Vibweka nyumba za kupanga, unakumbuka nini?

Vibweka nyumba za kupanga, unakumbuka nini?

Kuna wale ambao siku wakila maini, lazima walie nje,kuna mwengine akinunua kuku lazima amchinjie nyumbani, kuku lazima afinywe kwanza ili apige kelele watu wote mjue.
Hahaha hakyanani nimecheka, eti kuku lazima afinywe kidogo.
 
Magomeni nyumba ya vyumba sita ni shida, mtu kanivunjia chombo kimoja nikabeba vibatibati vyake vyote nikaenda tupa chooni siku tatu zote nikikuta vyombo vyake nakanyaga natupa chooni
yeye anakaa uwani anakujapikia katikati ya mlango wangu nikitoka nikikuta anapika naruka badala ya kupita pembeni, wakijidai vizibo wewe zibuka zaidi heshima itakuwepo tu
 
Last edited:

Pole sana mkuu unaonekana wewe mtata sana....sisi wenzako tumeshakubali matokeo...
 
Magomeni nyumba ya vyumba sita ni shida, mtu kanivunjia chombo kimoja nikabeba vibatibati vyake vyote nikaenda tupa chooni siku tatu zote nikikuta vyombo vyake nakanyaga natupa chooni
yeye anakaa uwani anakujapikia katikati ya mlango wangu nikitoka nikikuta anapika naruka badala ya kupita pembeni, wakijidai vizibo wewe zibuka zaidi heshima itakuwepo tu
Hii Inahitaji ujasiri hasa
 
Duh, ni kweli kabisa hili, huwa wanachangisha hela kwa wapangaji wote lakini umeme ananunua wa hela ndogo tu, hudhubutu kumuuliza atakujibu hovyo sana.
Kila kazi ina "Malupulupu yake" Hayo ndo malupulupu ya mwenye Nyumba.
 
dah,umenikumbusha kitu,hlf nimewaza sana nilipokumbuka jinsi bi mkubwa alivogombana na mpangaji mwenzake kwa kurushiana mitusi ya nguoni,nusu wapigane wakiwa chooni kisa zamu za kusafisha vyoo!
yaani bi mkubwa alikuwa anakerwa sna na jinc huyu jirani yake anavosafisha vyoo inapofika zamu yake(alikuwa anaripuaripua tu)na wakat wenzake ikifika zamu zao wanang'arisha hasa...sasa siku iyo bimkubwa alishindwa kumvumilia baada ya kuona huyu bi dada hajirekebishi,sas cku iyo ikabidi amtolee uvivu aise baada ya kumtaka arudie kusafisha choo aise kiliwaka apo!mwish wa siku kwa kuwa bimkubwa wangu ni mkubwa kumzidi huy dada,hlf kama ana ubabe flani ivi yule dada ilibidi aje chini na kukubali kurudia kusafisha choo. Lakini nilijickia aibu sana ikabidi nikajiliwaze maskani...nyumba za kupanga hizi mengi yanatokea.
 
Daaah!!kuna jamaa alikua fundi pikipiki akirud anatukuta tumefungulia mziki kwa saut!!akatuambia oya punguzen saut,tukamjibu kila mtu na starehe yake jamaa akasema poa,akaondoka afu akarud na bonge la baja akaingia nalo ndani!!akaliwasha afu akawa anavuta mafuta aisee nyumba nzima tukatoka,akasema kila mtu na starehe yake huku kashika bonge la spana!!nyie pigen mzik mi na baja langu afu asogee mtu nimpasue na spana!!
 
Back
Top Bottom