Jumanne Mkota
JF-Expert Member
- Jan 25, 2012
- 3,011
- 1,794
Hapo nyuma ya huo mtaa mbona kuna wakubwa zao ila wao ni wavaa suti! Ni sehemu tu ya kugawana majukumu! Nyie kaben hapa sie tukabe huku
Ulinzi shirikishi!
Ulinzi shirikishi!
Ni mita ngapi kutoka ikulu ya nchi!?
Polisi labda wako kwenye maandalizi ya kusimamia uchaguzi nadhani wakimaliza hilo watahamia hilo eneo kudhibiti hali ya mambo. Sina uhakika hadi wakati huo watakuwa wameathirika raia wema wangapi!
Ukistaajabu ya Musa hapo nyuma ya huo mjengo si ndio tuliambiwa kuna mtaa ambao una kila aina ya sodona au nimekosea njia?
Binafsi walitaka kunikata mapanga.Nilikuwa nafanya jogging majira ya saa moja usiku.Nilipofika karibu na viwanja vya basketball wakatokea jamaa wanne na mapanga.Ni bahati tu niko fit na waliponikimbiza niliwaaacha mbali.
Ni aibu kwa eneo hili kuwa na majambazi.Hili ni eneo karibu na ikulu na polisi wa doria wanapita kila mara.
Hivi ni kwa nini polisi wasiyawekee mtego majambazi haya wakayanasa.?
Hapo nyuma ya huo mtaa mbona kuna wakubwa zao ila wao ni wavaa suti! Ni sehemu tu ya kugawana majukumu! Nyie kaben hapa sie tukabe huku
Zifungwe taa,..km vipi, askari waweke ulinzi..
Una maana Polisi wetu hushirikiana nao, au ulimaanisha Usalama wa Taifa?
yote ni majibu sahihi kwani haiingii akilini kusema kamera za ulinzi za ikulu zinaona mwisho getin tu na hao polisi kujibu ni matukio ya kawaida bila kuongeza nguvu ni kudhihirisha ushiriki wao. Hivi vyombo viwili yafaa kuacha kutegeana kwa kusema swala la vibaka ni la polisi ilihali hapo ni usoni na machoni pa nchi. Hebu wajibikeni kwa pamoja ili kuuondoa uchafu huo hapo.
Hello wana JF,
Nimeshuhudia matukio ya vibaka kuvamia wapita njia (Ocean Road) kwenye mpaka wa IKULU mara mbili.
Tukio la kwanza lilitokea majira ya jioni baada ya wanawake wawili kuegesha gari yao pembeni kwa dharura, walivamiwa na vibaka wakanyang'anywa simu na mikoba yao na niliposimama kutoa msaada, vibaka hao walikimbia wakiwa na mali walizopora.
Pili imetokea juma lililopita saa sita mchana baada ya kijana mmoja mtembea kwa miguu kusimamishwa na vibaka, kumpiga makonde mazito baada ya kupinga amri yao huku wengine wakimpekua mifukoni wakachukua simu pesa na viatu kisha kutimkia ufukweni.
Tukio hilo lilitolewa taarifa kituo cha polisi Kivukoni na polisi walikiri ni matukio ya kawaida pale hivyo watafuatilia!
Wadau, Nini kifanyike?

Mkuu Unasemea Jioni ya saa ngapi? Tua nzie hapo