Vick Kamata: Utajiri hu unahitaji maelezo ya ziada

Vick Kamata: Utajiri hu unahitaji maelezo ya ziada

Baba ya watoto hajatajwa he he kuna picha ilitupiwa hapa mtoto wake wa kiume anafanana na rizmoko!
 
- Kaka wacha majungu na siasa za makengeza sio nyie mliotuambia hapa kwamba utajiri wa Sugu ni halali maana alikuwa muimbaji wa muziki sasa hapa tofauti ni nini hasa ya hawa wanamuziki wawili kuwa na utajiri unaofanana? Sometimes mnakuwa na siasa za kuchekesha tulipouliza hapa kuhusu utajiri wa Sugu mlisema ni mwanamuziki sasa what is the problem hapa?

Le Mutuz
Le Mutuz,sometimes silence speaks louder than words,sio kila kitu uchangie.Hivi by the way 2015 unategemea kugombea jimbo gani? maana naona sera mpya ni Sioi-ism,naona mwenzio mtoto wa marehemu waziri wa fedha yuko ulingoni.
 
Vicky kamata kama umo humu jf kamata maoni yangu,

kama unaweza kukamata fursa zaidi ya hizo kamata,akikamata mdosi kelele,akikamata mangi mwizi,akikamata naniliu kapendelewa. Cha msingi usiibe,mungu hapendi.

Kusanya hiyo mihela na ukajenge kwenu geita.
 
We kukata viuno mbele ya Mzee wa kaya halafu atoke kapa hâta siku moja.dada aliona fur sa kiuno mtaji sa sa à semé na watoto ni wa nani ndo mshangae.tangu lini baba wa watoto akafichwa hii ndo tz banal na BD mtaona mengi
 
- Kaka wacha majungu na siasa za makengeza sio nyie mliotuambia hapa kwamba utajiri wa Sugu ni halali maana alikuwa muimbaji wa muziki sasa hapa tofauti ni nini hasa ya hawa wanamuziki wawili kuwa na utajiri unaofanana? Sometimes mnakuwa na siasa za kuchekesha tulipouliza hapa kuhusu utajiri wa Sugu mlisema ni mwanamuziki sasa what is the problem hapa?

Le Mutuz

Acha kujipendekeza mtoto wa kiume.
 
Kama alishawahi fanya kazi BOT, inawezekana ni mafao ya BOT.:A S 13:
 
Hawa akina mama hua na speed ya kutisha ya kula hasa wakitokea kwenye umaskini mkubwa. Kuna njia nyingi za kupata utajiri haraka kwa kiongozi katika nchi isiyokua na uadilifu wa viongozi kama tanzania. Kwa hiyo kama kuna mashaka na utajiri wa vicky sio jambo la ajabu.
 
- Kaka wacha majungu na siasa za makengeza sio nyie mliotuambia hapa kwamba utajiri wa Sugu ni halali maana alikuwa muimbaji wa muziki sasa hapa tofauti ni nini hasa ya hawa wanamuziki wawili kuwa na utajiri unaofanana? Sometimes mnakuwa na siasa za kuchekesha tulipouliza hapa kuhusu utajiri wa Sugu mlisema ni mwanamuziki sasa what is the problem hapa?

Le Mutuz

Sugu amefanya kazi miaka mingapi ukilinganisha na Vicky..
 
ninavyojua mimi,vicky kamata kama mtoto wa kike ana "kitega-uchumi" chake na amekitumia barabara ktk kuchangamkia fursa hasa zile za kuwa karibu na wakubwa wa awamu hii ya jk.she deserves it all.
 
WANAWAKE na maendeleo, tufanye kazi, tusonge mbele, yelele…yelele… Hii sehemu ya mashairi ya wimbo wa staa wa muziki wa kizazi kipya na Mbunge wa Viti Maalum (UVCCM), Geita, Vicky Kamata anayetajwa kuwa na utajiri balaa. Vicky amepata mafanikio makubwa ambayo kila mwanamke Tanzania angependa kuyapata.

KABLA YA SIASA, KABLA YA BONGO FLEVA Kabla ya siasa aliishi maisha ya dhiki ambayo hakutegemea kama angekuja kupata mafanikio makubwa. Ni miongoni mwa Watanzania waliozaliwa katika familia duni. Katika kutafuta ‘kutoka’ kimaisha, Vicky amewahi kuwa mwanamuziki wa Bongo Fleva na kutunga nyimbo mbalimbali, wimbo wa Wanawake na Maendeleo ndiyo uliomtambulisha zaidi katika jamii. “Nimezaliwa kwenye familia duni, nimeishi maisha ya dhiki sana, mbali na muziki, nimewahi kuwa mwalimu wa shule ya msingi kule Moshi (Kilimanjaro) katika harakati za kusaka maisha, baadaye nilikwenda Morogoro. “Kila kitu kinabadilika kama ukimwamini Mungu,” alisema Vicky mwenye watoto wawili, Revocatus na Glory (jina la baba halikutajwa).

