Vibweka nyumba za kupanga, unakumbuka nini?

Vibweka nyumba za kupanga, unakumbuka nini?

Kama hujawahi kuishi nyumba za kupanga (kwa muktadha huu chumba kimoja) hasa uswazi utakuwa umekosa mengi sana.

Wengi wetu tumeanzia maisha kwenye chumba kimoja kabla ya kupanga nyumba nzima na hatimaye kujikomboa na zetu wenyewe... Kwahiyo kila mtu hakosi cha kusimulia.

Kinachoniacha hoi ni masharti na Vibweka vya mwenye nyumba au wapangaji. Kuna wenye nyumba hawataki masingo, wengine hawataki wana ndoa wengine hawataki watoto.

Kuna wenye nyumba hawapokei watu wa imani fulani hapo ili upate chumba inabidi ujipe jina fulani. Kuna wenye nyumba mwisho kuingia bafuni kuoga ni saa nne usiku, baada ya hapo litakalokupata ni juu yako.

Kuna wenye nyumba hawataki wageni wakutembelee au wageni wa jinsia fulani. Masharti ni mengi na yanatofautiana

Ukija kwa wapangaji wenzako ni shida.

Kuna baadhi huchaguliwa kusimamia nyumba hapo mtakoma. Ukiwa bachelor halafu nyumba imejaa wanawake pia ni shida hasa siku aje demu wako.

Ugomvi na majigambo kati ya wanawake na wanawake ni vitu vya kawaida hasa kuringishiana kwenye mavazi, vyakula na samani za ndani. Vijembe vya kanga taarab na vigodoro ni mambo ya kawaida sana, zamu za usafi wa korido Choo bafu na uwanja.

Haya yote yanaletwa kwakuwa mnakutana watu wa makabila tofauti, imani tofauti historia tofauti elimu tofauti n.k. n.k.

Ukitoka kuishi chumba cha kupanga hasa uswazi ni sawa na kuhitimu degree ya kwanza kwenye mambo ya kijamii.
Haya tumeshajua na wewe unamiliki kibanda. Weka japo kapicha basi tuhakikishe kama usemacho ni sahihi.
 
Haya tumeshajua na wewe unamiliki kibanda. Weka japo kapicha basi tuhakikishe kama usemacho ni sahihi.
1452753030752.jpg
utoto raha sana
 
KAKA mshana jr ahsante! wengi wetu umetukumbusha mbali sana! daah, ila kinachotia moyo, wengi wetu tulikuwa tunaweza kuhimili changamoto za nyumba za kupanga, na ndio maana unakuta kuna watu wamekaa ktk hizi nyuma miaka na miaka, wengine mpaka wamejukuu, wameozesha! lakini changamoto ni hizi hizi! daah, nyumba za kupanga ni kweli, mimi najihesabu nna degree 3, 2 zile za chuo na ile ya nyumba za kupanga kuanzia Vingunguti, Ilala quarters, Kinondoni shamba, Kinondoni Moscow mpk Kibaha, aisee hii ni degree 1st class mkuu!
 
Halafu Kama mwenye nyumba anakaa hapo hapo yeye ndio mnunuaji na kamwe hawaonyeshi risiti

Hiyo ilinikuta mwaka 98 Nilipanga Nyumba flan mwenye Nyumba kila ikifika mwisho wa Mwezi kipindi hicho nilikuwa msela kurudi home usiku so Anachofanya anandaa Bili yake ya Umeme anagawa kila chumba kama upo anakupa kama hupo anachomeka kiKARATASI kwenye Tundu ya Funguo so ukirudi kabla hujatumbukiza Funguo lazima ukutane na MEMO ya UMEME shida ilikuwa Bili ya kweli inapotoka duuh....Kipindi kile meter zilikuwa zile za Ringi...mnaweza kukaa hata miezi mi3 Bill haijaja...
 
Kuna wale ambao siku wakila maini, lazima walie nje,kuna mwengine akinunua kuku lazima amchinjie nyumbani, kuku lazima afinywe kwanza ili apige kelele watu wote mjue.
Shobo za uswazi halafu kwa kupenda cheap Jewelleries na manukato vingi vikiwa vya kuazima siku hiyo nyumba yote mtamjua
 
Me Nadhani Kero Kubwa Kuliko Zote Ni Zile Sauti Za Msuguano Wa Kitanda Pia Zikichagizwa Na Miguno Ya Kimahaba Toka Chumba Jilani.
Mkuu Usimbee Yakukute Hayo Mambo Wakati Upo Single Kwani Unaweza Ukahama Nyumba Bila Kupenda .
Halafu kuna wakati wanayoyafanya huko ni aibu tupu lakini wanafanya kwa sauti kuuubwaa
 
Kama hujawahi kuishi nyumba za kupanga (kwa muktadha huu chumba kimoja) hasa uswazi utakuwa umekosa mengi sana.

Wengi wetu tumeanzia maisha kwenye chumba kimoja kabla ya kupanga nyumba nzima na hatimaye kujikomboa na zetu wenyewe... Kwahiyo kila mtu hakosi cha kusimulia.

Kinachoniacha hoi ni masharti na Vibweka vya mwenye nyumba au wapangaji. Kuna wenye nyumba hawataki masingo, wengine hawataki wana ndoa wengine hawataki watoto.

Kuna wenye nyumba hawapokei watu wa imani fulani hapo ili upate chumba inabidi ujipe jina fulani. Kuna wenye nyumba mwisho kuingia bafuni kuoga ni saa nne usiku, baada ya hapo litakalokupata ni juu yako.

Kuna wenye nyumba hawataki wageni wakutembelee au wageni wa jinsia fulani. Masharti ni mengi na yanatofautiana

Ukija kwa wapangaji wenzako ni shida.

Kuna baadhi huchaguliwa kusimamia nyumba hapo mtakoma. Ukiwa bachelor halafu nyumba imejaa wanawake pia ni shida hasa siku aje demu wako.

Ugomvi na majigambo kati ya wanawake na wanawake ni vitu vya kawaida hasa kuringishiana kwenye mavazi, vyakula na samani za ndani. Vijembe vya kanga taarab na vigodoro ni mambo ya kawaida sana, zamu za usafi wa korido Choo bafu na uwanja.

Haya yote yanaletwa kwakuwa mnakutana watu wa makabila tofauti, imani tofauti historia tofauti elimu tofauti n.k. n.k.

Ukitoka kuishi chumba cha kupanga hasa uswazi ni sawa na kuhitimu degree ya kwanza kwenye mambo ya kijamii.
kuna nyumb moja niliwahi kupanga kuna jamaa mpangaji mwenzangu alikua mjeda huyu jomba akilewa bas anapita kukojolea milango yote mwingine no demu alikua akiingia toilet kudadadek choo lazma kizibe ana mavi makubwa balaaa ila uswazi raha full service 24/7
 
Back
Top Bottom