Vibaka kuzunguka Ikulu, Usalama upo?

Vibaka kuzunguka Ikulu, Usalama upo?

Yaanukitakakuchekaingiajfukutanenakinapdidyhhhhhhaaaaaaaweraaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Weraaaaaweraaaaeapiiishyyy mamaaawambagaraamisschahgaaa!!wapii dinaaaa kamanazikoroma ukigusaa ninahomaaa
 
Ndugu nakushauri kuanzia saa moja jioni usipite njia ile ya ocean road au sasa hivi inaitwa Barrack Obama drive nyuma ya Hotel ya Kimataifa ya Serena, uwe na gari au hata kwa miguu.

Kuna majambazi balaa watakuua kabisa uteketee duniani. Ukipita na gari hakikisha halitakuharibikia maeneo yale wala kupata pancha. Na ikipata pancha we tembea hivyo hivyo la sivyo mwisho wa dunia utakuwa umepiga hodi kwako. Ukisimama tu hutajua wametokea wapi na si zaidi ya mmoja.

Yamemtokea ndugu yangu aliyekuwa anatokea Hospitali ya Kansa Ocean Road saa mbili kasoro akasimamisha gari jirani na hospitali ya Aghakhan ili apate haja ndogo... Daaaaahh walitokea majambazi na mapanga na kilichotokea ni bas tu.

Nasikitika sana. Matukio ni mengi mno ya ocean road. Na urefu wa lile pori la viwanja vya Golf na Cricket ni mrefu sana kuanzia hospitali ya Aghakhan had kwenye uwanja wa basketball..Usipite usiku njia ile iwe kwa gari au kwa miguu.

NARUDIA TENA.. KWA UHAI WAKO KUENDELEA KUDUMU USIPITE OCEAN ROAD (BARRACK OBAMA DRIVE) IKIFIKA SAA MOJA USIKU UWE NA GARI AU HATA KWA MIGUU.

KULE NI JEHANAMU WATAKUUA...

Polisi tusaidieni!
 
Duuh leo nimepita kwa mguu mida kama ya saa moja kamili hivi njia ambayo unaona kile kiwanja sijui cha mpira nilikua na kamera kubwa njia nzima roho ilikua inasita ilibidi nitembee kati kati ya barabara sidhani kama nitapita tena
 
Ni kweli eneo hilo hata mimi niliwahi kupatwa na majanga ilikuwa saa moja kasoro jioni siku ya jpili.
 
Hii habari sio mara ya kwanza kuisikia ina maana mpk leo Polis hawajachukua hatua tu.

Sio huko tu hata hapo salenda huo msitu wa mto msimbazi mchana kweupe pyeee kukiwa na foleni tu kosa jamaa huwa wanaibuka kama nguchiro vile yaani utafikiri unaangalia sinema na huwa wanavaa tshrt nyeusi na kituo cha police kipo hapo hapo jirani.
 
Binafsi walitaka kunikata mapanga.Nilikuwa nafanya jogging majira ya saa moja usiku.Nilipofika karibu na viwanja vya basketball wakatokea jamaa wanne na mapanga.Ni bahati tu niko fit na waliponikimbiza niliwaaacha mbali.

Ni aibu kwa eneo hili kuwa na majambazi.Hili ni eneo karibu na ikulu na polisi wa doria wanapita kila mara.

Hivi ni kwa nini polisi wasiyawekee mtego majambazi haya wakayanasa.?
 
saiv uhalifu n kila pahala ,kule maeneo y tabata kun vijana wanapiga ngeta saa moja tu kigiza kikishaanz kuingia..
 
Binafsi walitaka kunikata mapanga.Nilikuwa nafanya jogging majira ya saa moja usiku.Nilipofika karibu na viwanja vya basketball wakatokea jamaa wanne na mapanga.Ni bahati tu niko fit na waliponikimbiza niliwaaacha mbali.

Ni aibu kwa eneo hili kuwa na majambazi.Hili ni eneo karibu na ikulu na polisi wa doria wanapita kila mara.

Hivi ni kwa nini polisi wasiyawekee mtego majambazi haya wakayanasa.?

Polisi wapo huku kwenye vibanda vya gongo na maskani za wavuta bange ..!
 
Duuh leo nimepita kwa mguu mida kama ya saa moja kamili hivi njia ambayo unaona kile kiwanja sijui cha mpira nilikua na kamera kubwa njia nzima roho ilikua inasita ilibidi nitembee kati kati ya barabara sidhani kama nitapita tena
hata hivo siku ingine ukishakuwa kwenye hali kama hiyo usithubutu kutembea katikati ya barabara maana ni rahisi kuwa spotted unatakiwa uwe unapita pembezoni kabisa mahali ambapo adui hawezi kukuona kwa urahisi.

Huu ujanja ulinisaidia sana ku survive wahuni wa maeneo hatari kama ungalimited yaani uwe salama ukishachelewa usiku pita kwenye vichochoro maana wao timing yao kubwa wanafanyia kwenye barabara kubwa maana wengi huwa wanakuwa wanatumia pale wanapochelewa.

copy that
 
Back
Top Bottom