Vibaka wananisumbua sana mtaani, nifanyeje?

Vibaka wananisumbua sana mtaani, nifanyeje?

Fanyeni vikao wakaazi na uongozi wa mtaa mjitafakari njia bora ya kuimarisha ulinzi
 
Mkuu nunua gun hata kibastola kidogo, vibaka huwa hawatoki mbali ni hapohapo mtaani. Sasa unatakiwa ufanye watu wajue unamilliki gun kivipi?.

Ukishanunua wewe amka usiku hata sa6 wengi wanakua hawajalala huu muda, piga bastola juu paah! Paaahh! Huku unaongea kwasauti Pumbavu sana nyie, washenzi nyie, mnabahati sana.

Ndugu yangu nakuhakikishia hapo mtaani heshima inaongezeka sana wataambizana kama upo uswahilini taarifa zinatembea sana hao vibaka hawaji sogea tena, gun inaogopeka sana. Ukipita mtaani watakua wanakuangalia tu huku wanaoneshana vidole[emoji28][emoji28].

Hii mbinu aliitumiaga babu yangu wakt anaamia mbagala enzi hzo vibaka kma wote, alifanya hvo toka sikuhyo ni heshima alloohhh
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
1. Weka CCTV camera

2. Fuga Mbwa

3. Fanya Propaganda Kati ya hizi;
a) Waite watu wenye Yale majoka makubwa wajifanye wanapita mtaani kuuza majoka ya ulinzi wakiwa na vipaza sauti huku wakionyesha hayo majoka.
Nenda pale wanapotangazia Jifanye unainunua joka kubwa watu wakiwa wanakuona.
Kisha wakupelekee nyumbani watu wakiona.

Baada ya hapo, nenda Stationary andika bango la tahadhari, Nyumba hii inalindwa na jokakubwa.
Kisha uje unipe Mrejesho.

Duniani 90% watu huogopa nyoka kuliko kiumbe yoyote Yule.
Mbwa sio wengi wanaomuogopa.

B) propaganda ya Waganga.
Tengeneza tukio bandia la kuwa nyumba yako inalindwa na Majini.
Hii inahitaji utafute Vijana waliobobea katika uigizaji, watokee mbali na hapo Kibaha.
Utajua namna ya kumalizana na Polisi baada ya Vijana hao kupelekwa Korokoroni.

4. Hama hapo ikiwa yote yameshindikana.
 
Nimejitahidi njia nyingi saana kuweza kukabiliana nao imekua ngumu. Naombeni msaada kiukweli nimefeli.

Juhudi chache

Nimejitahidi kuishi kama mlinzi kuamka usiku mara mbili na kuzunguka nyumba.

Ila leo saa mbili nimetoka kwenda dukani ndani ya saa moja narudi watoto wananiambia dirisha limefunguliwa na pazia kuanguka, nimefatilia nikagundua wamekuja vibaka wameiba vitu vichache.

Msaada wa mawazo tafadhali.
Ndugu pole sana. Maisha ni kusaidiana. Vibaka nao wana familia. Ukiibiwa ujue mtoto wa mwanaume mwenzio anaenda chooni. Tukae tukijua kuwa hawa vibaka ni ndugu, jirani ama watoto wa rafiki zetu. Tumewafuga wenyewe. Maisha ya leo ni full kupigana. Ukizubaa hata mkeo anakusachi. Ukipigwa kitaani nawe unaenda kumpiga Mwajiri wako kazini.
.
.
Daa nahisi nimefungulia koki
 
Imarisha usalama wa mali zako kulingana na uwezo wako
Wengi waliopo uswahili hawana mpango wa kufata mitindo ya ujenzi zaidi wao hujali usalama tu...kama upo uswahilini weka madirisha ya milango ikifika usiku unafunga au kama una hela ya kutosha tumia ushauri wa wadau waliosema.
 
Ina uzio niliongeza hadi kozi za tofauri ili wasiruke ukuta ila upande mmoja ndio hakuna uzio kwahiyo wafungua dirisha upande huo
Huo upande ni Kuna njia ya wapita kwa miguu?
 
Huo upande fuga kuku wa kienyeji,wale usiku lazima walie wakiona kitu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom