Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,815
- 4,558
Daktari Elisha Osati akiwa kipindi cha Mtazamo cha Clouds Plus ameeleza hali ya Virusi vya Corona ilivyo nchini pamoja na uchukuaji wa tahadhari.
Akijibu swali la Mtangazaji wa kipindi hicho lililomtaka kutoa tathmini ya hali ya Corona nchini Daktari Elisha alisema:
"Hili swali uliloniuliza lipo very tricky kulingana na wakati huu tulionao lakini ukweli ni kwamba tumekuwa tukiwahudumia Wagonjwa hawa wenye matatizo ya moyo, figo, damu kila mwaka. Tunachokiona kwa sasa ni tofauti ndio maana hatuwezi kukaa tukasubiri tutalaumiwa siku moja kwamba hatukufanya sehemu yetu."
Anaendelea, "Unajua debate imekuwa hapa nchini kwetu ugonjwa upo ama haupo na wakati tunaendelea kubishana hatuwaambii watu wachukue hatua muda huo watu wanaendelea kuambukizana until juzi nimeona kwenye Mwendokasi wametoa tamko. Tunamshukuru Mh. Rais juzi kanisani alisema ugonjwa upo ili watu wachukue tahadhari"
Kwahiyo, bado hatujachelewa, we need to focus kwenye kuwatibu hawa waliopo na kuwakinga wengine especially kwenye mambo ya chanjo lakini watu waendelee kuchukua tahadhari. Barako ni very important hususani unapoenda kwenye watu wengi kunawa kila wakati na kutumia sanitizers.