Uzinzi ni dhambi ya mauti...

Uzinzi ni dhambi ya mauti...

Hicho ndicho kilichoandikwa kwenye Biblia. Siyo msimamo wangu.
Japo kimeandikwa ila umetafsiri kwa hisia zako, hatari ya hiyo tafsiri yako ni kuwa watu watadhani dhambi ya uzinzi ndo dhambi isiyosameheka. Kumbe dhambi hiyo inasameheka na inaondolewa kwa kitubio kupitia damu ya Yesu Kristu.
 
dah kweli kabisa wakulugu tubadilizi uzinzi sio dili kabisa. tunajikosesha neema nyingi sana kwa furaha ya muda mchache.
ila sasa na hawa wazazi waache kutupiga hela nyingi kwenye mahari, serikali iingilie kati mahari mwisho iwe laki 2 tuu kwa wale ambao sio bikra na million 10 kwa wale ambao ni bikra. sio kwamba vijana hatutaki kuoa shida ni hizo tozo za hawa wazazi ndio maanai tunaishia kwenye uzinzi
million 10!? Kwan hiyo bikra Ina nini hasa
 
Nakazia hapa,1 Wakorintho 6:18-Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe....
 
million 10!? Kwan hiyo bikra Ina nini hasa
Hii ni ili wazazi wajitume zaidi katika kuhakikisha watoto wao wa kike wanakuwa sio breki pumbuz.
Its a virtue being virtuous and should be dully rewarded!
 
Nakazia hapa,1 Wakorintho 6:18-Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe....
Barikiwa sana kwa kufuatilia mkuu.
 
kabisa na hilo linaeleweka ila pale unapo onyesha jitihada za makusudi kuushinda uzinzi basi utakuwa kwenye njia salama kabisa. endelea hivyo hivyo.
Asante na ubarikiwe sana
 
Japo kimeandikwa ila umetafsiri kwa hisia zako, hatari ya hiyo tafsiri yako ni kuwa watu watadhani dhambi ya uzinzi ndo dhambi isiyosameheka. Kumbe dhambi hiyo inasameheka na inaondolewa kwa kitubio kupitia damu ya Yesu Kristu.
Mkuu, neno la Mungu ni siri. Na kwa mujibu wa Biblia yenyewe (1Wakorinto 14:26) inasema, kila mtu ana tafsiri yake juu ya neno la Mungu kulingana na namna anavovuviwa na Roho Mtakatifu.

Bilashaka hujauelewa vizuri uzi wangu, sasa kama dhambi ya uzinzi haisameheki, kivipi mimi niseme nimeokoka (nimesamehewa dhambi) na nilikuwa mzinzi wa kupindukia?

Labda niweke kumbukumbu sawa, hakuna dhambi isiyosameheka, damu ya Yesu iliyomwagika Msalabani ndiyo upatanisho wetu kwa Mungu (1Yohana 2:1-2).

Biblia imetumia lugha kali ya utisho (kutokusameheka), ili kuonyesha gadhabu ya Mungu juu ya dhambi hii ya uzinzi ikifanyika kwa mazoea eti kwasababu kuna msamaha, lakini ukiomba msamaha wa dhati kwa Mungu na kuahidi kutoirudia tena basi atakusamehe kwasababu yeye ni mwaminifu na wa haki.
 
Habarini za wakati huu wakuu..

Mimi ni kijana wa kiume, umri wangu ni kati ya miaka 30-37, sijaoa. Kwa taaluma ni Mwanasheria. Pia ni mwandishi wa vitabu vya Sheria kwa lugha ya Kiswahili.

Niko JF tangu 2012, ukifuatilia nyuzi zangu nyingi tangu najiunga JF utagundua kwamba zilikuwa zikihusiana na uzinzi huohuo (Biblia inasema kile kimtokacho mtu ndicho kilichoujaza moyo wake), kiukweli nimeandika mabandiko mengi sana humu JF ya kuutukuza uzinzi kwasababu uzinzi ndiyo ulikuwa umeujaza moyo wangu.

