Uzinzi ni dhambi ya mauti...

Uzinzi ni dhambi ya mauti...

Habarini za wakati huu wakuu..

Mimi ni kijana wa kiume, umri wangu ni kati ya miaka 30-37, sijaoa. Kwa taaluma ni Mwanasheria. Pia ni mwandishi wa vitabu vya Sheria kwa lugha ya Kiswahili.

Niko JF tangu 2012, ukifuatilia nyuzi zangu nyingi tangu najiunga JF utagundua kwamba zilikuwa zikihusiana na uzinzi huohuo (Biblia inasema kile kimtokacho mtu ndicho kilichoujaza moyo wake), kiukweli nimeandika mabandiko mengi sana humu JF ya kuutukuza uzinzi kwasababu uzinzi ndiyo ulikuwa umeujaza moyo wangu.

Unajua, kwa sisi wanaume, ipo fahari ukiwa na wanawake wengi. Lakini kwenye ulimwengu wa kiroho ipo hatari kubwa mbeleni kuliko hata hiyo fahari ya muda mfupi. Nakushuhudia kwamba ujana wangu nimeutumia kufanya uzinzi/umalaya wa kiwango cha SGR, nimetembea na wanawake wa marika na sifa tofautitofauti. Nimeumiza sana mioyo ya wanawake bila kujua hatari niliyokuwa naikaribia.

Baada ya kupitia changamoto flani ofisini nikajikuta nimeokoka. Mungu alianipitisha kwenye jaribu ambalo lilinifanya nimgeukie yeye kwasababu, kibinadamu nilikosa majibu ya changamoto hiyo, nikajisalimisha kwake, lakini nikiwa wokovuni, dhambi pekee niliyokuwa napambana nayo vikali ilikuwa ni hiyo ya uzinzi na ulevi, nikawa bado nafanya zinaa na kunywa pombe kwa kificho halafu natubu, kuna mambo yangu yakawa hayaendi.

Mimi ni msomaji mzuri sana wa Biblia, msomaji mzuri mno. Nilitambua kwamba ni hatari kufanya dhambi kwa kujua; lakini nikawa napuuza, nikijipa moyo kwamba eti nitatubu baadaye! Kwahiyo nikawa mlokole vuguvugu.

Siku za hivi karibuni nikamuomba Mungu sana anisaidie niushinde uzinzi na ulevi. Sasa naamini kwamba yasiyowezekana kwa mwanadamu yanawezekana kwa Mungu, ni kweli nimefanikiwa kuachana na uzinzi na ulevi, sikatai kwamba majaribu ni mengi hasa kwenye uzinzi, lakini mara zote Mungu ananitengenezea mlango wa kutokea kwenye kila jaribu. Ukiokoka, wadada ndiyo wanajileta kwa wingi hadi inatisha, usipokuwa na nguvu za Mungu unaweza ukasalimu amri!

HATARI ZA UZINZI:-
Kwanza ukisoma Yakobo 4:4 inasema, "Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu?". Kwa lugha nyepesi kabisa ni kwamba, ukizini tu, automatically unakuwa adui wa Mungu.

Ufunuo 21:8 inawataja wazinzi na adhabu watakayokutana nayo huko Mbinguni, lakini mwishoni wa mstari huo wa 8 kuna maneno, "mauti ya pili".

KWANINI UZINZI NI DHAMBI YA MAUTI?
Kwanza nitoe angalizo kwamba hakuna dhambi kubwa wala ndogo. Ila kwa asili, mara baada ya kuwepo kwa misingi ya Ulimwengu, Mungu amekuwa akichukizwa sana na uzinzi (Soma Hesabu 25:1-3).

Uzinzi ni dhambi ya mauti kwasababu, kwetu Wakristo hii miili yetu ni hekalu (makazi) ya Roho Mtakatifu (1Wakorintho 6:19). Mathayo 12:31-32 inasema kwamba dhambi nyingine zote zinasameheka isipokuwa dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu. Kwahiyo ukizini kwa kuutumia huo mwili wako ambao ni hekalu la Roho Mtakatifu unakuwa umemkufuru huyo Roho Mtakatifu aliyeko ndani yako, ataondoka na kukuacha ubaki peke yako.

