Mada za kijinga, zisizokuwa na maana, zenye kejeli, chuki, dharau, majigambo, dhiaka, sifa, ubinafsi, matusi n.k ndizo ambazo zina washabiki wengi humu jamvini, kama hauamini stay tuned..... Hata wale ambao huwa hawachangii chochote utawaona nao wanajitokeza kuanza kutoa matusi kwa dini na imani nyingine. Jinsi inavyoonekana ni wazi kabisa hawa wazungu na waarabu wamejua kuteka na kuchezea akili za waafrika. Yaani waafrika tumekuwa kama mapumbavu fulani na hizi imani kisha cha kushangaza ni kwamba sijui kwenye nyumba za ibada somo kubwa linakuwa ni kutukana dini ya mwenzako ndio unakuwa unafutiwa madhambi, nashindwa kuelewa, maana yake unakuta mtu anataja kabisa iman yake kisha anatoa matusi kwa imani nyingine. Waafrika wenzangu humu jamvini ebu tuamke kwanza na kuachana na huu utumwa, kama unafuata iman fulani basi wewe endelea kuifuata, lakini jaribu angalau kuheshimu imani za wengine.
Yaani ukiangalia baadhi ya statements humu ndani unaweza hata kulia na kushangaa kweli watanzania wa jamiiforums tunaojiita Great Thinkers tumefikia huku.
Lakini mwisho wa siku naomba hizi chuki zenu mnazoonyeshana wazi ziishie humu humu kwenye keyboards na monitors, lakini zisifike mtaani manake itakuwa kama C.A.R vile.
Mungu wabariki watanzania wote, Mungu Bariki waafrika wote ili angalau tutokwe na hizi tongotongo.