http://changamoto.co.tz/index.php?o...nbyZvcHRpb249Y29tX2NvbnRlbnQmSXRlbWlkPTE1NA==Tuesday, 10 February 2009 http://changamoto.co.tz/index.php?v...t&print=1&page=&option=com_content&Itemid=154 http://changamoto.co.tz/index.php?v...ango&format=pdf&option=com_content&Itemid=154
VATICAN City State au kwa kifupi Vatican ni nchi yalipo makao makuu ya Kanisa Katoliki duniani. Kesho inatimiza miaka 80 ya uhuru iliyoupata kutoka Italy.
Makala hii inatumia fursa hii kufafanua kilichozoeleka kuitwa Ubalozi wa Vatican. Mwisho tutaona kuwa kumbe hawa si mabalozi wa Vatican. Je ni mabalozi wa nini? Nakushauri msomaji tuwe pamoja hadi mwisho.
Si ajabu kukutana na swali kuwa ni nini maslahi ya Ubalozi wa Vatican hapa nchini wakati ni nchi ya kidini yaani Kanisa Katoliki.
Je, ni kweli Wakatoliki hatuulizi swali hili? Kwamba muuliza swali akificha jina basi tusidhani kwamba ni mkatoliki?
Hapana. Balozi wa Vatican nchini Australia, Askofu Mkuu Charles Daniel Balvo anasimulia kwenye Sheria za Kanisa zinazohusu wawakilishi wa Papa ndani ya kitabu kiitwacho New Commentary on the Code of Canon Law kilichotolewa mwaka 2003 kwa ushirikiano wa Beal, Corriden na Green.
Ameeleza kwamba wakati wa Mtaguso (Vatican II) maaskofu walitaka ufafanuzi zaidi kuhusu kazi za mabalozi hawa baadhi wakipendekeza kuwa mpango wa kuendelea kuwa na mabalozi hauendi na wakati, hivyo ufutwe {Ukurasa. 491, aya ya sita}.
Mtaguso ni mkutano wa maaskofu wote duniani. Hapa nchini, Placidus Gervasius Nkalanga, Askofu Mstaafu wa Bukoba ndiye aliye hai aliyekuwa tayari ni askofu wakati wa Mtaguso. Kipindi hicho alikuwa ni Askofu Msaidizi wa Bukoba wakati Jimbo hilo likiongozwa na Laurian Kadinali Rugambwa.
Kanisa Katoliki ni dhehebu pekee ambalo makao yake makuu ni nchi (Sovereign territory). Kiongozi wa Kanisa (Papa) ndiye Mkuu wa nchi hiyo. Tujikumbushe nchi hiyo ilivyozaliwa.
Kanisa halikumiliki mali wala ardhi, hadi ilipofika mwaka 321BK umiliki uliruhusiwa. Wapo waliotoa majengo na ardhi kuwa mali ya Kanisa. Mnamo karne ya 16 Papa alipewa hata maeneo ambayo ni nchi azitawale. Nchi hizo zilizoitwa Papal States zilienea katikati ya Italy na mbili ndani ya Ufaransa yaani Venaissin na Avignon.
Dunia ilibadilika, Marekani ikajitawala (1776) na mapinduzi Ufaransa yalifuata miaka 15 baadaye. Mapinduzi hayo yaliteka zile Papal State mbili kuzifanya zisiwe tena miliki ya Papa.
Baada ya Ufaransa, huko Italy lilianza vuguvugu la kuunganisha tawala za Italy kuwa tawala moja. Papal States zilitekwa na hadi mwaka 1860 zilishamezwa na Italy mpya kasoro eneo la Roma alimoishi Papa.
Mwaka 1861 Italy mpya iliitangaza Roma kuwa Mji Mkuu na kuuteka Septemba 20, 1870. Hii ndiyo siku iliyofuta Papal States zilizodumu kwa karne kadhaa na mwaka uliofuata, Italy ilimtaka Papa kuwa chini ya mamlaka yake, japo haikumzuia kuteua mabalozi wanaomuwakilisha duniani.
Ilishindikana Papa kuwa chini ya Italy ikabidi abaki ndani ya eneo la Vatican yeye na waliomrithi wakijulikana kama mfungwa ndani ya Vatican. Hali ilibaki hivyo kwa miaka 60.
Hatimaye Februari 11, 1929 makubaliano yalifikiwa kwa jina la Mkataba wa Lateran. Eneo la Vatican likageuzwa kuwa nchi inayojitegemea (sovereign territory) chini ya Kanisa Katoliki.
Vatican ni nchi ndogo iliyozungukwa na jiji la Roma. Mpaka wa Tanzania unazidi kilomita 4,247 wakati unaoizunguka Vatican haufiki kilomita nne. Jijini Mwanza safari ya kutoka Benki Kuu hadi Mkuyuni inazidi ya kuizunguka Vatican.
Dar es Salaam kwenye barabara ya Morogoro, safari ya Fire au Zimamoto hadi daraja la Manzese pia ni zaidi ya kuizunguka Vatican.
Si rahisi kuuelewa ubalozi kwa sababu tu kuna nchi ya Vatican. Ni lazima kujua taasisi iitwacho Holy See.
Sheria ya Kanisa inaifafanua Holy See kwamba Holy See ni Papa na idara zote za Roman Curia katika kuendesha Kanisa zima duniani (Can. 361).
Tayari tuna ufafanuzi kuhusu Vatican kama nchi na Holy See kama kikundi cha viongozi. Inawezekana kufafanua ubalozi katika hatua hii. Lakini pia tujadili hali inayoitwa Sovereignty. Sina hakika UHURU ndiyo tafsiri fasaha kwa neno hili.
Nadharia za Sovereignty zinakubaliana kwamba ni hali ya kuwa na mamlaka ya mwisho kuendesha serikali, nchi au watu. Mihimili kama serikali (executive), bunge(legislative) na mahakama (judiciary) hugawana uhuru huu wa ndani (Internal sovereignty). Majimbo ya Marekani yana uhuru huu wa ndani ambapo si lazima yafanane uendeshaji.
Uhuru wa kimataifa (External sovereignty) ni hali ya kutambulika na mataifa mengine pia kukidhi vigezo vya sheria za kimataifa (International laws).
Uhuru huu (Sovereignty) unaviweka wapi vyombo viwili, nchi ya Vatican na kingine kikiwa Holy See?
Vatican ina ardhi kama Tanzania japo ni ndogo. Tanzania ina haki ya kuweka mabalozi nchi za nje. Haki hii inaenda kwa Vatican City pia. Ni wazi ubalozi wao yabidi uitwe Ubalozi wa Vatican (Vatican Embassy) na si vinginevyo.
Jambo la msingi kutambua ni kwamba, Holy See ndiyo inayosimamia mahusiano ya kidiplomasia kwa mujibu wa sheria za kimataifa, pia kupokea na kutuma mabalozi na wala si Vatican City State. Hivyo kuanzia sasa halitatumika tena neno Ubalozi wa Vatican badala yake neno Holy See litatawala makala hii.
Ni haki kudadisi kwa nini Vatican isitoe mabalozi, jukumu hilo lifanywe na Holy See. Turejee neno Sovereignty tukiiangalia Holy See, uongozi wa Kanisa tangu kale. Papa au Holy See wameteua wawakilishi tangu karne ya nne.
Holy See imetambulika bila kuingiliwa kabla ya karne ya 16. Tumeona ilivyopata nchi zake, yaani Papal States. Ilipokuzwa dhana ya uhuru (Sovereign State), Holy See iliendelea kutambulika tayari ikiwa na Papal States. Ferdinando Cardinal d'Adda amekuwa balozi wa Papa (Holy See) nchini Uingereza Machi 03, 1687.
Kuepusha magomvi, mwaka 1815, Ulaya walikubaliana kuipitia upya ramani ya bara hilo katika mkutano wa Vienna (Congress of Vienna-1815). Kifungu (article) cha nne cha maamuzi kilimpa Nuncio au mwakilishi wa Papa (Holy See) hadhi kubwa ya kidiplomasia (dean) katika nchi anayopelekwa.
