Video nyingine ya uwindaji haramu Tanzania

Video nyingine ya uwindaji haramu Tanzania

ImageUploadedByJamiiForums1408433145.729206.jpg
Wangepeleka kabisa tangazo hili CNN au BBC ili ulimwengu ujue kabisa kuwa utawala wa CCM ndivyo ulivyoamua kuliko kuiuza nchi kwa njia za siri.


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Tusipoangalia, baada ya muda si mrefu watawaruhusu hata kuwinda hata binadamu. Tusibiri?
 
Baada ya Mchg Msigwa kuanika huu ushenzi magazeti ya Rostam Azizz Mtanzania yalikuja na story ya ajabu ya kutetea ushenzi wa Green Miles kwamba wanaonewa na makampuni ya kimarekani.tena yakatumbukiza na udini ni bahati mbaya Rais wetu na vyombo vya ulinzi na yusalama vimelala pengine vinasubiri hali ikiwa mbaya ndio utasikia vinachukua hatua.
 
Mmefanya nchi yenu shamba la bibi kwa sababu ya ubinafsi na uroho wa kutajirika harakaharaka.
 
Unajua hili taifa bila wananchi kuamua hatutafaidika na rasilimali zetu,mda nmwingine tuna walaamu wawezekaji badala ya kulaumu sera na sheria zetu mbovu, unafikri kwa nn KATIBA MPYA, haitopakina, CCM anafanya au anacheza mchezo anao jua faida yake iko wapi, katiba mpya ndio ingetukomboa na kuleta sera na sheria ambazo zitalisadia taifa badala ya kuwanufaisha wachacahe wenye kisu kikali. so hatuna budi kuzitathimini sheria zetu, na pili wananchi tuchukue hatua hizi mbuga za wanyama ziko kwenye arddhi yetu, hivyo hatuna budi kuamua liwalo na liwe.
 
kama Mwangosi aliuwawa kwa kupigwa na bunduki na kusambaratisha matumbo yake na yeye ndie binadamu na alikuwa analalamika kwa lugha wanayoifahamu si rahisi kwao kumuonea huruma myama ambae hawajui lugha yake
 
Hivi karibuni Peter Msigwa aliweka hadharani video inayoonyesha wahusika wa Kampuni ya Uwindaji ya Green Miles Safaris Limited, wakitenda uhalifu wa wazi dhidi ya wanyama, wakikiuka sheria za Tanzania na kimataifa katika uwindaji.

Juzi Ijumaa tarehe 12 Agosti 2014, Motherboard wametoa video nyingine ikionyesha uharamia dhidi ya wayanma uliokuwa unafanywa na Green Miles Safaris Limited. Inadaiwa kuwa video ni sehemu ya video ndefu ya karibu masaa mawili inayoonyesha wakiwaua wanyama wakiwa kwenye gari, wakikimbiza na wanyama wachanga kwa gari, kuruhusu watoto wadogo kuwapiga risasi wanyama na kukamata mnyama mdogo na kuanza kumteza huku kichanga kikipiga kelele na kujaribu kukimbia bila mafanikio.

Utakachoona ni kama vile wawindaji hao wanawinda ndani ya uani wao bila wasiwasi wowote. Motherboard imejaribu kuwasiliana na Nyalandu na Msigwa lakini hawaku-respond, lakini mwakilishi wa Green Mile alisema kuwa serikali na Dallas Safari Club ndiyo wa kulaumiwa kwa unyanyasaji huu wa wanyama.

Green Mile Safari Co Ltd wanashangaa kwa nini unyanyasaji huo ulitokea mbele ya maafisa wa serikali. Wanadai kinachoitwa unyanyasaji wa wanyama kama kinavyoonekana kwenye video hapo chini ni mpango wa wapinzani wao kutoka Marekani kwamba hawashangai kwa kwa Nyalandu kuwasifu Dallas Safari Club baada ya kuwaadhibu Green Mile safari Ltd: Leaked Animal Abuse Video Shows Everything That's Wrong with Big Game Hunting | Motherboard


Hawa kweli si Waarabu wa Loliondo? Hebu sikilizeni lugha inayotumika.
 
Last edited by a moderator:
Baada ya Mchg Msigwa kuanika huu ushenzi magazeti ya Rostam Azizz Mtanzania yalikuja na story ya ajabu ya kutetea ushenzi wa Green Miles kwamba wanaonewa na makampuni ya kimarekani.tena yakatumbukiza na udini ni bahati mbaya Rais wetu na vyombo vya ulinzi na yusalama vimelala pengine vinasubiri hali ikiwa mbaya ndio utasikia vinachukua hatua.
Rais wenu hawezi kupingana na maslahi ya Rostum Aziz. Huo ni ukweli usiopingika.
 
Angekuwa ni mtanzania kafanya hivi angepata shida sana.
kweli njii hii kuna viongozi ni wajinga wa fikra na wazembe sana wa mawazo.
Asiye na uruma na maji kamwe hawezi kuonea huruma moto.:angry:
 
Siamini Kama waziri bado Ana endelea kuwapo madarakani kwa udhalilishaji mkubwa wa maliasili zetu.Nachelea kusema tuliwapa madaraka wamejisahau wanahisi nchi hii ni yao na jamaa.Kiukweli imeniuma sana.Tuanzishe kampeni ya kulinda maliasili zetu.Hii ilipaswa kuoneshwa na TV zote nchini watu wengi wajue jinsi maliasili zetu zinavyochezewa
 
Ni wakati wa kuishinikiza serikali itoe tamko la kuharamisha utalii wa uwindaji!
Utalii huo hauna tofauti na ujangili kwa sababu mantiki na muktadha ni ule ule!

Haya ni yanayorekodiwa na wenyewe wenye vitalu; yale maovu yaliyopitiliza yatakuwa ni makubwa zaidi! Eti kisa ni waarabu toka falme za uarabuni! Shame!
 
[8/19/2014, 8:06pm] ‪+255 684 094 617‬: Ajari mbaya imetokea Sikonge mkoan Tabora muda mfupi ulio pia Basi la AM na SABENA zagongana usokwa uso watu 50 wamefariki dunia na idadi yaweza kuongezeka
[8/19/2014, 8:07pm] ‪+255 684 094 617‬: Hadi sasa kichwa cha dereva wa Sabena hakijapatikana, na mbaya zaidi hakuwa Mwajiriwa bali ni day worker, chanzo cha ajali hiyo ni kutaka kuli Overtake bac la Sasebossa na kujikuta akigongana na AM uso kwa uso. Hadi sasa ni maiti zaid ya 50 zimeripotiwa kupatikana
 
Back
Top Bottom