Verify you are not robot!!

Verify you are not robot!!

Farolito

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2018
Posts
14,971
Reaction score
35,038
Wakuu,
Nini malengo ya website mbalimbali kuuliza swali hilo? na wakati mwingine kukupa task mbalimbali kama kuchagua magari, traffic lights nk.
✅Ina maana wanaogopa marobot yataharibu au vipi?
✅Je robot lenyewe kama ni kweli inataka kuingia humo haliwezi kujibu hilo swali kwamba I'm not robot?
Naomba kueleweshwa kitaalamu.
Ahsante

3fca1d6faf8d4efcbe8ba5e446d4efa1.jpg
a7fb9308ac064aaff266898a07445106.jpg
 
Robot si kwa maana ya machine, huko mitandani kuna software nyingi unapoingiza taarifa zako zenyewe inazikusanya kwa siri bila wewe kufahamu na baadae wanazitumia kufanya hacking.

Ndio maana kuna kipengele cha “2fa” pia
 
ili kuhakikisha anayetumia website ni mtu halisi na sio bot

Bots huwa zinatumika kufanya spam, kujaribu ku-hack akaunti, au kujaza fomu mara nyingi sana. Hiyo verification (kama kuchagua picha au kuandika herufi) inasaidia kuzuia mambo hayo na kulinda website pamoja na watumiaji wake.

Mfano ukiingia kwenye darkweb kuna huduma ya email bomber ili kumsaidi carder/loader kufanya KAZI yake vizuri bila muhusika wa account kuona notification

Email bomber(email spammer) unatumia outomated bots scripts kutumia target email kufanya registration kwenye sites mfano discord na zingine kwahiyo ili kuzui bot wanaweka verification captcha

Nb.for educational purposes
 
Asante kwa maelezo, Je ina maana hizo Boys haziwezi kujibu hizo Captcha, au haziwezi kujibu hilo swali?
 
Robot si kwa maana ya machine, huko mitandani kuna software nyingi unapoingiza taarifa zako zenyewe inazikusanya kwa siri bila wewe kufahamu na baadae wanazitumia kufanya hacking.

Ndio maana kuna kipengele cha “2fa” pia
Kwahio robot au software haziwezi kujibu hilo swali?

"2fa" ni nini sijaelewa?
 
Asante kwa maelezo, Je ina maana hizo Boys haziwezi kujibu hizo Captcha, au haziwezi kujibu hilo swali?
Zikijaribu kujibu maswali zinagundukika na website husika Kwa sababu zitajibu haraka Sana na Kwa spidi inayofanana tofauti na binadamu anajibu Kwa kusita na spidi tofauti kutoka image moja Hadi nyingine. Pia ? Pia movement ya cursor anapotumia binadamu inakuwa haijanyoka lakini robot linanyosha kama rula, hapo ndio litagundulika kwamba huyu sio robot.
Pia nasikia muda mwingine robot linajichanganya linajibu maswali ya Siri ambayo binadamu huwezi kuona hapo hapo ndio linadakwa kwamba huyu mtembeleaji WA website sio binadamu.

Nimejaribu ku-sreenshot majibu yangu nione kama nimepatia, AI imeongeza nyama nzito Kwa kusema hivi:

3. "Maswali ya Siri" (Honeypots)
Mdau amegusia kuhusu robot kujibu maswali ambayo binadamu haoni. Hapa anazungumzia kitu kinaitwa Honeypots.
Wataalamu wa website huweka "input fields" (sehemu za kujaza taarifa) ambazo zimefichwa kwa kutumia CSS (zisionekane na macho ya binadamu).
Binadamu hataona chochote, kwa hiyo hatajaza.
Robot linasoma code ya website, hivyo litaona kuna sehemu ya kujaza na litaweka data. Kitendo tu cha kile kijisanduku kilichofichwa kujaa, mfumo unajua hapa "mgeni" si binadamu
 
Back
Top Bottom