Lakini pia, dhambi pekee inayofanyika mwilini katika amri 10 za Mungu ni dhambi ya uzinzi, dhambi nyingine zote ni nje ya miili yetu.

Kwahiyo ukizini na mwanamke unafanyika kuwa mwili mmoja naye (1Wakorintho 6:15-16) , kwahiyo kama mwanamke alikuwa na mapepo yanahamia kwa mwanaume, halikadhalika kama mwanaume alikuwa na mapepo yanahamia na kwa mwanamke. Kwa mfano; kama mwanamke/mwanaume unayezini naye ana pepo (roho) ya kukataliwa na wewe unaanza kukataliwa, kama alikuwa na pepo la umasikini, linahamia na kwako pia. So usishangae mambo yakibadilika, tatizo ni huo uzinzi wako.

Kwahiyo vijana wenzangu hasa humu MMU msione ufahari kuzini, mnaziangamiza nafsi zenu wenyewe. Hata Samsoni (Mnadhiri wa Mungu) aliiangamiza nafsi yake mwenyewe kwa uzinzi.

Mwisho, Mtume Paulo kwenye Waraka wake wa kwanza kwa Wakorintho Sura ile ya 7:1-2 anatuambia, tusiwaguse (tusizini na wanawake), lakini kwasababu wanaume tumejawa na tamaa, basi tuoe mke mmoja. Namuomba sana Mungu anaitangulie katika mchakato wangu niliounza wa kupata mke mwema.

Kwa wewe uliyeoa halafu ukazini, hatari ni kubwa zaidi, kwasababu maombi yako hayatajibiwa na Mungu (Soma 1Petro 3:7).

Sensa ya Watu na Makazi ni tarehe 23/08/2022; tujiandae kuhesabiwa, mimi niko tayari, wewe je?

Aksante kwa kusoma uzi wangu na Mungu akutie nguvu uufanyie kazi. Amen!
We need a positive power to fight against negative power.
 
Kama jini naweza hata kuongea naye na nimzuri .... kwani we jamaa kama unapata utelezi wa bure bila usumbufu unataka nini tena mkuu .... kwenye haya maisha niunganishe na huyo jini ... mademu wakibongo wamesha nichosha kila siki virungu
Kaka una mizaha sana
 
Tumia akili yako kujua kama usinzi ni dhambi. Eva aliletwa kwa Adam, wakazaana na kuijaza Dunia. Ninachojua kubaka ni kosa, unalazimisha. Hiyo starehe kaweka Mungu. Mme au mke wa mtu ni kosa, nimemaliza.

Sent using Jamii Forums mobile app
mmmh!!? Kumbuka aliweka na utaratibu wa kuijaza Dunia sio kufanya fanya tu na hizo taratibu zilikuwepo ata kabla ya ujio wa hizi dini za kiarabu na kimagharibi
 
Habarini za wakati huu wakuu..

Mimi ni kijana wa kiume, umri wangu ni kati ya miaka 30-37, sijaoa. Kwa taaluma ni Mwanasheria. Pia ni mwandishi wa vitabu vya Sheria kwa lugha ya Kiswahili.

Niko JF tangu 2012, ukifuatilia nyuzi zangu nyingi tangu najiunga JF utagundua kwamba zilikuwa zikihusiana na uzinzi huohuo (Biblia inasema kile kimtokacho mtu ndicho kilichoujaza moyo wake), kiukweli nimeandika mabandiko mengi sana humu JF ya kuutukuza uzinzi kwasababu uzinzi ndiyo ulikuwa umeujaza moyo wangu.

Unajua, kwa sisi wanaume, ipo fahari ukiwa na wanawake wengi. Lakini kwenye ulimwengu wa kiroho ipo hatari kubwa mbeleni kuliko hata hiyo fahari ya muda mfupi. Nakushuhudia kwamba ujana wangu nimeutumia kufanya uzinzi/umalaya wa kiwango cha SGR, nimetembea na wanawake wa marika na sifa tofautitofauti. Nimeumiza sana mioyo ya wanawake bila kujua hatari niliyokuwa naikaribia.

