Vibweka nyumba za kupanga, unakumbuka nini?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
280,635
729,525
Kama hujawahi kuishi nyumba za kupanga (kwa muktadha huu chumba kimoja) hasa uswazi utakuwa umekosa mengi sana.

Wengi wetu tumeanzia maisha kwenye chumba kimoja kabla ya kupanga nyumba nzima na hatimaye kujikomboa na zetu wenyewe... Kwahiyo kila mtu hakosi cha kusimulia.

Kinachoniacha hoi ni masharti na Vibweka vya mwenye nyumba au wapangaji. Kuna wenye nyumba hawataki masingo, wengine hawataki wana ndoa wengine hawataki watoto.

Kuna wenye nyumba hawapokei watu wa imani fulani hapo ili upate chumba inabidi ujipe jina fulani. Kuna wenye nyumba mwisho kuingia bafuni kuoga ni saa nne usiku, baada ya hapo litakalokupata ni juu yako.

Kuna wenye nyumba hawataki wageni wakutembelee au wageni wa jinsia fulani. Masharti ni mengi na yanatofautiana

Ukija kwa wapangaji wenzako ni shida.

Kuna baadhi huchaguliwa kusimamia nyumba hapo mtakoma. Ukiwa bachelor halafu nyumba imejaa wanawake pia ni shida hasa siku aje demu wako.

Ugomvi na majigambo kati ya wanawake na wanawake ni vitu vya kawaida hasa kuringishiana kwenye mavazi, vyakula na samani za ndani. Vijembe vya kanga taarab na vigodoro ni mambo ya kawaida sana, zamu za usafi wa korido Choo bafu na uwanja.

Haya yote yanaletwa kwakuwa mnakutana watu wa makabila tofauti, imani tofauti historia tofauti elimu tofauti n.k. n.k.

Ukitoka kuishi chumba cha kupanga hasa uswazi ni sawa na kuhitimu degree ya kwanza kwenye mambo ya kijamii.
 
1452745344287.jpg
1452745355745.jpg
1452745403221.jpg
 
Hahahahahaha swaala la umeme nishida,,,,mchana hakuna kuwasha usiku tu
Hiyo huwa noma kweli kweli. Nakumbuka kikao kimoja kujadili bill ya umeme moja ya maazimio ilikuwa watumiaji wakubwa walipe zaidi.
Mmoja wa watuhumiwa wa matumizi makubwa akapiga marufuku wapangaji wenzie kwenda kuomba maji ya baridi, kuazima pasi yake ya umeme.
Mwenye Tv akapiga marufuku kwenda kuangalia taarifa ya habari au mpira /boxing.
Nusura kikao kivunjike lakini mwishowe ikakubaliwa kuwa kila mtu alipe sawa!
 
Hiyo huwa noma kweli kweli. Nakumbuka kikao kimoja kujadili bill ya umeme moja ya maazimio ilikuwa watumiaji wakubwa walipe zaidi.
Mmoja wa watuhumiwa wa matumizi makubwa akapiga marufuku wapangaji wenzie kwenda kuomba maji ya baridi, kuazima pasi yake ya umeme.
Mwenye Tv akapiga marufuku kwenda kuangalia taarifa ya habari au mpira /boxing.
Nusura kikao kivunjike lakini mwishowe ikakubaliwa kuwa kila mtu alipe sawa!
Hapo waliwakomesha wale watata. Watu kila siku wanaazima pasi ila likija swala la kulipa umeme wanasema wao hawana pasi. Ukifika muda wa habari sebule haitoshi kwa jinsi watu wanavyojaa kuangalia tv halafu mwisho wa siku unaambiwa mwenye Tv ulipe zaidi lol.
 
Mi na sista angu tulipanga chumba Unguja wakati fulani kwa muda wa miezi 3 ambao tulikuwa field .
Yani ilikuwa ndo mara yetu ya kwanza kupanga lakini tulikutana na masharti makubwa kuliko hata umri wetu.
1. Wageni jinsia ya kiume hawaruhusiwi kabisa hata kama ni mzazi wako.
2. Marufuku kusikiliza nyimbo za dini ( za kikristo)
3. Haturuhusiwi kurudi nyumbani zaidi ya saa 4 usiku hata kama tunatoka kazini.
4. Ni marufuku kuongea chooni na ikitokea umevunja sharti hilo litakalokukuta ni juu yako.
5. Na masharti mengine kibao madogo madogo ambayo hayatekelezeki ikiwepo kutopiga pasi ili kusave TUKUZA, .
Tuliyavunja karibu yote na kufukuzwa hata Kabla ya mwezi kwisha,
 
Back
Top Bottom