Video:John Heche amlipua Waziri Mpango Bungeni

Video:John Heche amlipua Waziri Mpango Bungeni

Hataree sana! Dr Mpango atapata tabu sana kuendelea kufanya kazi na Magu maana inabidi awe muongo na bahati mbaya takwimu za uchumi huwa zipo wazi na haziongopi ni vyema akajiuzulu kuliko kupoteza heshima yake kutetea upuuzi
Mr mpango hana mpango na kila mipango yake haitekelezeki kwa 100% ni Waziri wa fedha mzigo
 
Hawa maprofesa jamani wanapata shida(wanadhalilika) kwenye masuala haya ya siasa ukizingatia inabidi wajibu hoja bila kumpa changamoto mkulu.
Ushauri wangu: Ni bora wangerudi vyuoni kufundisha sababu bado wana mchango mkubwa. Ilinisikitisha sana Dr.Mpango alipopewa changamoto ile ya makontena na yule mkuu wa mkoa,yaani alikuwa na hasira kisa yule ndugu.
Utawala huu mkuu wa wilaya, mkoa wana nguvu kuliko mawaziri hujiamulia chochote pasipo kumuuluza wala kupata ruhusa toka kwa Waziri wa Tamisemi, kuna vioja vingi Naibu Rais wa jamuhuri ya Tanzania na Rais wa Dsm ndugu Bashite yeye ana nguvu kuliko Waziri mkuu, makamu wa Rais na mpaka Rais wa Zanzibar.
 
Unamaanisha aliyweka post au waliorekodi video? Wahusika wakuu katika hili ni Bunge TV

Huyo mtayarishaji aliyeitengeneza kwaajili ya mtazamaji na msikilizaji, alitakiwa kutambua aina ya audience waliopo
Wapo wanaoona na kusikia
Wapo wanaoona na kutosikia - wangepata ujumbe kwa text
Wapo wasioona lakini wanasikia
 
haya mawe yatamuua mpango, pesa haionekani jamaa anauliza ama wanazilalia
 
haya mawe yatamuua mpango, pesa haionekani jamaa anauliza ama wanazilalia
Wanachukua pesa Hazina kienyeji pasipo idhini ya Bunge, Gavana wa BOT na katibu mkuu wa wizara ya fedha huwapa pesa mda wowote wakitaka hata Usiku wa saa nane, pesa zote zinatumika kuwanunua madiwani, wenyeviti, wabunge kurudia chaguzi kwa gharama kubwa ni pesa hizo hizo wanachukua ndiyo maana Bajeti huwa hazitekelezeki kutokana CCM kuingiza Nchi kwenye matumizi mabaya ya pesa za umma.
 
Utawala wa Majimbo ni muhimu sana Ulaya America, South Africa na hapo kenya wanautumia ni Utawala ambao ni mzuri ktk kuthibiti pato la taifa, huu Utawala wa kutumia wakuu wa mikoa umepitwa na wakati sana, Nchi nyingi hawatumii wakuu wa mikoa bali Mamea hata china Nchi ya kikoministi haina cheo cha mkuu wa mkoa bali ni magavana na mamea kwenye miji mikubwa.
 
Mbona umetupa mifupa mitupu... weka tu nyama nyama basi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom