Vichwa 15 vya treni kununuliwa na Serikali

Vichwa 15 vya treni kununuliwa na Serikali

Mwenyewe huyo ni nani wakati havina mwenyewe
Kama havina mwenyewe si ivitaifishe tuu kuna haja ya kuunda tume ambayo itakula pesa kumtafuta mmiliki ambaye ni invisible
BAK tusaidie hapa
Mkuu aliyeiloga serikali hii kafa! iweje litolewe tamko hapo awali kuwa vichwa vile havina mwenyewe halafu leo useme tunafanya uchunguzi kubaini kama ni vizima tufanye biashara! Biashara hiyo wafanye na shetani au nani? Serikali ilikuwa inajua wazi vichwa vile ni mali yetu na haiwezekani kabisa vikaletwa pale bila kutoa sehemu ya malipo (Dr. Mwakyembe anajua wazi suala hilo). Tukiachia hili ikumbukwe na niliwahi kuviona kwa macho vile vichwa ni mitumba na sheria inakataza serikali kununua mitumba! au ndiyo yale2 ya Bomba mapenzi yanajirudia
 


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeunda tume ya watu 11 kuchunguza vichwa 15 vya treni ambavyo Rais Magufuli alivikuta bandarini vikiwa havina mwenyewe mwanzoni mwezi Julai, 2017 ili kama vitathibitika kuwa ni vizima serikali ivinunue.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema hayo leo jijini Dar es Salaam na kusema kuwa serikali imekusudia kuvinunua vichwa hivyo vya treni kwa matumizi endapo vitakuwa ni vizima na kama havitakuwa na matatizo yoyote.

Prof. Makame amesema endapo vichwa hivyo vikionekana ni vizima kwa mujibu wa uchunguzi ukaofanywa na tume hiyo ya watu 11 iliyoundwa na serikali hivyo serikali itakaa chini na mmiliki wa vichwa hivyo 15 vya treni na kuzungumza naye biashara.

Mwezi Julai Rais Magufuli alipokuwa akiweka jiwe la msingi katika mradi wa upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam alisema ameviona vichwa vya treni zaidi ya 15 ambavyo kwa muda huo vilikuwa vinaonekana havina mmiliki, na kudai kuwa vichwa hivyo vya treni ni vibovu. Rais aliagiza Wizara husika kulifanyia kazi jambo hilo ili ukweli ufahamike kuhusu vichwa hivcyo 15 vya treni.

Chanzo: EATV

Tukumbuke TAKUKURU waliwahi kumtaja mmiliki wa vichwa hivi, pitia hapa=>
TAKUKURU imemtaja mmiliki wa vichwa vya treni vilivyokutwa Bandarini na rais Magufuli kuwa ni Electro-Motive Diesel




Habari hapa

Sasa kama hivyo vicha wakishajua havina mwenyewe wakivinunua hizo hela wanampa nani,Nadhani lakusema hapo ni kuvitaifisha.

LUMUMBA
 
mlitutangazia uma kuwa havina mwenyewe na ni vibovu japo kwenye ubavu vikiandikwa "TRL" na leo mnaunda timu ya uchunguzi kuona kama ni vizima halafu mkae chini na mmiliki ili mvinunue.. mbona ni kama maigizo tu yanaendelea

kuna kitu
 
Kutoka watu wasiojulikana mpaka vichwa vya treni ambavyo havijulikani mwenyewe Duuh kali sana
 
Sasa havina mwenyewe Mara serikali itakaa na mwenye Mali awauzie basi sielewi ila nna Mashaka na waandishi wetu ueledi wao.
Mwandishi hana tatizo fungua clip usikilize Prof. Mbalawa anavyoongea halafu rejea matamshi ya bwana magogoni
 
Hii ndio serikali inayopinga ufisadi!

Alafu Raisi alijuaje kama ni vibovu?