Papal States zilipofutwa na Italy (1870-1928), mapapa hawakuwa tena na nchi. Wala Vatican walimoishi haikuwa nchi. Kipindi chote hicho (miaka 60), Holy See imeendelea kutambuliwa uhuru wake (Sovereignty) na kupokelewa mabalozi wake walioteuliwa na Papa.
Pia mwaka 1961 Umoja wa Mataifa ulitoa makubaliano mapya ya kidiplomasia (Vienna Convention on Diplomatic Relations of 1961). Wawakilishi wa Papa wametajwa kwenye vifungu 14(1)(a) na 16(3). Balozi za Holy See huitwa Apostolic Nunciature of the Holy See.
Kuzaliwa kwa Vatican kuliiongezea Holy See chombo kingine huru (Sovereign) kwa vigezo vya kimataifa. Holy See ina umri wa karne nyingi. Vatican ndiyo kwanza inafikisha miaka 80. Hivyo, Holy See ni mzoefu mzuri duniani kwa masuala ya ubalozi kama si mmoja wa waanzilishi. Uhusiano wake (Nunciature) nchini Iraq ulianza Disemba 17, 1832 na Askofu Mkuu Henri-Marie Amanton akiwa mwanzilishi katika hadhi ya Apostolic Delegate. Holy See duniani ina ubalozi kwenye nchi 173, baadhi ni Iran, Yemen, Sudan, Morocco, Brazil n.k.
Holy See ina mahusiano maalum kwa Palestina na Russia. Pia ina mahusiano ya kibalozi na taasisi isiyo na nchi, lakini inatambulika huru iitwayo Sovereign Military Order of Malta (SMOM).
Vatican na Holy See ni vitu viwili tofauti vilivyo huru. Holy See imeteua mabalozi karne nyingi na imeendelea hivyo hata baada ya kuzaliwa Vatican City State.
Kwa uhuru (Sovereignty) uliopo Holy See na Vatican City State kila moja zaweza kutoa pasi za kusafiri (passport). Udogo wa Vatican na shughuli za Holy See havileti mazingira ya utoaji pasi mara kwa mara. Inapotokea, Holy See hutoa pasi maalum (Diplomatic passport).
Vatican City kama nchi yaweza kutoa pasi za kawaida (normal passports) japo yaelekea hilo limekabidhiwa kwa Holy See pia. Mahujaji kwenda Vatican hupata viza ya Italy kwenye ubalozi wa Italy.
Vatican City haijatangaza utaratibu wa kuteua mabalozi wakati utaratibu wa Holy See umo kwenye sheria za Kanisa, mabalozi wakiwa aina ya wawakilishi wa Papa au Papal Legates (Can. 363-367).
Hivyo ni vigumu kuhoji kwa nini nchi iwe na ubalozi wa Holy See. Yapo mawazo yanayofananisha kwa kuuliza Mbona tuna ubalozi wa Vatican ambayo ni nchi ya kidini?
Jibu la kwanza ni kwamba, hakuna ubalozi wa Vatican ila kuna ubalozi wa Holy See. Jibu la pili linahitaji msaada wetu tulio wakatoliki. Hata Vatican na Holy See zisitambuliwe kimataifa, bado mwakilishi huyu (Nuncio) anahitajika penye wakatoliki (Can. 362).
Nafasi yake kwa wakatoliki haitaathirika na kutotambuliwa huko. Masuala yetu atayafikisha kwa Papa kama kawaida. Itakayopotea ni hadhi yake ya kiubalozi tu.
Yeye ni sehemu ya utaratibu wa Kanisa. Nchi kuikubali hali yake ya kibalozi si suala la wakatoliki wala watanzania. Ni suala la Umoja wa Mataifa chini ya mkataba wa Vienna wa mwaka 1961.
Hivyo, swali hili halina tija kuwauliza wakatoliki au viongozi wa nchi ya Tanzania. Swali hili mahala pake ni Umoja wa Mataifa unaoweza kulijadili kwa uthabiti wa hoja itakavyojengwa.
Kila la heri Vatican City State kufikisha miaka themanini.
Source: ChangaMoto