Baada ya kupitia changamoto flani ofisini nikajikuta nimeokoka. Mungu alianipitisha kwenye jaribu ambalo lilinifanya nimgeukie yeye kwasababu, kibinadamu nilikosa majibu ya changamoto hiyo, nikajisalimisha kwake, lakini nikiwa wokovuni, dhambi pekee niliyokuwa napambana nayo vikali ilikuwa ni hiyo ya uzinzi na ulevi, nikawa bado nafanya zinaa na kunywa pombe kwa kificho halafu natubu, kuna mambo yangu yakawa hayaendi.

Mimi ni msomaji mzuri sana wa Biblia, msomaji mzuri mno. Nilitambua kwamba ni hatari kufanya dhambi kwa kujua; lakini nikawa napuuza, nikijipa moyo kwamba eti nitatubu baadaye! Kwahiyo nikawa mlokole vuguvugu.

Siku za hivi karibuni nikamuomba Mungu sana anisaidie niushinde uzinzi na ulevi. Sasa naamini kwamba yasiyowezekana kwa mwanadamu yanawezekana kwa Mungu, ni kweli nimefanikiwa kuachana na uzinzi na ulevi, sikatai kwamba majaribu ni mengi hasa kwenye uzinzi, lakini mara zote Mungu ananitengenezea mlango wa kutokea kwenye kila jaribu. Ukiokoka, wadada ndiyo wanajileta kwa wingi hadi inatisha, usipokuwa na nguvu za Mungu unaweza ukasalimu amri!

HATARI ZA UZINZI:-
Kwanza ukisoma Yakobo 4:4 inasema, "Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu?". Kwa lugha nyepesi kabisa ni kwamba, ukizini tu, automatically unakuwa adui wa Mungu.

Ufunuo 21:8 inawataja wazinzi na adhabu watakayokutana nayo huko Mbinguni, lakini mwishoni wa mstari huo wa 8 kuna maneno, "mauti ya pili".

KWANINI UZINZI NI DHAMBI YA MAUTI?
Kwanza nitoe angalizo kwamba hakuna dhambi kubwa wala ndogo. Ila kwa asili, mara baada ya kuwepo kwa misingi ya Ulimwengu, Mungu amekuwa akichukizwa sana na uzinzi (Soma Hesabu 25:1-3).

Uzinzi ni dhambi ya mauti kwasababu, kwetu Wakristo hii miili yetu ni hekalu (makazi) ya Roho Mtakatifu (1Wakorintho 6:19). Mathayo 12:31-32 inasema kwamba dhambi nyingine zote zinasameheka isipokuwa dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu. Kwahiyo ukizini kwa kuutumia huo mwili wako ambao ni hekalu la Roho Mtakatifu unakuwa umemkufuru huyo Roho Mtakatifu aliyeko ndani yako, ataondoka na kukuacha ubaki peke yako.

Lakini pia, dhambi pekee inayofanyika mwilini katika amri 10 za Mungu ni dhambi ya uzinzi, dhambi nyingine zote ni nje ya miili yetu.

Kwahiyo ukizini na mwanamke unafanyika kuwa mwili mmoja naye (1Wakorintho 6:15-16) , kwahiyo kama mwanamke alikuwa na mapepo yanahamia kwa mwanaume, halikadhalika kama mwanaume alikuwa na mapepo yanahamia na kwa mwanamke. Kwa mfano; kama mwanamke/mwanaume unayezini naye ana pepo (roho) ya kukataliwa na wewe unaanza kukataliwa, kama alikuwa na pepo la umasikini, linahamia na kwako pia. So usishangae mambo yakibadilika, tatizo ni huo uzinzi wako.

Kwahiyo vijana wenzangu hasa humu MMU msione ufahari kuzini, mnaziangamiza nafsi zenu wenyewe. Hata Samsoni (Mnadhiri wa Mungu) aliiangamiza nafsi yake mwenyewe kwa uzinzi.

Mwisho, Mtume Paulo kwenye Waraka wake wa kwanza kwa Wakorintho Sura ile ya 7:1-2 anatuambia, tusiwaguse (tusizini na wanawake), lakini kwasababu wanaume tumejawa na tamaa, basi tuoe mke mmoja. Namuomba sana Mungu anaitangulie katika mchakato wangu niliounza wa kupata mke mwema.

