiwe, nenda upate tabibu,
Mke kukimbia nyumba si wizi ni kuzidiwa!

Kaondoka ana kisa, si letu hilo ni lao,
Kumhukumu mkosa, ati kaacha mbachao,
Vikizidi vinatesa, mtu hurudia kwao,
Mke kukimbia nyumba, si ziwi ni kuzidiwa!!

Ukimtenda mwenzio, wengine wanangojea,
Mnyanyase na vilio, wapo wanaoombea,
Wawe ndio kimbilio, ndio wenza wagombea,
Mke kukimbia nyumba, si wizi ni kuzidiwa!

Ukiwa naye mwandani, mpende akakupende,
Simfanye kisirani, mtoto wa watu akonde,
Utenda mahakamani, ati jaji akulinde,
Mke kukimbia nyumba, si wizi ni kuzidiwa!

Utadai bilioni, ati mke umeporwa,
Kakuaga hadharani, hakusubiri kuparwa,
Watakucheka watani, umezidiwa hujaporwa,
Mke kukimbia nyumba, si wizi ni kuzidiwa.

Natama ninatuwama, wa kijiji nimesema,
Shujaa amesimama, kapendwa na huyo mama,
Haki yako kulalama, lakini kwanza tazama,
Mke kukimbia nyumba si wizi ni kuzidiwa!

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)

Sheria ya ndoa (1971) inasema hivi (msisitizo wangu):

73.-(1) A husband or wife may bring a suit for damages against
any person who has, for any reason, enticed or induced his or her
for spouse to desert him or her.
(2) A suit brought under this section shall be dismissed if the court
is satisfied that the conduct of the plaintiff has been such as to justify
or excuse his or her spouse leaving the matrimonial home
.
 
Last edited by a moderator:
MMjj utaua watu kwa ghadhabu. Unasema ...ukimtenda mwenzio, wengine wanangojea...sivyo?
 
Mwanakijiji nimekupata tena kwa herufi kubwa...jamaa anachekesha sana yaani duh kukimbiwa nyumba unatafuta mchawi! nasikia mwali kaondoka toka March, jamaa ndio leo anakumbuka kuwa alioa mke kanisani.
Waswahili wa pwani wanasema ukisha mwacha mke kwa zaidi ya miezi sita pasipo sababu au makubaliano, sii wako tena.
 
kwa tunaomjua jamaa... anatumika tu!!!

yes ni mwanakwaya mzuri sana wa ile kwaya iliyoendaga kongo ikaharibu, pombe ni kwa kwenda mbele sana... na anajua yalishaisha ila anatumika kwa kuahidiwa lots of cash

kimoyomoyo anajua kwamba yuko relieved
 
Yaani unatoka kupiga boksi yani halafu unapokumbana na kitu kama hiki...ha ha ha...yaani jioni imeisha ni kitu cha kucheka!Safi sana Mwanakijiji...kazi nzuri...
 
Ukipenda chongo.............................
 
Nikiondoa siasa zote na kurudi kwenye issue ya mke wa mtu kukaa na mtu mwingine, kabla ya talaka.

Hili halikubaliki, na ni kinyume cha maadili ya ndoa na ya Kiafrika. Unless mniambie huyu mwanamke alikuwa mke wa mtu akapata talaka, which does not seem to be the case here.

Yaani leo tunatetea infidelity kwa sababu aliyetenda ni Slaa ?

Slaa anazidi kujionyesha kwamba hana staha na taadhima za urais. Kama tunaangalia swala la ndoa, mimi ni bora nimchague mtu ambaye hajaoa (na hakai kunyumba na mke wa mtu) kuwa rais kuliko kumchagua mtu anayekaa na mke wa mtu kindoa, bila mke huyo wa mtu kupata talaka rasmi.
 
Ndoa ya Slaa ndiyo imeleta matatizo ya wa TZ kama kudorora kwa uchumi wetu,wachache kugawana mali asili zetu,ukosefu wa huduma za msingi za jamii,kukithiri kwa rushwa na mengineyo mengi yanayofanya"life expetency"ya MTZ izidi kushuka siku hadi siku?
 
Yaani leo tunatetea infidelity kwa sababu aliyetenda ni Slaa?

