Salaam wakuu,
Nina project moja ya ku-shoot video nataka kufanya kule Ngorongoro crater. Nataka kuchukua video hizo kutokea juu kwenye ukuta wa crater (crater rim) ambao uko kwenye mwinuko wa kiasi cha mita 600 kutoka kwenye sakafu ya kreta (crater floor) yaani kule chini waliko wanyama. Crater ya Ngorongoro ina kipenyo cha takribani kilometa 20. Ni video camera gani yenye optical zoom (siyo digital zoom) ya kutosha itakayoniwezesha kuona wanyama na kupiga picha katika eneo lote la crater kutokea juu kwenye ukuta wa crater?
Naomba wataalamu mnipe ushauri.