Valentine day yangu imeharibika wana jamii naomba msaada wenu

Valentine day yangu imeharibika wana jamii naomba msaada wenu

Mimi ni Kijana wa kiume nina mahusiano na my Girlfriend for almost two years na tulikubaliana mwezi huu tukatambulishane kwa wazazi,na Mungu akipenda tufunge Ndoa Mwaka Huu kwa kweli tulikuwa tunapendana sana.
Lakini bahati mbaya mwezi mmoja uliopita nilikuwa naangalia sms kwenye simu yake na nikaja gundua kwamba kuna siku aliniambia usiku hatapatikana kwenye simu because ya Charge kwani anasema umeme siku hiyo ulikuwa haupo,,Lakini kwenye sms nikagundua alikuwa hajalala nyumbani usiku huo alilala nje na jamaa mwingine, mbaya zaidi nilivyokutana nae akaanza ku-delete sms za huyo jamaa.kwa hiyo nikagundua kwa sasa hivi anani cheat.
Nilikaa kimya kwa mwezi mzima sijmuambia kitu na uhusiano wetu ukaendelea kama kawaida ili nijue ukweli.

PILI kila tukiwa naye huwa ananisave kwenye phone yake kama My husband lakini nikaja gundua pindi tuanapoachana ananibadilisha jina.

TATU amekuwa akinidanganya sana mfano ananiambia yupo nyumbani lakini nikifuatalia nagundua kwamba hayupo nyumbani.

NNE kila nikimtumia sms hata iwe ya msingi kiasi gani haijibu mpaka nimpigie halafu nikimuuliza ananiambia hajaiona lakini nikafuatilia nikagundua kwamba at same time anaweza mtu mwingine akamtumia akamjibu at spot.

So nikaamua kumuambia ukweli kwamba kama kweli ananipenda and kweli yuko willing kuwa na mimi aniambie ukweli wa mambo hayo lakini akaanza kuwa mkali kwamba anataka nijue nani kaniambia kuwa yeye ni malaya wa kulala na wanaume hovyo,,tulikuwa tunafanya maongezi kwa njia ya simu kwa sababu alikataa tukutane kwa maongezi kwa kisingizio kwamba yupo busy lakini nilivyofuatilia nikagundua kwamba anaweza kukutana na watu wengine kwa starehe lakini hataki kukutana na mimi kwa mambo ya msingi.

Alivyoanza kuwa mkali akakata simu,kila nikimpigia ili tuongeee ikiwezekana tuyamalize hataki kupokea simu.

Nisaidiane wana jamii nifanyeje? na Valentine yenyewe imeharibika.

Unajua vitu vingine siyo ushauriwe, unaona kwa macho yako. Huyo hakupendi, hana muda na wewe, hana hata mshipa wa penzi kwako. Kula kona kama unaelewa ninachosema. Hiyo valentine unaweza kutana nayo popote.

Ubarikiwe.
 
Jamani sasa hapa unataka kusaidiwa nini nawakati hiyo picha yenyewe tuu ni msaada tosha!!

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
She is not faithful to you, yet she needs your hand in marriage
 
Mbona watu mnapelekeshwa na hayo masaa 24 kama siku moja ambayo naona ya kawaida tu? Mnajipa stress tu kuiga tamaduni za wazungu.

61690_211682135641721_1448144511_n.jpg
 
She is not meant for you, leave her alone as soon as possible.
Ukijifanya unajua kupenda zaidi atakuharibu na utadata mbaya. Hakupendi ila kuna vitu vyako huenda mkwanja ndoo unamfanya awe na wewe. Ukiondoka anakusave guruwe au kenge?
 
Na ukilazimisha mpaka ukaoa, utajuta maishani mwako. Take it from me.
 
stress ni ugonjwa wakujitakia.. unaweza kuepukana nao!
 
  • Thanks
Reactions: msd
Dah, huyo kishachukuliwa. Cha kufanya kaa kimya na usianzishe mawasiliano. Ndani ya wiki ukiona hakujibu, basi futa mawazo yake tafuta mwenzi mwingine.
Ahsante Ndo maamuzi yangu niliyofikia kwa sasa,nione kitatokea nini ndani ya week ya kutokuwa na mawasiliano
 
God sometimes removes a person from your life for your protection. Don't run after them..........All discarded lovers should be given a second chance, but with somebody else.......huna haja kujifanya ruba temana naye mapema
 
She is not meant for you, leave her alone as soon as possible.
Ukijifanya unajua kupenda zaidi atakuharibu na utadata mbaya. Hakupendi ila kuna vitu vyako huenda mkwanja ndoo unamfanya awe na wewe. Ukiondoka anakusave guruwe au kenge?
Ukweli tulikuwa na upendo wa dhati lakini kabadilika kwa muda mfupi sana
 
Hapo umeingia choo cha kike...........Hamna muke wala mupenzi...Valentine mbona bado nzuri nenda katembelee kituo cha watoto yatima kwani hawana wa kuwapenda na kile kiasi ulichoandaa cha kuspend kiasi toa ili mungu akuletee mke bora.
 
Switch a red light in your head she is not of the marriage type she is of playing type.
 
Neno zuri ninalokupa ndugu ni ACHANA NAYE,inaonyesha umeumia sana lakini ndio mambo ya ku-fall kichwa kichwa(yaani kama ni
nyoka kwenye shimo wewe umeingia mwili mzima)katika penzi,inaumiza sana najua hiyo kitu,siku nyingine if it happens you fall to another one sijiachie full,acha akiba kidogo,just incase akikutenda maumivu yake yanakuwa sio kivile.Kitu kingine usipende kulazimisha mapenzi ukigundua kuna sign za mtu kuku-cheat,achana naye immedeately,watu wanakunywa sumu kwa kuyaendekeza haya mambo maana aslimia karibu 70 ya mapenzi huwa ni kudanganyana,ukweli ni kidogo sana.Jaribu kutofautisha kati ya kupendana na kutamaniana utagundua penzi lako liko kundi gani.
 
Chapa lapa, hakuna mapenzi hapo
 
Hafai kuwa hata mpenzi wako... atafaa kuwa mke kweli?
NB: Ndoa ndiyo maisha yako ukibugi tu, utajuta maisha yako yote.
 
huwezi jua mungu kakuepusha na nini .tena mshukuru sna kaonyesha true color at the begining.huyo ungeweka nda lazima uwe na drip karibu na kitanda au kitanzi chakujinyongea ndugu yangu,move on its not toooo late to start afreash move on mkuu.
 
Back
Top Bottom