mechard Rwizile
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 1,571
- 875
Leo umeifanya thamani ya jamii kuwa kubwa sana kwangu. Nimejifunza na lililonifurahisha zaidi wewe ni mtu mwenye busara maana huna jazba kama baadhi ya wanamtandao wanavyofanya. Umeimarisha ufahamu wangu. Tangu mwanzo sijaongelea maudhui ya mada zako ile ya Dr. Shein na ufalme wa arabuni na hata hii ya Dr. Salim Ahmed salimu, mtu mjuzi na mstaarabu wa viwango vya juu kabisa katika historia ya nchi yetu. Tumeongelea zaidi lugha/ methali. Huu ni mjadala mkubwa japo hauwavutii watu wengi.Hahaha sawa mkuu,inawezekana uko sawa,...lakini nionavyo mimi huu msemo unamaanisaha vingine kabisa,baniani ni wahindi wenye dini ya "Hindu",kwa wakati huo hawa walikuwa wahindi maskini,kwani walikuwa wakibaguliwa na wahindi wenzao ambao wengi walikuwa waislam...,kazi yao ilikuwa uchuuzi (machinga)na kuuza vitu vidogo vidogo
"Baniani mbaya kiatu chake dawa" inamaanisha mtu hata kama yuko mbaya lakini ana mazuri yake...
nimeona nikuwekee post moja ya mwaka 2013 yenye methali hii ya baniani mbaya kiatu chake dawa.,uzidishe maarifa mkuu,bofya chini hapo😉
Baniani mbaya kiatu chake dawa!!!!!!
Ki ukweli watu wengi wamekuwa wakiikosea methali hii kwa miaka mingi sasa. Watalaam wa lugha hii wanafanya makosa kuhusiana na kuruhusu makosa kuendelea kufanyika. Na kadri inavyozoeleka wengine wanadhani basi ni sahihi. Mimi na wewe tumekubaliana karibu kila eneo isipokuwa dau kwa upande wangu na dawa kwa upande wako. Kwa maana hii nitakubaliana na neno "dawa" kama methali mpya, yaani ya kizazi chenu lakini ile ya wahenga itabaki kuwa "baniani mbaya kiatu chake dau". Kama umefatilia unaona uhusiano uliopo kati ya baniani, Ubaya wake, kiatu chake, dau lake. Wewe unasema baniani mbaya kiatu chake dawa kwa ugonjwa upi?