Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,405
Suala la Zitto kutangaza nia yake kuwania Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema Uchaguzi Mkuu Ujao wa mwaka 2015, limepokewa kwa hisia na tafsiri mbalimbali ndani ya Jamii; Pamoja na mgawanyiko huu wa hisia na tafsiri, mgawanyiko mkubwa upo katika kambi kuu mbili; Kambi ya Kwanza ni ile inayo muunga Mkono Zitto kwa uamuzi huu, wakiwepo viongozi kadhaa ndani ya Chadema; Kambi ya Pili ni ile inayo mpinga Zitto kwa uamuzi huu, akiwemo Mwasisi wa Chadema, Mzee Edwin Mtei;
Mgawanyiko wa kambi hizi kubwa, unatoa picha moja kubwa kwamba: Zitto ni Mgombea mwenye Uzito Mkubwa; Lakini pamoja na Uzito Huu Wa Zitto katika suala husika, Uzito uliopelekea Jamii kugawanyika katika kambi hizi kubwa mbili, bado hoja zinazotolewa na kambi zote – ama za kumpinga au za kumuunga mkono Zitto katika uamuzi wake huu mzito, badala ya kutawaliwa na uzito wa hoja, zinatawaliwa na wepesi wa hoja;
Tukianza na Upande wa Kwanza wa Hoja:
Upande huu ni ule unao mpinga Zitto; Wepesi wa hoja za kambi hii katika suala hili Zito linalohusu Urais wa Nchi ni kwamba, hoja hizi hazinukuu, na wala hazitoi mrejeo wowote kwa UMMA, kuelimisha iwapo Uamuzi Mzito wa Zitto unakiuka KANUNI zozote za Chadema; Wepesi huu wa hoja unapelekea maswali makuu matano kwa kambi hii, inayopinga Uamuzi wa Zitto; JE:
Tukihamia Kwenye Upande wa Pili wa Hoja:
Upande huu ni ule unaomuunga mkono Zitto; Wepesi wa hoja za kambi hii kwa suala hili Zito linalohusu Urais wa Nchi ni kwamba, hoja hizi haziakisi matarajio na matamanio ya wananchi walio wengi katika Tanzania ya leo, hasa kuelekea mwaka 2015; Wepesi huu wa hoja unapelekea maswali makuu manne kwa kambi inayo unga Mkono Uamuzi wa Zitto; JE:
Ni matumaini yangu kwamba, majibu kwa maswali haya yatasaidia kambi hizi kuu mbili kuja na hoja nzito ama Kumpinga, au Kumuunga Mkono Zitto Katika nia yake ya kuwania Urais wa Tanzania, 2015, badala ya kuendelea kutawaliwa na Wepesi wa hoja katika suala hili Zito;
Mbali ya Zitto, hata huko mbeleni tujitahidi kupima wagombea wengine wote kutoka vyama vyote kwa mwendo huu, kwani kwa kufanya hivyo, tutahamia katika ushindani wa siasa wenye tija kwa wananchi kwa maana ya kwamba - SIASA ZA MASUALA - ZINAZOLINGANISHA MASUALA NA WATU (WAGOMBEA) badala ya SIASA ZA WATU (WAGOMBEA) - ZINAZOLINGANISHA WATU NA WATU (WAGOMBEA), kama ilivyo sasa;

- Pingamizi hii inatokana na Zitto kukiuka Kanuni Yoyote Ya Chadema KIKATIBA?
- Kama Jibu ni NDIO, Zitto Amekiuka Kanuni ipi?
- Adhabu ya Kukiuka Kanuni Hii Ya Kikatiba ni ipi?
- Maamuzi Juu ya Adhabu hiyo hufanywa na Kikao Kipi?
- Kwanini Zitto Anapingwa Barabarani na Vibarazani Badala ya Ndani Ya Kikao Hiki?
Tukihamia Kwenye Upande wa Pili wa Hoja:
Upande huu ni ule unaomuunga mkono Zitto; Wepesi wa hoja za kambi hii kwa suala hili Zito linalohusu Urais wa Nchi ni kwamba, hoja hizi haziakisi matarajio na matamanio ya wananchi walio wengi katika Tanzania ya leo, hasa kuelekea mwaka 2015; Wepesi huu wa hoja unapelekea maswali makuu manne kwa kambi inayo unga Mkono Uamuzi wa Zitto; JE:
- Zitto Anasimamia Wapi Kuhusu Suala La Mfumo Wa Muungano?
- Zitto Anasimamia Wapi Kuhusu Mfumo wa Uchumi Wa Nchi, ambapo kwa upande mmoja, wapiga kura wengi ni wale Waliosalitiwa na Ujamaa, na kwa upande wa Pili, Wagombea Urais kutoka Vyama Vyote Vya Siasa Wanaendesha Maisha Yao Kiliberali na Kibepari?
- Zitto Anasimamia Wapi Kuhusu Miiko ya Uongozi, Hasa Suala La Rushwa?
- Zitto Anasimamia Wapi Kuhusu Katiba Mpya, hasa nini kiwemo na nini kisiwemo, pamoja na mkakati wake wa kusimamia na kuyalinda hayo?