Inakuwaje tena leo tena vinafanyiwa uchungu wakati Raisi alishasema ni vibovu?
Naona kaelekeza iundwe tume ya kuvisafisha baada ya kukumbushwa sambusa aliyokula
 
Mkuu aliyeiloga serikali hii kafa! iweje litolewe tamko hapo awali kuwa vichwa vile havina mwenyewe halafu leo useme tunafanya uchunguzi kubaini kama ni vizima tufanye biashara! Biashara hiyo wafanye na shetani au nani? Serikali ilikuwa inajua wazi vichwa vile ni mali yetu na haiwezekani kabisa vikaletwa pale bila kutoa sehemu ya malipo (Dr. Mwakyembe anajua wazi suala hilo). Tukiachia hili ikumbukwe na niliwahi kuviona kwa macho vile vichwa ni mitumba na sheria inakataza serikali kununua mitumba! au ndiyo yale2 ya Bomba mapenzi yanajirudia

Kweli mkuu aliyetuloga kashakufa na kaburi lake halijulikani lilipo tungeenda hata kufukua mifupa yake ingeweza kutusaidia
Mmiliki hajulikani
Mnaunda tume kuvichunguza kama viko salama
Halafu mvinunue
Kutoka kwa nani na nani anapokea pesa
 


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeunda tume ya watu 11 kuchunguza vichwa 15 vya treni ambavyo Rais Magufuli alivikuta bandarini vikiwa havina mwenyewe mwanzoni mwezi Julai, 2017 ili kama vitathibitika kuwa ni vizima serikali ivinunue.

Prof. Makame amesema endapo vichwa hivyo vikionekana ni vizima kwa mujibu wa uchunguzi ukaofanywa na tume hiyo ya watu 11 iliyoundwa na serikali hivyo serikali itakaa chini na mmiliki wa vichwa hivyo 15 vya treni na kuzungumza naye biashara.

Chanzo: EATV
Hapo tu.
 
Vichwa vya Mwakyembe labda kama anaona aibu kumtengua Mwakyembe ambae alikuwa waziri....mawasiliano Uchukuzi....wakaagiza vichwa na mabehewa yale fake.....ambayo w inflate ma bei makubwaa
 
Vilitelekezwa? Maana havikuwa na mwenyewe je?vimelipiwa ushuru? Kodi ya bandari?
Nani alikuwa akivilipia?

Mhhhhh
 
Si mmeambiwa havina mwenyewe,utasikia bilioni kadhaa zimetumika kununua
 
1. Vimekutwa havina mwenyewe halafu tunavinunua hela tunampa nani
2. Alivyosema ni vibovu alikuwa hajachunguza, nikimaanisha aliropoka?
 
kweli watanzania tunafanywa wajinga kiasi hiki? we prof. wa manzese utanunua kwa nani wakati mwenye navyo humjui? kweli maprof wa UD hawana tofauti na yule wa korogwe maji mafupi
 
Anaenyoosha maelezo yuko Nairobi kwaiyo wanafanya faster kabla ajarudi wataumbuka

Vibovu vinanunuliwa then vinaenda chuo cha usafirishaji kujifunzia mana avitoweza kaz kama ile kivuko chetu nw kitakua cha mafunzo na spear part ya jeshi
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ndio maana hii nchi ina maajabu mengi kuzidi nchi yoyote duniani!
Sasa hizo pesa watamlipa nani wakati mmiliki hajulikani!? ...pamoja na madhaifu yaliyopo lakini kuna watu unaweza kuwa unawaheshimu kama huyu Prof. Waziri ila ukiangalia anachoongea na body language inakurudisha kwenye msemo wa mzee Mwinyi! Nilisha 'unfollow' mange kimambi kote lakini mambo kama haya yanafanya nianze kumfollow tena.
 
Mmmh hawa watu naona wanasubiria siku ya kiama tu,vichwa havina mwenyewe harafu mkae chini na mwenyewe mfanye biashara hii inaingia akilini kweli?tuoneeni huruma kidogo.
 
Back
Top Bottom