NAMBA MOJA AJAYE NCHINI
JF-Expert Member
- Oct 29, 2019
- 8,535
- 17,479
Chama na serikali vikajitahidi sana kufikisha umeme vijijini Ili wananchi wapate huduma hii, na wananchi wakafanya mchakato wa gharama kubwa Ili wapate umeme na kweli wakaupata.
Baada ya kulipia LUKU na kuanzia kupata huduma hii mchezo wa kipumpavu ukaanza hasa na fundi mkuu wa TANESCO akishirikiana na mafundi uchwara ambao Wanakata umeme kama mtoto anazima kibatari na kukiwasha!
Ipo hivi
Wanaweza amua tangu asubuhi hadi jioni umeme ukawepo halafu ikifika muda wa mechi ya Simba au Yanga yaani sekunde chache kabla ya gem kuanza Wanakata umeme ikifika halftime Wana washa Tena halafu mechi ikianza Tena second half Wanakata tena,ni kama kwamba ni maksudi kabisa Ili kuwa KERA wananchi!
Wamejaribu kuwasiliana na viongozi wa chama na serikali katani hapo lakini hakuna Cha maana hata leo wamecheza kamchezo kao,
Nilipouliza kwa kina ni kwanini wanafanya hivyo, Baadhi ya wadau wakasema hao mafundi uchwara wawili wakiongozwa na fundi mkuu katani hapo wanapewa rushwa na wauza Solar na mafuta ya petrol Ili wahusika biashara zao zisidode!!
Chama na serikali vinahujumiwa kumbuka TANESCO lazima warudishe walau gharama za uendeshaji Ili huduma hii iendelee!
Nakumbuka hata ule umeme wa Solar wa aliekua mbunge wa Igalula ulikufa kwa style ya hujuma hadi leo vimebaki chuma chakavu na nguzo zinazooza bila kufanya kazi ya mwanzo na ule umeme ulikufa zipo solar tu pale ambazo ni chuma chakavu!!!
Cha kushangaza Diwani yupo huyo ndio mzembe kweli kweli anachojua ni kuuza duka la dawa, Hashughuliki na changamoto za wananchi, katibu wa chama katani hapo nae Hana sauti Wala viongozi wa chama!!
Zimenifikia nimezituma, wenye mamlaka chukueni hatua!
Mungu ibariki Tanzania, nchi yetu tuipendayo sana!