Parabolic
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 2,886
- 3,174
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi, amemjibu Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, kufuatia kauli zake za kutilia shaka mafanikio ya nchi.
Soma: Sugu amvaa Kihongosi, amtaka aachane na Heche
Akizungumza Septemba 26, 2026 katika mkutano wa hadhara uliofanyika Tanga Mjini mkoani Tanga, Kihongosi amebainisha kuwa alimsikia Heche akiwa Bariadi mkoani Simiyu akidai kuwa haoni kilichofanyika nchini tangu kupatikana kwa Uhuru.
Akijibu kauli hizo mbele ya wananchi wa Tanga, Kihongosi amesisitiza kuwa CCM iko tayari kumpa Heche data na takwimu sahihi ili kuondoa kile alichokiita upotoshaji kuhusu uelekeo wa nchi.Kihongosi pia alijibu madai ya Heche kwamba anatajwa mara kwa mara na viongozi wa CCM au kwamba Kihongosi ni kijana mdogo asiye na hoja, akimfahamisha kuwa mwanasiasa wa kweli hupimwa kwa hoja za msingi na siyo kwa ‘makelele’ au umri.
Chanzo: Jambo TV.