Kiranga sidhani kuna anayetetea infidelity hapa. Namshukuru sana MMJ maana hainiingii akilini mwenzio amekuaga, amekukimbia kwa zaidi ya miezi sita na hujafuatilia hata mara moja, leo unaibuka na madai umenyanganywa mke. Kwa desturi zetu za kiafrika, kama amekutoroka, unakwenda kwao kutoa taarifa, na aghalabu unarudishiwa mahari. Pili, naona hao waliochonga ngoma hii wameharakisha mno kama walivyokwisha sema wengine hapa, Mh ametoa taarifa tu kuwa yeye ni Mchumba wake; hawajaoona bado.

Shida ya Slaa ni kusema mno! Na hata huyo Josephine! Ingetosha kubaki pale kwamba wao ni wachumba, lakini kusema kwamba wameishi tena kinyumba sasa hii wapi na wapi, bwana. Si sahihi na siwezi nikaacha kulikemea hili. Lakini nisipoambiwa kama nilivyoambiwa nitabaki nasema lakini washenzi hawa wameshaonjana, lakini sitaenda mbali, maana kwa namna fulani ni kama jamii yetu ya sasa imeshakubali kama desturi kwamba huwezi ukawa na mchumba bila ya kumfanya hawara(concubine). Hii ni bahati mbaya sana.

Mimi nadhani twendelee na kile tulichotaka kufanya, uchaguzi, haya ni mambo yameletwa kututoa kwenye mstari na wamefanikiwa kweli!!!! na inauma
 
Huu ushabiki unatupeleka pabaya, let's be serious!!

Tatizo kubwa lililoifikisha nchi hii hapa ilipo ni kulindana na kuwaabudu viongozi ata pale ambapo makosa yao yapo dhahiri.

Nasikitika kuwa katika karne ya 21 bado watanzania wanaelekea kwenye njia hiyo ya ujima.
 
Ndoa ya Slaa ndiyo imeleta matatizo ya wa TZ kama kudorora kwa uchumi wetu,wachache kugawana mali asili zetu,ukosefu wa huduma za msingi za jamii,kukithiri kwa rushwa na mengineyo mengi yanayofanya"life expetency"ya MTZ izidi kushuka siku hadi siku?

Kwenye thread za matatizo ya uchumi wa TZ nimeandika kuhusu matatizo haya, nimeubalasa uongozi wa nchi inavyotakiwa, nimewasema CCM na Kikwete, na hata Nyerere, inavyotakiwa, kwa hiyo sioni haja ya kurudia hayo hapa, yatakuwa mambo yaendayo nje ya mada.

Mleta mada kaleta mada ya ndoa ya Slaa (au kuharibu ndoa kwa Slaa to be precise) na mimi najibu mada kwa kuongelea jambo hilo hilo.

Tukirudi kwenye mada, wewe unaonaje hili jambo la mwanamme mmoja kukaa kindoa na mwanamke mwingine ambaye bado ni mke wa mwanamme mwingine na hawajatalikiana rasmi. Unaona hili ni jambo la ustaarabu kweli? Muondoe Slaa, fanya kwa mwanamme yeyote yule.

Unaona hili ni jambo halali kweli ?
 
Tusiishie hapo tu kwenye kuishi na mtu ambaye bado ndoa yake haijavunjwa kisheria. Je ni sawa (kama tunavyosikia kuhusu Kikwete) kwa mtu aliye kwenye ndoa kutoka nje ya ndoa yake na kutembea kimapenzi na watu wengine?

Manake sasa huko tunakoelekea ni kubaya. Tutakosa hata anayetufaa kwani asiye na dhambi hizi na awe wa kwanza kumnyooshea mwenzake kidole....
 
Kwenye thread za matatizo ya uchumi wa TZ nimeandika kuhusu matatizo haya, nimeubalasa uongozi wa nchi inavyotakiwa, nimewasema CCM na Kikwete, na hata Nyerere, inavyotakiwa, kwa hiyo sioni haja ya kurudia hayo hapa, yatakuwa mambo yaendayo nje ya mada.

Mleta mada kaleta mada ya ndoa ya Slaa (au kuharibu ndoa kwa Slaa to be precise) na mimi najibu mada kwa kuongelea jambo hilo hilo.

Tukirudi kwenye mada, wewe unaonaje hili jambo la mwanamme mmoja kukaa kindoa na mwanamke mwingine ambaye bado ni mke wa mwanamme mwingine na hawajatalikiana rasmi. Unaona hili ni jambo la ustaarabu kweli? Muondoe Slaa, fanya kwa mwanamme yeyote yule.

Unaona hili ni jambo halali kweli ?

Hili sio jambo zuri sio tu kimaadili bali hata kisheria;kuishi na mke/mme wa mtu kabla hajapata talaka halali toka kwenye mahakama za kisheria ni kosa ndani ya katiba yetu!