MAFANIKIO YAANZA Mwaka 2006, Vicky alifanikiwa kuajiriwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) akiwa ni afisa uhusiano. Mwaka 2010, Vicky alifanikiwa kuwa mbunge wa viti maalum akiuwakilisha Mkoa wa Geita.

MJENGO WA GHOROFA MBILI Akiwa mbunge, Mheshimiwa Vicky ameingia kwenye orodha ya wanawake mabilionea nchini kwa kuangusha mjengo wa kifahari wa ghorofa mbili Sinza jijini Dar es Salaam wenye thamani ya shilingi bilioni moja na milioni mia nne. Ndani ya ghorofa hilo kuna bwawa la kisasa la kuogelea ‘swimming pool’ ambalo linatumiwa na familia yake.

MAGARI YAKE SASA Kama walivyo matajiri wengine, mheshimiwa huyo anamiliki magari manne ya kifahari, yote yakiwa na thamani ya shilingi milioni 261. Ana Toyota Voxy- Noah ambalo alilitoa sokoni kwa shilingi milioni 16. Kamata pia anamiliki BMW X5 likiwa na thamani ya shilingi milioni 130. Mara nyingi anapokwenda bungeni, Vicky hutembelea gari linalomudu mikiki ya barabarani, Toyota Land Cruiser ‘VX’ ambalo lina thamani ya shilingi milioni 90. Pia mwanamama huyo ana gari aina ya Toyota Altezza alilolinunua kwa shilingi milioni 25.

ANAMILIKI MGODI WA DHAHABU Wakati hayo yakiwa wazi, chanzo makini kilidai kuwa, mheshimiwa huyo amenunua mgodi wa dhahabu Geita, jambo ambalo ni sehemu kubwa ya mafanikio yake. “Vicky amenunua mgodi wa dhahabu Geita, mimi ni mtu wangu wa karibu, hapendi kusema mafanikio yake wala watu wajue lakini ukweli ndiyo huo. Eneo ni kubwa, muda si mrefu uchimbaji utaanza,” kilisema chanzo cha habari.

ANA SHAMBA LA EKARI 157 Utajiri wa mheshimiwa huyo unaendelea kuanikwa kuwa, ni pamoja na shamba lenye ekari 150, Kisarawe, Mkoa wa Pwani. Pia ana shamba la miti Kibamba, Dar lenye ekari 7. NI MFUGAJI Mbali na mambo mengine, Vicky ni mfugaji kama ilivyo asili ya Wasukuma. Anafuga ndege aina ya kanga, kuku wa kisasa na mbuzi.

ANASOMESHA WATOTO WASIOJIWEZA Katika mambo ambayo huenda yanachangia kuchota baraka, mheshimiwa Vicky anawalipia ada ya sekondari watoto yatima, walemavu na wasiojiweza kimaisha, idadi yao ikifikia 75.

KIPATO CHAKE KIKOJE?

Dodoso zinaonesha kwamba, kwa kazi ya uheshimiwa, kwa mwezi anaingiza shilingi milioni 15 ukijumlisha posho zote za ubunge, ujumbe wa kamati ya bunge na mshahara.

AMFUNIKA ANNE MAKINDA Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa, jumba la kifahari la Vicky Kamata linalifunika lile la bosi wake ambaye ni spika wa bunge, mheshimiwa Anne Makinda. Yeye nyumba yake ipo Kijitonyama.

ULINZI NYUMBANI KWAKE USIPIME Uwazi lilipata bahati ya kufika nyumbani kwa Vicky na kukumbana na ulinzi wa mitambo ya kisasa ya kuzuia wezi na majambazi kwa saa 24. Ili mgeni aingie ndani ya geti huhojiwa na walinzi kwa dakika zisizopungua kumi.

HI NDIYO CCM INAYOWATETEA MASIKINI NA WAKULIMA NAWANYONGE.

dr wa magogoni anahusika!tz ni kichwa cha mwendawazimu
 
Itafika mahali hawa tutawakamata tu. Tutaanza na historia ya kodi waliyolipa kisha tutapiga hesabu kujua kipato chao ni halali, vinginevyo watatakiwa kulipa kodi pamoja adhabu, hapo ndipo ule mwisho wa ujanja ujanja wao utakwisha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom