Vichwa 15 vya treni kununuliwa na Serikali

Vichwa 15 vya treni kununuliwa na Serikali

Kwani Bill of landing ilikuwa addressed kwa nani hapa Tanzania?
Usanii mwingine sio mzuri kuwafanya Watanzania wote ni mazwazwa
 
Hii kali ya mwaka. Watanunua kutoka kwanani wakati havina mwenyewe. ? Au fedha itaachwa tu hapo hapo bandarini na watu kujichenga zao?
 
Kama mzigo ulitelekezwa bandarini mwenyewe hajulikan kw nn serikali isitaifishe tu!hizo fedha zifanye kazi nyingine
 
Mkuu aliyeiloga serikali hii kafa! iweje litolewe tamko hapo awali kuwa vichwa vile havina mwenyewe halafu leo useme tunafanya uchunguzi kubaini kama ni vizima tufanye biashara! Biashara hiyo wafanye na shetani au nani? Serikali ilikuwa inajua wazi vichwa vile ni mali yetu na haiwezekani kabisa vikaletwa pale bila kutoa sehemu ya malipo (Dr. Mwakyembe anajua wazi suala hilo). Tukiachia hili ikumbukwe na niliwahi kuviona kwa macho vile vichwa ni mitumba na sheria inakataza serikali kununua mitumba! au ndiyo yale2 ya Bomba mapenzi yanajirudia
na ndio maana kwaki_embe yuko kimyaaaaaa
 
Ni waandishi ndo hawana ueledi au serikali mbona sielewi,Mara vichwa havina mwenyewe tena serikali itakaa na mwenyewe ili kuvinunua vichwa hivyo..!!!!!??????? Napoteza imani
 
Hivi mnasoma kweli mwenyewe fungueni link mtamjua
 
Mwenyewe huyo ni nani wakati havina mwenyewe
Kama havina mwenyewe si ivitaifishe tuu kuna haja ya kuunda tume ambayo itakula pesa kumtafuta mmiliki ambaye ni invisible
BAK tusaidie hapa
Msichanganye habari, vichwa hivi si vile vya Mara ya kwanza, ambavyo vilikosa mwenyewe
 
Hii awamu ina deal na watu wa ajabu sana
Watu wasiojulikana
Wanafunzi Hewa
Wafanyakazi hewa
Vichwa vya train hivina mwenyewe, lakini Serikali inataka kuvinunua, sijui kwa nani?
 
Ingizo jipya la igizo la waliokunywa pombe ya jose` yohani..
 
Serikali inajiuzia yenyewe hivyo vichwa, kuna harufu ya Ufisadi hapa...
 
kwani mwenyewe alishapatikana?

Ha ha haaa!! hii hata darasa la pili B anajua kabisa huu usanii sasa kitu kama hakina mwenyewe si ni swala kutaifisha tu.
 


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeunda tume ya watu 11 kuchunguza vichwa 15 vya treni ambavyo Rais Magufuli alivikuta bandarini vikiwa havina mwenyewe mwanzoni mwezi Julai, 2017 ili kama vitathibitika kuwa ni vizima serikali ivinunue.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema hayo leo jijini Dar es Salaam na kusema kuwa serikali imekusudia kuvinunua vichwa hivyo vya treni kwa matumizi endapo vitakuwa ni vizima na kama havitakuwa na matatizo yoyote.

Prof. Makame amesema endapo vichwa hivyo vikionekana ni vizima kwa mujibu wa uchunguzi ukaofanywa na tume hiyo ya watu 11 iliyoundwa na serikali hivyo serikali itakaa chini na mmiliki wa vichwa hivyo 15 vya treni na kuzungumza naye biashara.

Mwezi Julai Rais Magufuli alipokuwa akiweka jiwe la msingi katika mradi wa upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam alisema ameviona vichwa vya treni zaidi ya 15 ambavyo kwa muda huo vilikuwa vinaonekana havina mmiliki, na kudai kuwa vichwa hivyo vya treni ni vibovu. Rais aliagiza Wizara husika kulifanyia kazi jambo hilo ili ukweli ufahamike kuhusu vichwa hivcyo 15 vya treni.

Chanzo: EATV

Tukumbuke TAKUKURU waliwahi kumtaja mmiliki wa vichwa hivi, pitia hapa=>
TAKUKURU imemtaja mmiliki wa vichwa vya treni vilivyokutwa Bandarini na rais Magufuli kuwa ni Electro-Motive Diesel

Aliyetajwa na TAKUKURU ni mtengenezaji na muagizaji ni TRC ndiyo maana vina chapa yake. Sasa waziri ananunua tena kwa TRC au? sijaelewa kabisa maana shida ilikuwa mambo ya 10% maana vilikuwa na B/L inayoonyesha aliyeviagiza vinginevyo visingepadishwa kwenye meli.
WaTZ Karibu Carabash Mwenge tuanze wknd.
 


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeunda tume ya watu 11 kuchunguza vichwa 15 vya treni ambavyo Rais Magufuli alivikuta bandarini vikiwa havina mwenyewe mwanzoni mwezi Julai, 2017 ili kama vitathibitika kuwa ni vizima serikali ivinunue.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema hayo leo jijini Dar es Salaam na kusema kuwa serikali imekusudia kuvinunua vichwa hivyo vya treni kwa matumizi endapo vitakuwa ni vizima na kama havitakuwa na matatizo yoyote.

Prof. Makame amesema endapo vichwa hivyo vikionekana ni vizima kwa mujibu wa uchunguzi ukaofanywa na tume hiyo ya watu 11 iliyoundwa na serikali hivyo serikali itakaa chini na mmiliki wa vichwa hivyo 15 vya treni na kuzungumza naye biashara.

Mwezi Julai Rais Magufuli alipokuwa akiweka jiwe la msingi katika mradi wa upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam alisema ameviona vichwa vya treni zaidi ya 15 ambavyo kwa muda huo vilikuwa vinaonekana havina mmiliki, na kudai kuwa vichwa hivyo vya treni ni vibovu. Rais aliagiza Wizara husika kulifanyia kazi jambo hilo ili ukweli ufahamike kuhusu vichwa hivcyo 15 vya treni.

Chanzo: EATV

Tukumbuke TAKUKURU waliwahi kumtaja mmiliki wa vichwa hivi, pitia hapa=>
TAKUKURU imemtaja mmiliki wa vichwa vya treni vilivyokutwa Bandarini na rais Magufuli kuwa ni Electro-Motive Diesel

Kazi kwelikweli
 
Pesa ya walipa kodi atalipwa Nani wakati hivyo vichwa vimejileta vyenyewe? Mbona mnatuchanganya!!!
 
Back
Top Bottom