Unajua, kwa sisi wanaume, ipo fahari ukiwa na wanawake wengi. Lakini kwenye ulimwengu wa kiroho ipo hatari kubwa mbeleni kuliko hata hiyo fahari ya muda mfupi. Nakushuhudia kwamba ujana wangu nimeutumia kufanya uzinzi/umalaya wa kiwango cha SGR, nimetembea na wanawake wa marika na sifa tofautitofauti. Nimeumiza sana mioyo ya wanawake bila kujua hatari niliyokuwa naikaribia.

Baada ya kupitia changamoto flani ofisini nikajikuta nimeokoka. Mungu alianipitisha kwenye jaribu ambalo lilinifanya nimgeukie yeye kwasababu, kibinadamu nilikosa majibu ya changamoto hiyo, nikajisalimisha kwake, lakini nikiwa wokovuni, dhambi pekee niliyokuwa napambana nayo vikali ilikuwa ni hiyo ya uzinzi na ulevi, nikawa bado nafanya zinaa na kunywa pombe kwa kificho halafu natubu, kuna mambo yangu yakawa hayaendi.

Mimi ni msomaji mzuri sana wa Biblia, msomaji mzuri mno. Nilitambua kwamba ni hatari kufanya dhambi kwa kujua; lakini nikawa napuuza, nikijipa moyo kwamba eti nitatubu baadaye! Kwahiyo nikawa mlokole vuguvugu.

Siku za hivi karibuni nikamuomba Mungu sana anisaidie niushinde uzinzi na ulevi. Sasa naamini kwamba yasiyowezekana kwa mwanadamu yanawezekana kwa Mungu, ni kweli nimefanikiwa kuachana na uzinzi na ulevi, sikatai kwamba majaribu ni mengi hasa kwenye uzinzi, lakini mara zote Mungu ananitengenezea mlango wa kutokea kwenye kila jaribu. Ukiokoka, wadada ndiyo wanajileta kwa wingi hadi inatisha, usipokuwa na nguvu za Mungu unaweza ukasalimu amri!

HATARI ZA UZINZI:-
Kwanza ukisoma Yakobo 4:4 inasema, "Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu?". Kwa lugha nyepesi kabisa ni kwamba, ukizini tu, automatically unakuwa adui wa Mungu.

Ufunuo 21:8 inawataja wazinzi na adhabu watakayokutana nayo huko Mbinguni, lakini mwishoni wa mstari huo wa 8 kuna maneno, "mauti ya pili".

KWANINI UZINZI NI DHAMBI YA MAUTI?
Kwanza nitoe angalizo kwamba hakuna dhambi kubwa wala ndogo. Ila kwa asili, mara baada ya kuwepo kwa misingi ya Ulimwengu, Mungu amekuwa akichukizwa sana na uzinzi (Soma Hesabu 25:1-3).

Uzinzi ni dhambi ya mauti kwasababu, kwetu Wakristo hii miili yetu ni hekalu (makazi) ya Roho Mtakatifu (1Wakorintho 6:19). Mathayo 12:31-32 inasema kwamba dhambi nyingine zote zinasameheka isipokuwa dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu. Kwahiyo ukizini kwa kuutumia huo mwili wako ambao ni hekalu la Roho Mtakatifu unakuwa umemkufuru huyo Roho Mtakatifu aliyeko ndani yako, ataondoka na kukuacha ubaki peke yako.

Lakini pia, dhambi pekee inayofanyika mwilini katika amri 10 za Mungu ni dhambi ya uzinzi, dhambi nyingine zote ni nje ya miili yetu.

Kwahiyo ukizini na mwanamke unafanyika kuwa mwili mmoja naye (1Wakorintho 6:15-16) , kwahiyo kama mwanamke alikuwa na mapepo yanahamia kwa mwanaume, halikadhalika kama mwanaume alikuwa na mapepo yanahamia na kwa mwanamke. Kwa mfano; kama mwanamke/mwanaume unayezini naye ana pepo (roho) ya kukataliwa na wewe unaanza kukataliwa, kama alikuwa na pepo la umasikini, linahamia na kwako pia. So usishangae mambo yakibadilika, tatizo ni huo uzinzi wako.

