Video nyingine ya uwindaji haramu Tanzania

Video nyingine ya uwindaji haramu Tanzania

EMT

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
14,477
Reaction score
15,356
Hivi karibuni Peter Msigwa aliweka hadharani video inayoonyesha wahusika wa Kampuni ya Uwindaji ya Green Miles Safaris Limited, wakitenda uhalifu wa wazi dhidi ya wanyama, wakikiuka sheria za Tanzania na kimataifa katika uwindaji.

Juzi Ijumaa tarehe 12 Agosti 2014, Motherboard wametoa video nyingine ikionyesha uharamia dhidi ya wayanma uliokuwa unafanywa na Green Miles Safaris Limited. Inadaiwa kuwa video ni sehemu ya video ndefu ya karibu masaa mawili inayoonyesha wakiwaua wanyama wakiwa kwenye gari, wakikimbiza na wanyama wachanga kwa gari, kuruhusu watoto wadogo kuwapiga risasi wanyama na kukamata mnyama mdogo na kuanza kumteza huku kichanga kikipiga kelele na kujaribu kukimbia bila mafanikio.

Utakachoona ni kama vile wawindaji hao wanawinda ndani ya uani wao bila wasiwasi wowote. Motherboard imejaribu kuwasiliana na Nyalandu na Msigwa lakini hawaku-respond, lakini mwakilishi wa Green Mile alisema kuwa serikali na Dallas Safari Club ndiyo wa kulaumiwa kwa unyanyasaji huu wa wanyama.

Green Mile Safari Co Ltd wanashangaa kwa nini unyanyasaji huo ulitokea mbele ya maafisa wa serikali. Wanadai kinachoitwa unyanyasaji wa wanyama kama kinavyoonekana kwenye video hapo chini ni mpango wa wapinzani wao kutoka Marekani kwamba hawashangai kwa kwa Nyalandu kuwasifu Dallas Safari Club baada ya kuwaadhibu Green Mile safari Ltd: Leaked Animal Abuse Video Shows Everything That's Wrong with Big Game Hunting | Motherboard

 
Last edited by a moderator:
... Aisee, Wanyama Wananyanyaswa Hivo?? Hii Inchi Imeoza Na Inanuka!
 
Hii serkali imeshindwa kabisa na ni dharau kubwasSana kwa watanzania
 
Hivi huwa wanatumia vigezo gani kuwapa hawa wapuuzi vibali hivi na wangekuwa kwao wangekuwa wanafanya hivi vitendo ila only in Tanzania wanatesa wanyama kila kinachokatiza wanawinda hadi watoto wa wanyama baada ya mda si wataisha
 
Hivi huwa wanatumia vigezo gani kuwapa hawa wapuuzi vibali hivi na wangekuwa kwao wangekuwa wanafanya hivi vitendo ila only in Tanzania wanatesa wanyama kila kinachokatiza wanawinda hadi watoto wa wanyama baada ya mda si wataisha

... Mkuu, Usiwalaumu Hao Wawindaji, Walaumu Viongozi Wako Wa Hichi Ki Inchi Kwa Kushndwa Kulinda Rasilimali Zetu.. Hata Watz Tumezubaa Sana
 
Na kuna waandishi wa habari tena wanajiita wahariri wanawapa watu kama hawa kurasa za kutosha kwenye magazeti yao. Huku wakitoa hukumu green miles wameonewa. Seriously????????? (? na wale wasio na uelewa on these issues wafanye nini.
 
Wanaojiita "Wawekezaji" always wapo juu ya sheria.

Na hilo litapita bila kufanyiwa kazi
 
Hivi huwa wanatumia vigezo gani kuwapa hawa wapuuzi vibali hivi na wangekuwa kwao wangekuwa wanafanya hivi vitendo ila only in Tanzania wanatesa wanyama kila kinachokatiza wanawinda hadi watoto wa wanyama baada ya mda si wataisha

Kuna requirements kila kampuni inatakiwa iwe nazo, nina uhakika 70% of hunting companies hazijafikia hivyo vigezo and the MNRT went ahead and issued them with hunting blocks bila kuwauliza watafanya nini kufikia vigezo vilivyowekwa.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
... Mkuu, Usiwalaumu Hao Wawindaji, Walaumu Viongozi Wako Wa Hichi Ki Inchi Kwa Kushndwa Kulinda Rasilimali Zetu.. Hata Watz Tumezubaa Sana

Na hawana uchungu wala uzalendo hawa viongozi sema ndo walipofika mana wanajua wananchi chochote kikitokea hawa react wamepoa hata viongozi tukiwalaumu wakati wananchi hawa react kwa chochote kila kitu ni sawa tu
 
Mkuu EMT,

Sometimes we as Tanzanians can ask ourselves a very simple question, that, has the president of the United Republic of Tanzania ever seen this kind of shit? hasn't he? We are yet waiting for the USAID to intervene and do something for us. ie kwa hisani ya watu wa Marekani. Au labda mpaka CITES au IUCN waingilie kati. Maanake Rais wetu hata kutamka tu kwamba kuna kitu kama hiki kimemkera sijasikia wala kusoma popote.

Maskini Tanznaia yangu nchi................mpaka lini????????????????????
 
Hivi hii wizara ya maliasili na utalii ina majini au mashetani? Hawa mawaziri na wafanyakazi wao wanakuwa wapi wakati haya yakitokea? Aaaah! Wanaleweshwa na vijisenti vya pembe hivyo wanakuwa bize kutangaza ufalme baa na nyumba ndogo siyo? Yafaa waondoke sasa waiache wizara ikiwa haina mfanyakazi yeyote ili hao watesaji wajinafasi. Hivi, wanasheria mnaungoja ushahidi gani zaidi ya hu uliotolewa na raia wema? Na hakuna mahakama za kimataifa za kuwashtaki hawa watesaji wa wanyama kama za kwetu hazina uwezo huo? Ccm acheni kulinda uovu sasa kwani yatosha.
 
Inasikitisha kwa kweli kwanza kwa kuwaona Watanzania kama hawana haki ya kupata kitoweo cha wanyama pori wakati zamani walikuwa wanaruhusiwa kwa masharti nafuu na bado rasilimali zetu zililindwa lakini pia kuwapa wageni mamlaka ya uwindaji bila uangalizi maalumu kiasi kwamba wanajichukulia wanyama wanavyotaka mpaka wanyama wadogo ambao ndio muhimu kwa ukuaji wa wanyama pori maana ukiwaua hao ndio mwisho wa kizazi hico. Kutokana na haya wananchi wanaoishi jirani na hizi hifadhi kama wamesusa vile kutoa ushirikiano kwa serikali kutokana na serikali kuwaona si chochote wala lolote. Nadhani ifike mahala sasa tuangalie contribution ya uwindaji wanyamapori kwenye uchumi wa nchi na kama haulipi ni bora kuangalia chanzo kingine cha mapato na wanyama wetu wakabaki tuwe tunawaangalia na kupewa ruhusa watz wenyewe kupata kitoweo mara moja moja au kama vipi wawe wanaainisha mahitaji yao ya wanyama alafu wanasindikizwa na mamlaka husika huku wakibakia na role ya kuchagua mnyama alafu wawakilishi wetu wanapiga mpaka kupata idadi inayotakiwa na kisha wanasepa
 
Back
Top Bottom