Uzuri na Ubaya wa maisha ya mkoani Iringa

Uzuri na Ubaya wa maisha ya mkoani Iringa

Kamgomoli

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2018
Posts
1,926
Reaction score
4,110
Nimebahatika kuishi mikoa ya Tabora, Katavi, Mbeya, Morogoro, Ruvuma na Dodoma. Na sasa naishi Iringa tangu 2012. Je nini uzuri na ubaya wa mkoa wa Iringa hasa Mjini?

1. Iringa Manispaa si kubwa sana. Ni mji mdogo unaokua na umetulia sn. Hakuna vurugu na mishe mishe nyingi za kibiashara kama Mbeya na Morogoro.Umejengwa vizuri na kwa mpangilio ukilinganisha na baadhi ya mikoa kama Mbeya.

2. Kabila kuu hapa ni Wahehe. Ni watu poa na wasiopenda kudharauliwa na majivuno. Hawana mila potofu kama ilivyo kwa baadhi ya mikoa. Starehe yao kubwa ni pombe ya Ulanzi inayopatikana sana mwezi wa February.

3. Hakuna msongamano mkubwa wa bajaji hivyo hakuna kero za bajaji kama Mwanjelwa.

4. Ni mji msafi. Ni nadra kuona uchafu umezagaa hasa katikati ya mji na hakuna matope mvua ikinyesha. Maji hupotea mara moja mvua inapoisha.

5. Kuna vyuo na taasisi nyingi za elimu ambazo ziko karibu karibu.

6. Kiasi cha uhalifu ni kidogo sana. Kwa ujumla Iringa hakuna mateja au wahuni kama wale wa Arusha. Vijana wengi wa Iringa wamejikita kwenye kazi rasmi na zisizo rasmi.

7. Hali ya barabara inaridhisha kwa kiasi fulani. Barabara muhimu nyingi zina rami. Na zile ambazo hazina rami zinarekebishwa kila wakati hivyo kupitika vizuri.

8. Gharama za maisha ni za kawaida. Bei ya kupanga wastani ni elfu 20,25 mpaka 30 kutegemea na ubora na mahali.

9. Bei ya misosi. Kwa mama ntilie msosi unaanzia 1500 hadi 3000 kutegemea na aina ya mboga. Maharage,Nyama au samaki. Chips nyama 2000-3000

10. Hali ya hewa. Hali hewa ya Iringa Mjini hasa ni vipindi 2. Kipindi cha baridi na joto. Msimu baridi jotoridi huwa nyuzi 12C mpaka 24C. Msimu wa joto huwa 18C hadi 28. Ni nadra sana joto kupanda hadi 30C na msimu wa joto ndio msimu wa mvua.

11. Hali mvua. Pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa bado mkoa wa Iringa unapata mvua za kutosha na hivyo kuna uhakika wa kufanya kilimo maeneo ya vijijini. Mazao yanayolimwa ni Mahindi, Maharage, Mpunga, Viazi vitamu, Viazi mviringo, bila kusahau zao la miti linalolimwa wilaya za Kilolo na Mafinga.

12. Biashara. Kibiashara Iringa si mji wa mishe mishe nyingi. Bado idadi ya watu ni ndogo. Maduka mengi ya bidhaa ni madogo madogo na makubwa kiasi tofauti na miji kama Dodoma, Morogoro na Mbeya.

13. Utalii. Uwepo wa hifadhi ya Ruaha na Makumbusho ya Mkwawa unafanya kuwe na fursa mbalimbali za kitalii. Mfano makampuni ya Safari tours yanayosafirisha watalii.

Kwa ujumla Iringa inaendelea sana tena si kwa kubanana kama mikoa mingine. Huduma nyingi za kijamii zinazambaa kwenda nje ya mji. Mfano uwepo wa Stendi mpya nje ya mji eneo la Igumbilo umepunguza msongamano wa magari katikati ya mji kwa kiasi kikubwa

Mwisho. Iringa ni moja ya sehemu nzuri sana kuishi kwa mtu anayependa utulivu , ila kwa wazee wa mishe mishe inaweza isiwe sehemu sahihi.