Kwa wewe uliyeoa halafu ukazini, hatari ni kubwa zaidi, kwasababu maombi yako hayatajibiwa na Mungu (Soma 1Petro 3:7).

Sensa ya Watu na Makazi ni tarehe 23/08/2022; tujiandae kuhesabiwa, mimi niko tayari, wewe je?

Aksante kwa kusoma uzi wangu na Mungu akutie nguvu uufanyie kazi. Amen!
We kama umeupata UKIMWI pambana na kuhudhuria CTC tusitishane mzee wangu samahani sana.
 
Nafikiri kuna haja ya kuzungumzia dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu,hapa.
ni kweli, hiyo mifano nimewahi kumsikia mmoja wa mhubiri akiitoa ila inaponichanganya nimekutana na kipengere katika chapishi hili
mwandishi anasema : -

Dhambi ya kumkufuru Roho haiwezi kufanywa na watu ambao bado hawajaokoka.

Wala Dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu
haiwezi kufanywa na mkristo yoyote tu wa kawaida ambaye hajainuliwa na Mungu katika ngazi yoyote ya utumishi katika huduma iliyowekwa na Mungu ndani yake.
 
Unampenda yesu ama Yesu?
Acha kuandika kisukuma bwashee 😁
Anaweza kukasirika kwa utani ulioungizia asielewe mahali unapohisi kakosea, ungemuambia jina la Yesu au Mungu au Malaika wa Bwana au mengineyo yanayoenda na na hayo ni vema yangeandikwa kwa kuanza na Herufi kubwa kuonesha hali ya Utii na ukuu wa majina hayo.
 
Kasome Biblia vizuri.
Bado hujajua maana ya kumkufuru Roho Mtakatifu.
Ogopa sana kupunguza au kuongeza neno katika Neno la Mungu. Ni heri ufundishe kile ambacho una hakika nacho kwa 100%.
Neno la Mungu si masomo ya upatu kwamba kila mkufunzi anaweza kuja na gear yake
 
dah kweli kabisa wakulugu tubadilizi uzinzi sio dili kabisa. tunajikosesha neema nyingi sana kwa furaha ya muda mchache.
ila sasa na hawa wazazi waache kutupiga hela nyingi kwenye mahari, serikali iingilie kati mahari mwisho iwe laki 2 tuu kwa wale ambao sio bikra na million 10 kwa wale ambao ni bikra. sio kwamba vijana hatutaki kuoa shida ni hizo tozo za hawa wazazi ndio maanai tunaishia kwenye uzinzi
Mahari ni issue?
Si ni suala la kuelewana we na mtu wako?
 
Thats where u go wrong....ndoa sio kutomberna wewe. Ndoa inahusisha familia mbili sio sio suala la kuelewana we na mtu wako.
Kutomberna ndio kitu cha kuelewana wee na mtu wako
 
Anaweza kukasirika kwa utani ulioungizia asielewe mahali unapohisi kakosea, ungemuambia jina la Yesu au Mungu au Malaika wa Bwana au mengineyo yanayoenda na na hayo ni vema yangeandikwa kwa kuanza na Herufi kubwa kuonesha hali ya Utii na ukuu wa majina hayo.
Kwa nini akasirike? Labda kama anavuta bange na kunywa kimpumu ndo atakasirika 😂
 
watajitunza lakin vijana tutashindwa kumudu hio 10mil mwisho wake mabinti watajiachia ili waolewe kirahis
U make a valid point ..therefore i apoint u minister of gender affairs here in jf. So what shuld be the bride price for a demure virgin young lady minister?
 
Hivi huyu ni wew au umeshikiwa simu😂
Ndio mie huyo huyo aloyekutongoza pm alafu ukinipiga kibuti.
Well ukweli usememwe tuu uzinzi sio kabisa ila napo wazazi ndio wanatufanya tuwe wazinzi mahari wanaweka bei mbaya sana. Na nyie wanawake mna tamaa za kupitiliza kweli binadamu tunapenda vizuri basi muwe tayari kuvuta smida sio mkute ready made.
 
🤣🤣🤣Ila wew looh
 
Back
Top Bottom