Wizara ya Elimu na hili za kuzuia nyimbo zisizo na maadili kwenye mabasi ya wanafunzi tu? Linashangaza!

haha

JF-Expert Member
Apr 21, 2013
1,400
1,628
Kuna wakati maamuzi mengine yanashangaza kidogo au Sana!! Sijajua basata Huwa inawaogopa Bongo favour au vipi!?

Juzi Wizara ya Elimu imekuja na azimio la kukataza nyimbo zisizo na maadili kupigwa kwenye mabasi ya shule!! Amaa!!!, kumbe mnajua kuna nyimbo zisizo na maadali? Kwanini, msizifungie zisisikike popote?

Je, Mwanafunzi atanyimwa tu kuzisikiliza kwenye school basi lakini siku akipanda daladala azisikie?, Je, Vipi sisi watoto wetu wasiopanda school basi wao ruksa kusikia?

Kwanini msiweke Sheria Kali msanii alazimike kupeleka nyimbo Basata kabla ya kuiachia kwenye media ili kama Ina kasoro zirekebishwe!!! Kwa kweli Basata hapa mmefeli.

Kwanini Kuna kubembelezana kuliko pitiliza kati ya Serikali/Basata na wasanii wanaoimba upuuzi?
 
Kuna wakati maamuzi mengine yanashangaza kidogo au Sana!! Sijajua basata Huwa inawaogopa Bongo favour au vipi!...
Nafikiri hujasikia TANGAZO vizuri

Wizara imezuia nyimbo zote kupigwa kwenye mabasi ya wanafunzi na hata TV.
Kimsingi, unamtoa mwanafunzi Nyumbani anawazia somo la Hesabu, halafu unamuwekea Manyimbo ya kumchanganya akili kwenye gari? Yalikuwa mambo ya ajabu kabisa hayo

Binafsi nikitoka kwenye shughuli zangu za kuchosha kichwa, hata sitaki kelele za manyimbo sembuse mwanafunzi anayekwenda darasani pengine kufanya test.

Nauona ni uamuzi mzuri sana tena umekuja kwa kuchelewa!
 
Watanzania sijui shida ni nini, ama ni ujuaji au stress za maisha. Mtu anaweza pinga kitu kabla hata hajakitafakari na kutazama uzito wake katika maisha yake au jamii inayomzunguka.

Sasa jiulize, mtu anapinga kitu kama hiki kwa faida ya nani, yaani wanafunzi waliwekewa mziki kwenye basi la shule wanafaidika na nini kiakili ?
 
Back
Top Bottom