Karibu Iringa
 
Nyongeza

*Starehe kubwa ya vijana mbali na pombe ya ulanzi ni ngono.

*Ni mkoa unaoongoza kwa ngono zembe,hususani kwenye camps zinazojengwa porini wakati wa uvunaji wa mazao ya misitu.

*Kuna vyakula vingi vya aina tofauti na vipatilanavyo kwa gharama nafuu.
 
Na pia ni mkoa pekee ambao unaweza kuelekea mashariki ukaja kutokea Magharibi.....Sema Baadhi ya vitu vina boa..Mfano Vyumba Baadhi ya maeneo kama M/togwa ni gharama Sana afu nyumba za kiboya....Pia Pamba(nguo) Iringa ni gharama Sana ndomana mabishoo wengi wa Iringa wamekondeana,sababu ya kujinyima Kula ili wapendeze
 
Naunga mkonyo hoja,kingine ni uchache wa huduma za kifedha,yaani ukiwa mufindi na unatumia tigopesa jiandae kuifuata mafinga...Mpesa moja inaweza kuhudumia vijiji hata viwili na mwenye hiyo huduma anaheshimika kwelikweli!
Na pia ni mkoa pekee ambao unaweza kuelekea mashariki ukaja kutokea Magharibi.....Sema Baadhi ya vitu vina boa..Mfano Vyumba Baadhi ya maeneo kama M/togwa ni gharama Sana afu nyumba za kiboya....Pia Pamba(nguo) Iringa ni gharama Sana ndomana mabishoo wengi Iringa wamekondeana,sababu ya kujinyima Kula ili wapendeze
 
Mwembetogwa bei juu kwa sababu ya wanafunzi wa vyuo. Hiyo hali ni sehemu zote hata Mazimbu Moro.
Na pia ni mkoa pekee ambao unaweza kuelekea mashariki ukaja kutokea Magharibi.....Sema Baadhi ya vitu vina boa..Mfano Vyumba Baadhi ya maeneo kama M/togwa ni gharama Sana afu nyumba za kiboya....Pia Pamba(nguo) Iringa ni gharama Sana ndomana mabishoo wengi wa Iringa wamekondeana,sababu ya kujinyima Kula ili wapendeze
 
Naunga mkonyo hoja,kingine ni uchache wa huduma za kifedha,yaani ukiwa mufindi na unatumia tigopesa jiandae kuifuata mafinga...Mpesa moja inaweza kuhudumia vijiji hata viwili na mwenye hiyo huduma anaheshimika kwelikweli!
Kweli mkuu Miamala ya kifedha Baadhi ya maeneo Iringa ni tatizo na Mawakala ni wachache Sana ....hasa Maeneo ya Mufindi, Baadhi ya maeneo ya Kilolo na Maeneo yote kutokea Isele mpaka Ruaha mbuyuni....Sehemu nyingine hakuna Mawakala kabisa
 
Ni shida mkuu labda watumiaji ni wachache,wengi wanalima nakujipatia vyakula wanahifadhi ndani maisha yanasonga hawana matumizi mengi ya fedha kabisa zaidi ya nyama choma,ulanzi na ugimbi na mafuta ya pikpiki

Basi kama ndio Iringa bado sana
 
Nyongeza

*Starehe kubwa ya vijana mbali na pombe ya ulanzi ni ngono.

*Ni mkoa unaoongoza kwa ngono zembe,hususani kwenye camps zinazojengwa porini wakati wa uvunaji wa mazao ya misitu.

*Kuna vyakula vingi vya aina tofauti na vipatilanavyo kwa gharama nafuu.
Ungekuwa unaongozakwa ngono zembe basi ungeonoa kwa kuzaliana jomba, lakini matokeo yake ni moja kati ya mikoa ambayo rate ya kuzaliana ni ndogo sana
 
Molimoli twe twigita.....
Iringa kwetu kwinoga!!!
Mwe iringa raha jamani
 
Back
Top Bottom