Hello wana JF,
Nimeshuhudia matukio ya vibaka kuvamia wapita njia (Ocean Road) kwenye mpaka wa IKULU mara mbili.
Tukio la kwanza lilitokea majira ya jioni baada ya wanawake wawili kuegesha gari yao pembeni kwa dharura, walivamiwa na vibaka wakanyang'anywa simu na mikoba yao na niliposimama kutoa msaada, vibaka hao walikimbia wakiwa na mali walizopora.
Pili imetokea juma lililopita saa sita mchana baada ya kijana mmoja mtembea kwa miguu kusimamishwa na vibaka, kumpiga makonde mazito baada ya kupinga amri yao huku wengine wakimpekua mifukoni wakachukua simu pesa na viatu kisha kutimkia ufukweni.
Tukio hilo lilitolewa taarifa kituo cha polisi Kivukoni na polisi walikiri ni matukio ya kawaida pale hivyo watafuatilia!
Wadau, Nini kifanyike?
Kwa tahadhari zaidi soma;
Jihadhari unapokuwa maeneo haya Dar es Salaam
Daktari Mgiriki auwawa Tanzania..

Vijana 6 wamekamatwa usiku huu baada ya kuhusika na wizi kwa kumtishia muuza sigara na karanga maeneo ya Ocean Road kuelekea BOT.
Vijana hawa walimtishia huyu muuzaji sigara akiwa na pakiti kumi za sigara na karanga zisizozidi za sh5000! Baada ya kuoneshwa panga na kisu aliwakabidhi mzigo na kutishiwa kuuawa kama atapiga kelele!
Kijana akajificha sehemu alipoona pikpiki akaomba msaada wakaenda kuwasubiria maeneo ya KFC!
Hapo ndipo kijana akishirikiana na walinzi wengine waliokuwa wakiwasubiri kwa hamu wakapiga ukunga wa wezi! Wazee wa CRDB wakamaliza kazi yao huku waungwana wanawarushia mawe vichwani.
Nimeacha wanasubiri defender kuwachukua! Samahani dini yangu hairuhusu kupiga picha za wenye damu, ningewawekea!
Muwe makini area hiyo usiku kuanzia saa moja!
Ndugu nakushauri kuanzia saa moja jioni usipite njia ile ya ocean road au sasa hivi inaitwa Barrack Obama drive nyuma ya Hotel ya Kimataifa ya Serena, uwe na gari au hata kwa miguu.
Kuna majambazi balaa watakuua kabisa uteketee duniani. Ukipita na gari hakikisha halitakuharibikia maeneo yale wala kupata pancha. Na ikipata pancha we tembea hivyo hivyo la sivyo mwisho wa dunia utakuwa umepiga hodi kwako. Ukisimama tu hutajua wametokea wapi na si zaidi ya mmoja.
Yamemtokea ndugu yangu aliyekuwa anatokea Hospitali ya Kansa Ocean Road saa mbili kasoro akasimamisha gari jirani na hospitali ya Aghakhan ili apate haja ndogo... Daaaaahh walitokea majambazi na mapanga na kilichotokea ni bas tu.
Nasikitika sana. Matukio ni mengi mno ya ocean road. Na urefu wa lile pori la viwanja vya Golf na Cricket ni mrefu sana kuanzia hospitali ya Aghakhan had kwenye uwanja wa basketball..Usipite usiku njia ile iwe kwa gari au kwa miguu.
NARUDIA TENA.. KWA UHAI WAKO KUENDELEA KUDUMU USIPITE OCEAN ROAD (BARRACK OBAMA DRIVE) IKIFIKA SAA MOJA USIKU UWE NA GARI AU HATA KWA MIGUU.
KULE NI JEHANAMU WATAKUUA...
Polisi tusaidieni!
Waheshimiwa,
Jana usiku wa saa mbili na nusu katika eneo la daraja la Selander, nilishuhudia mwanaume mwenye asili ya kizungu akiwa kang'ang'aniwa na vijana wa kibongo kama sita hivi kwa nia ya 'kumsachi' na kumpora
Matukio kama haya yalivuma sana miezi kadhaa ya nyuma kisha kukawa shwari, na wengi wetu labda tulidhani sasa hakuna hatari tena (mimi nikiwemo)
kwa nililoshuhudia jana ni wazi kwamba bado tunapaswa kuwa makini sana tupitapo maeneo yale.
Cha kushangaza hili lilitokea almost right infront of the police station, mwanzo kabisa wa daraja ukiwa unatokea mjini.
Usalama hakuna kwa eneo la kituo cha polisi , je huko vichochoroni kwetu??
Anyways it was just a word to alert you all, msijiachie mkipita pale kwenye gari na simu zenu na 'pochi' zitadakwa kama mwanzo.
TEKEA PEOPLE
Kwa tahadhari zaidi soma;
Jihadhari unapokuwa maeneo haya Dar es Salaam
Daktari Mgiriki auwawa Tanzania..