VAT juu ya ununuzi wa umeme wa TANESCO

warea

JF-Expert Member
Jan 22, 2010
244
65
Naomba kuelimishwa juu ya mahesabu ya kukokotoa VAT kwenye mauzo yenu ya umeme wa TANESCO.

Nimeona kuwa TANESCO wanakosea kukokotoa VAT kwenye kiasi anacholipa mteja.
Badala ya kukokotoa VAT kutokana gharama ya umeme alionunua mteja, TANESCO wanakata kwanza VAT halafu inayobaki ndio wanaigawia kwenye bei ya umeme, halafu wanakupa umeme.

Mfano. Ukilipa 100,000. Wanakata kwanza VAT 18,000 halafu wanakupa umeme wa hela inayobaki yaani 82,000. Kama bei ya umeme ni 297.98 utapata unit 275.19.

Kiuhalisia walitakiwa ununue kiasi fulani cha umeme, wakokotoe jumla ya gharama ya huo umeme, halafu wakudai VAT kulinganga na umeme ulionunua.
Mfano Kwa 100,000, ungeweza kununua unit 284.4 kwa gharama ya 84,745.76 kwa bei ya 297.98, VAT ingekuwa 15,254.24.

Kwa mtindo huu wa kukata VAT kwanza mteja analipa VAT kubwa zaidi na kununua umeme pungufu.

Ni kweli TANESCO wameshindwa kuweka kanuni ya kukokotoa VAT?

Naomba kusahihishwa kama nimekosea.
 
Hawa nao ni Wezi tu!Nimeshangaa nimekatwa na hela ya REA 3%·Anyway,Watanzania wazuri sana wakuibiwa!
 
Naomba kuelimishwa juu ya mahesabu ya kukokotoa VAT kwenye mauzo yenu ya umeme wa TANESCO.

Nimeona kuwa TANESCO wanakosea kukokotoa VAT kwenye kiasi anacholipa mteja.
Badala ya kukokotoa VAT kutokana gharama ya umeme alionunua mteja, TANESCO wanakata kwanza VAT halafu inayobaki ndio wanaigawia kwenye bei ya umeme, halafu wanakupa umeme.

Mfano. Ukilipa 100,000. Wanakata kwanza VAT 18,000 halafu wanakupa umeme wa hela inayobaki yaani 82,000. Kama bei ya umeme ni 297.98 utapata unit 275.19.

Kiuhalisia walitakiwa ununue kiasi fulani cha umeme, wakokotoe jumla ya gharama ya huo umeme, halafu wakudai VAT kulinganga na umeme ulionunua.
Mfano Kwa 100,000, ungeweza kununua unit 284.4 kwa gharama ya 84,745.76 kwa bei ya 297.98, VAT ingekuwa 15,254.24.

Kwa mtindo huu wa kukata VAT kwanza mteja analipa VAT kubwa zaidi na kununua umeme pungufu.

Ni kweli TANESCO wameshindwa kuweka kanuni ya kukokotoa VAT?

Naomba kusahihishwa kama nimekosea.

Ebu weka hiyo receipt hapa tuone.
 
naomba kuelimishwa juu ya mahesabu ya kukokotoa vat kwenye mauzo yenu ya umeme wa tanesco.

Nimeona kuwa tanesco wanakosea kukokotoa vat kwenye kiasi anacholipa mteja.
Badala ya kukokotoa vat kutokana gharama ya umeme alionunua mteja, tanesco wanakata kwanza vat halafu inayobaki ndio wanaigawia kwenye bei ya umeme, halafu wanakupa umeme.

Mfano. Ukilipa 100,000. Wanakata kwanza vat 18,000 halafu wanakupa umeme wa hela inayobaki yaani 82,000. Kama bei ya umeme ni 297.98 utapata unit 275.19.

Kiuhalisia walitakiwa ununue kiasi fulani cha umeme, wakokotoe jumla ya gharama ya huo umeme, halafu wakudai vat kulinganga na umeme ulionunua.
Mfano kwa 100,000, ungeweza kununua unit 284.4 kwa gharama ya 84,745.76 kwa bei ya 297.98, vat ingekuwa 15,254.24.

Kwa mtindo huu wa kukata vat kwanza mteja analipa vat kubwa zaidi na kununua umeme pungufu.

Ni kweli tanesco wameshindwa kuweka kanuni ya kukokotoa vat?

Naomba kusahihishwa kama nimekosea.
mkubwa uko sawa..............lakini mbona fomula ni rahisi sana,yaani ingekuwa hivi:
X+0.18x=amount paid(kiasi kilicholipwa)
x inasimaa badala ya kiasi halisi kinachotumika kununua umeme,kwa hiyo o.18x ndiyo vat,kwani vat ni asilimia 18.kama ni kweli wanafanya hivyo(kwani sina document inayothibitisha)basi kwa kila laki moja unayotumia kununua umeme,unaibiwa jumla ya tsh 2,745.76...ni mimi na wewe ndio tunapaswa kulifuatilia hilo,na kama ni kweli tunapaswa kulalamika kupitia ewura.big up mkubwa kwa ugunduzi wako.
 
Back
Top Bottom