A
Anonymous
Guest
Sisi wananchi wa Mtaa wa Ruhuwiko katika Manispaa ya Songea tunakabiliwa na changamoto kubwa ya vitendo vya wizi vinavyofanywa na vibaka ambao wamekuwa wakivamia maeneo yetu ya makazi mara kwa mara.
Matukio haya hutokea zaidi nyakati za usiku, ambapo wahalifu hao huingia kwenye makazi ya wananchi na kusababisha hofu na hasara mbalimbali. Ingawa tumekuwa tukijitahidi kuimarisha ulinzi shirikishi kwa kujikusanya na kufanya doria za wananchi, hali inaonyesha kuwa uwezo wetu unaelekea kuzidiwa na ukubwa wa tatizo hili.
Kutokana na hali hiyo, tunaomba Jeshi la Polisi kuongeza doria katika eneo letu ili kusaidia kudhibiti vitendo hivi vya uhalifu na kurejesha usalama wa wananchi.
Kwa sasa, wakazi wengi wanaishi kwa hofu kutokana na ongezeko la matukio ya wizi na kuhisi kutokuwa salama katika makazi yao. Tunaamini kuwa uwepo wa doria za mara kwa mara utasaidia kuimarisha usalama na kuwarejeshea wananchi amani na utulivu.