Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 11,583
- 15,381
Tabia ya kuweka picha za video katika mabasi wakati wa safari hukusudia kupunguza uchovu wa safari. Katika basi kuna watu wa dini, umri, rika na kabila tofauti.
Aidha inaweza kutokea kukawa na mtu anasafiri na wakwe zake ama viongozi wa kidini. Kumbe video zinazowekwa ni muhimu kuzingatia maadili.
Imekuwepo tabia isiyofaa kimaadili ambako zinawekwa video ambazo zina vipindi (scene) chafu, zinazoonyesha ufanyikaji mapenzi, ama zinazoonyesha watu wako uchi ama wenye uchezaji usio maadili kiasi cha kuleta simanzi kwa wasafiri.
wapo wasanii wanaonyeshwa kwenye video wamevaa nguo za kulalia na embe linaonekana wazi, na wa kiume "tango" linaonekana wazi, hii ni mbaya na inaaribu maadali ya watoto wetu.
Kila basi ukipanga unawekewa bongo movie, wanatukana kabisa wazi, mfano "pumbavu " wewe, 'kichwa kama tumbo la madenge", "mweusi kama bi"chau" na matusi mengine, ila kwa kwenzetu wazungu wakitukana Neno linakatishwa, sijui bongo hawa Basata wanalipwa mwisho wa Mwezi ili nini, LAKINI KUNA MTU AKASEMA Kuna wabunge wasamii kule bungeni, hawawezi kubali hayo mambo yaondolewe.,wao ndio wanafuria.
Nashauri Baraza la sanaa kushirikiana na watu wa mabasi TABOA kuchuja maudhui yanayoonyeshwa kwenye basi maana wakati mwingine inaleta fadhaa kwa wasafiri.