Uzuri wa mwanamke upo wapi? Ni upi?

Uzuri wa mwanamke upo wapi? Ni upi?

mi huwa nahic kama naibiwa vile coz mtu aliyekamilika hawezi kuhangaika hivyo huwa nahisi kuna ubovu fulani unafichwa
 
uzuri wa mwanamke kwanza ni sura mutu yoyote mwanamme yoyote asije danganya kuwa kavutiwa na tabia, si kweli cha kwanza kuvutia mwanamke kwa mwanaume ni sura bila sura kukuvutia huwezi hat kutaka kujua tabia zake nadhani tupo pamoja
 
Wanawake ni maua jamani
Tunafanya vile tunapenda ...isiwape tabu sana
 
baadhi wanajiremba kupita kiasi unamkuta dada domo jekundu km kalamba damu halafu mwingine utamuona hereni kwenye pua km jini .........wanachukiza sana.
 
Mungu akuumba kama ilivyo unahangaika nn mm naona kama wanawake wenye tabia kama hizo wamepungiwa akili
 
 
Last edited by a moderator:
heheheheheh aluuu!
One man's meat is another man's fish..sorry poison.
Mtoa mada, we komaa na kuku wa kienyeji tu maana ndio saizi yako.Hao wengine huwawezi.

Baada ya utangulizi ngoja sasa tuwekane sawa:

1. Urembo kwa mwanamke inategemea naye anaelewa nini kuhusu urembo.Wengine hawana aah wala beeh kuhusu urembo na ndio maana hujikandika vipodozi na kukaa na minywele miezi bila kuosha! Nywele za bandia za kushonea za quality nzuri zenye kuoesheka mara kwa mara kama nywele asili ni bei mbaya.Kuna wenye kupenda urembo lakini mambo ya fedha yanagomba.

2. Urembo unaendana na mtu na kwa kipimo, kutegemeana na mtu mahali alipo, au anapokwenda,kazi afanyayo nk.Kazi kwenu kina baba/kaka kuwapa wake/marafiki wenu wa kike support kifedha na ushauri ili waendane na mnavyotaka au kutamani.Huwezi kulalamika tu bila kutafuta suluhu.

3.Wanaume kwa kiasi kikubwa mnawasukuma wanawake kwenda mbali na hata kufanya mambo yenye kuwaletea madhara ili mradi tu mfurahie. Hebu acheni kukimbizia wanawake warembo muone kama wanawake watahangaika hivyo.Mwanaume mwenye mwanamke "natural" hufurahia kupunguza matumizi nyumbani lakini huhangaika sana kuipendezesha nyumba ndogo, Mwisho wa siku mwanamke asilia nyumbani hulaumiwa kwa kujiachia! Mnadhani wanawake wanafurahia kuketi masaa 6 kusukwa au kufanyiwa waxing na mambo mengine yenye kuleta maumivu ya kutisha? ACHENI HIZO WANAUME!

kitu NATURAL ina raha yake na mara nyingi katika mapenzi inatakiwa umpende mtu (mwanamk/mwanaume) jinsi alivyo sivyo alivojipamba kwa kuwa wadada wengine ukimkuta amejipamba na ukmbahatisha siku amesahau mawigi yake huwezi kumtambua...kwa ujmla mapambo yanatakiwa yasipoteze muonekano wako halisi vinginevyo utakuwa mtumwa wa urembo ili usionekane umebadilika,na uchaguzi wa mapambo ni muhimu unamkuta mdada real black na wigi kubwa kama la Masanja hadi anapoteza mvuto badala ya kuungeza.
 
Always we jokes but all ladies are according to the status so they differ colour,behavour,even treatment to their homes or houses!
 
 
Last edited by a moderator:
...Beautiful Meagan Good

 
Last edited by a moderator:
UKIMCHUNGUZA BATA SIKU ZOTE HUTAMLA
Inavyoonesha we kaka kazi yako ni kujaribu tu wanawake mara huyu mara yule na wala hujui nini unachotaka kwa mwanamke. wewe usiangalie huyu vp wala yule kama unataka mwanamke tafuta wa preference yako hao wakujiremba waachie wenzio wanaotaka marembo kha!
 
mi huwa nahic kama naibiwa vile coz mtu aliyekamilika hawezi kuhangaika hivyo huwa nahisi kuna ubovu fulani unafichwa

hakuna aliyekamilika na ndio maana tunafanya tuwezavyo turidhishe nafsi zetu. Sasa kama mtu ana kinywele kimoja kichwani, akitupia kiwigi chake na akapendeza kuna ubaya gani.
Mtoa mada, uzuri wa mwanamke ni confidence aliyonayo na hayo tunayofanya yanatuongezea confidence.
 
mimi napenda sana urembo, lakini urembo wangu ni wa vitu asili, kama kucha huwa nafuga za kwangu najitahidi kusafisha sa na zinang'aa na zinapendeza, napenda sana nywele zangu japo mara chache nasuka rasta.
 
........................... Sijui ni ugonjwa au ni jambo ambalo hata wanaume wenzangu huwa linawakumba?

kwa kweli huo ni ugonjwa kamuone neurologist haraka iwezekanavyo pole kaka. nasema ugonjwa kwa sababu kwa kawaida kujipamba koote kwa usoni hakuhusishi kujipamba kinenani huko kunabaki kama kulivyo
 
mada kali kweli! kweli! nimeyasoma mengi na nimejifunza mengi kupitia mada hii.
 
Sawa kujiremba nisawa lakini kunawanawake wengine wanazidisha urembowao, ila kiukweli mimi binafis kunaulembo ninao uchukia ka kuongeza makalio, matiti nakujibadilisha rangi, kiukweli mimi nawachukia watu wanao fanya hivyo. hapa nilipofikia sijawai hona mzungu anayejiremba, ila hayomambo tumeletewa sisi watanzania tusiofikilia mbele.:flypig:
 
Back
Top Bottom