Lkn nimeshtuka zaidi inaposemwa kuwa ukikaa na mke/mme wa mtu basi usipewe kura kwenye chaguzi na hivyo HAUFAI kuwa Rais wa TZ;hapo ndipo tunapopingana na wengine;Matatizo ya ndoa yanazungumzika ndani na nje ya mahakama(kama ambavyo mme huyu anataka fidia ya bilion 1 ili amuachie Slaa mwana mama huyu) lkn kufanya watz wote waufaidi uchumi wao inabidi achaguliwe kiongozi mwenye nia ya dhati ya kufanya hivyo!

Je sasa tuanze kujikita kwenye kuzungumzia suala la ndoa ya Slaa tukiacha kujadili jinsi ambavyo TZ ya mika 5 ya JK ilivyopteza dira?Je huu sio mpango wa CCM wa kuona watz tunapoteza muda wa kutowabana kwa nini hamna maisha bora hadi sasa kama walivyotuhaidi?
 
Kwenye thread za matatizo ya uchumi wa TZ nimeandika kuhusu matatizo haya, nimeubalasa uongozi wa nchi inavyotakiwa, nimewasema CCM na Kikwete, na hata Nyerere, inavyotakiwa, kwa hiyo sioni haja ya kurudia hayo hapa, yatakuwa mambo yaendayo nje ya mada.

Mleta mada kaleta mada ya ndoa ya Slaa (au kuharibu ndoa kwa Slaa to be precise) na mimi najibu mada kwa kuongelea jambo hilo hilo.

Tukirudi kwenye mada, wewe unaonaje hili jambo la mwanamme mmoja kukaa kindoa na mwanamke mwingine ambaye bado ni mke wa mwanamme mwingine na hawajatalikiana rasmi. Unaona hili ni jambo la ustaarabu kweli? Muondoe Slaa, fanya kwa mwanamme yeyote yule.

Unaona hili ni jambo halali kweli ?
Mkuu toka lini tumefuata maisha ya viongozi wetu kuwa msingi wa mila na desturi za mwafrika au Mtanzania ktk siasa?.. Je, unataka watu wazungumze kuhusu maisha ya JK na wale waliomtangulia au yale ya Mkapa hayatoshi kuonyesha kwamba kiongozi anaweza kuishi na mke wa mtu aloachika.

Na kama kweli tunataka kuchukua haramu kulingana na dini basi kwa fikra zako unafikiria JK msafi, na hata tukianzia Nyerere utakuta mengi yanayo karibiana na hili yapo. Tena basi tukianza kudai kujua watoto wa hawa viongozi wetu nje ya ndoa jambo ambalo ni kubwa zaidi sidhani kaa atabakia mtu hata huko bungeni.
Maadam hili sii jambo kubwa ktk mazingira yetu hata kama ndio sababu ya kudumaa kwa uchumi wetu basi la kufanya ni kuweka sheria. Na zaidi ya hapo hata kama Dr.Slaa amefanya makosa bado ni kesi ya madai (civil case) ambayo kwa mila na desturi zetu talaka haina maandishi ila unampomfukuza mke ndio imetoka kama hujasajili ndoa hiyo.

Huyu jamaa anaweza kabisa kuwa hakusajili ndoa yake ktk vyombo vya serikali laa sivyo angeweza kuitoa na kuonyesha usajili wa ndoa yake ili hata hizo mahakama zifanye kazi yake kisheria. ndoa zinazotolewa hati na makanisa au misikiti sio uthibitisho wqa kupelekwa mahakamani kwani inaweza kuandikwa siku yoyote na ikarudishwa tarehe nyuma. Ni usajili tu wa kisheria unaoweza kumfunga Bibie ikiwa pia hakuna separation ambayo pia inampa ruksa bibie kutafuta maisha mapya. Kabla ya talaka Dr. Slaa haruhusiwi kumwoa huyo bibie lakini kupiga anaweza kabisa kupiga na halali wakiwa separate na mumewe.

Kimsingi huyu jamaa kesi kama hii inamweka yeye kkatika hali ngumu zaidi ikiwa mama huyu atathibitisha alivyokuwa abused na mtajwa ikabidi aingie mitini. Na kwa desturi za kibongo kama jamaa alikuwa na kipapi kingine wakati bibie akiondoka haikumwingia akilini kabisa kwamba ndio kavunja ndoa yake. Na Dr.Slaa kama mwokozi akachukua wajibu wa mwanamme rijali..
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom