waseme nini wakati wao ndo wateja wakuu, kama hawaongelei jambo hili zito hivi kwanini tusiwanyooshee vidole???Hotuba ya wapinzani leo imempongeza Ntetema, hotuba ya waziri wa serikali haijasemea jambo hili.
The was this new report on ITV yesterday. It was very shocking. Imagine mganga amekamatwa na miguu ya albino. Ilikuwa ni habari ya kusikitisha especially after seeing those live pictures. Miguu miwili imekatwa na kuwekwa kwenye mfuko. Worse enough ni kwamba mganga husika alifanikiwa kutoroka. Washirika wake akiwemo mke wake mdogo wanashikiliwa na polisi. Sijui Tanzania tunakwenda wapi. Mimi naona wanaopatikana na hatia wote ya kuua au kukata viungo vya albino wanyongwe hadharani with live TV coverage.
Tanaznia ipo vitani siku nyingi sema mpaka vita vikikaribia ikulu ndio watawala wanashituka, hata wale wa Sadam Hussein walikuwa wakiimba bado wako salama wakati adui alikuwa sebuleni.
Asiyeamini kwamba vita vimeanza siku nyingi angojee kitanda alicholalia kikichomwa.
Kila mtanzania anamaumivu yake.
Albino wanatolewa sadaka,
Wanafunzi wanafukuzwa shule.
Waalimu hawalipwi.
Wagonjwa mahospitali wanakufa KWA KUKOSA HUDUMA.
mafisadi wanatia kichefuchefu kila mtu.
Viongozi wako likizo huku wakituzomea na shida zetu.
Kazi hakuna.
wasomi wanadharauliwa.
Wafanya biashara wazawa wanaoonekana nuksi.
Machinga kilio cha samaki.
Kila kona inahuzunika.
kikwete kakumbatia washikaji na waliompeleka ikulu na fedha zao.
wananchi tumekua wasindikizaji na macho ya huruma.
Vita gani tena tunasubiri, tupo vitani, kazi iliyobakia ni kupindua kitanda kila mtu alale chini.
Maneno mazito sana .
Hivi Vicky Ntetema matisho anayapata akiwa kule kule BBC UK ama yuko BBC Dar ?
Vicky Ntetema aliyapata matisho akiwa BBC Dar TZ. Baada ya vitisho wameamua kumrudisha London na jana tu ndo nimemsikia akisoma habari aikiwa BBC London.
Mbona hasemi nani anayemtishia? Na kwa sababu gani?