Kumekuwa na ujambazi was kutumia visu namapanga!!majuzi shemejio alinipigia nikamchukue ifm!!nilipopita oceanaroad nikakuta MTU anaporwa pikipiki walipoona nasimama wakakimbilia upande was bfoward!!nkawatonya jamaa walinzi nikarudinao nikakuta jamaa wamemkata mkono awezikuendesha tukapiga ukunga wakajaa watu tukasubiri defender wakambeba!! Maisha borakwa kilamtz!bado was Amboni awajafika loh wakivuka KWAHERI PWANI KARIBU DSM LOH SHIDAA
Vijana 6 wamekamatwa usiku huu baada ya kuhusika na wizi kwa kumtishia muuza sigara na karanga maeneo ya Ocean Road kuelekea BOT.
Vijana hawa walimtishia huyu muuzaji sigara akiwa na pakiti kumi za sigara na karanga zisizozidi za sh5000!
Baada ya kuoneshwa panga na kisu aliwakabidhi mzigo na kutishiwa kuuawa kama atapiga kelele!
Kijana akajificha sehemu alipoona pikpiki akaomba msaada wakaenda kuwasubiria maeneo ya KFC!
Hapo ndipo kijana akishirikiana na walinzi wengine waliokuwa wakiwasubiri kwa hamu wakapiga ukunga wa wezi!!
Wazee wa CRDB wakamaliza kazi yao huku waungwana wanawarushia mawe vichwani.
Nimeacha wanasubiri defender kuwachukua !!
Samahani dini yangu hairuhusu kupiga picha za wenye damu, ningewawekea!
Muwe makini area hiyo usiku kuanzia saa moja!
Sea View, Ocean Road na Viwanja vya Golf Gymkhanna Club:
Maeneo haya kuna vibaka hatari sana ambao hushambulia kwa kikundi na kupora mali zote na kukuacha ukiwa majeruhi. Maeneo haya yametulia sana na yanaonekana ni salama sana kwani yako jirani na ikulu, lakini hayana usalama wowote na ni hatari kabisa.
Usipite maeneo hayo kwa miguu mida ya kuanzia saa kumi na mbili na nusu giza likiwa linaingi, maana utakumbwa na dhahama.
Ni rahisi sana kuwakamata wezi sehemu kama izo kama itafanyika ambush ya kweli sema kila kitu kimekua siasa ndio shida..
Hii habari sio mara ya kwanza kuisikia ina maana mpk leo Polis hawajachukua hatua tu.
Ukistaajabu ya Musa hapo nyuma ya huo mjengo si ndio tuliambiwa kuna mtaa ambao una kila aina ya sodona au nimekosea njia?
Ni mita ngapi kutoka ikulu ya nchi!?KULE NI JEHANAMU WATAKUUA...
Polisi tusaidieni!