Kwahiyo vijana wenzangu hasa humu MMU msione ufahari kuzini, mnaziangamiza nafsi zenu wenyewe. Hata Samsoni (Mnadhiri wa Mungu) aliiangamiza nafsi yake mwenyewe kwa uzinzi.

Mwisho, Mtume Paulo kwenye Waraka wake wa kwanza kwa Wakorintho Sura ile ya 7:1-2 anatuambia, tusiwaguse (tusizini na wanawake), lakini kwasababu wanaume tumejawa na tamaa, basi tuoe mke mmoja. Namuomba sana Mungu anaitangulie katika mchakato wangu niliounza wa kupata mke mwema.

Kwa wewe uliyeoa halafu ukazini, hatari ni kubwa zaidi, kwasababu maombi yako hayatajibiwa na Mungu (Soma 1Petro 3:7).

Sensa ya Watu na Makazi ni tarehe 23/08/2022; tujiandae kuhesabiwa, mimi niko tayari, wewe je?

Aksante kwa kusoma uzi wangu na Mungu akutie nguvu uufanyie kazi. Amen!
Nikupe hongera kwa uamuzi wako wa hekima ku-surrender kwa Mungu.
Nikushauri kidogo tu,
1. Fahau kuoa sio solution la kushinda uzinzi.Utaendelea kujaribiwa mpaka proven victorious kwenye eneo hilo,na zipo njia za kuku-sustain ushinde, know them.
2. Kubali kuwa mwanafunzi ufundishwe ili uukuliwe wokovu(watch out na mafundisho potofu as we live at the end of edges).
Matendo 8:26-34..
Verse 31. Akasema nitawezaje kuelewa,mtu asiponiongoza?Akamsihi Filipo apande na kuketi pamoja naye.
(Ni habari ya yule towashi kutoka Kushi/Ethiopia ambaye Filipo alimsaidia kuelewa alichokuwa anakisoma kwenye chuo Cha nabii Isaya).
Siwezi kuweka hapa maana ya kumkufuru Roho Mtakatifu kimaandiko nafikiri sio mahali sahihi sana.
Incase utahitaji waweza kunicheki pm.
Mungu akubariki na kukupa ushindi wa kuushinda mwili na tamaa zake, through him we are more than the conquerors.
 
Mkuu, kwanza nikushukuru sana kwa mchango wako mzuri. Kabla sijakufata PM na kwa faida ya wengine pia, naomba uziweke hapa njia za kuniwezesha kushinda. Tafadhali sana...
 
Mkuu, kwanza nikushukuru sana kwa mchango wako mzuri. Kabla sijakufata PM na kwa faida ya wengine pia, naomba uziweke hapa njia za kuniwezesha kushinda. Tafadhali sana...
Atiririke tuko wengi tungependa kuzijua hizo njia...
 
Nikupe hongera kwa uamuzi wako wa hekima ku-surrender kwa Mungu.
Nikushauri kidogo tu,
1. Fahau kuoa sio solution la kushinda uzinzi.Utaendelea kujaribiwa mpaka proven victorious kwenye eneo hilo,na zipo njia za kuku-sustain ushinde, know them.
2. Kubali kuwa mwanafunzi ufundishwe ili uukuliwe wokovu(watch out na mafundisho potofu as we live at the end of edges).
Matendo 8:26-34..
Verse 31. Akasema nitawezaje kuelewa,mtu asiponiongoza?Akamsihi Filipo apande na kuketi pamoja naye.
(Ni habari ya yule towashi kutoka Kushi/Ethiopia ambaye Filipo alimsaidia kuelewa alichokuwa anakisoma kwenye chuo Cha nabii Isaya).
Siwezi kuweka hapa maana ya kumkufuru Roho Mtakatifu kimaandiko nafikiri sio mahali sahihi sana.
Incase utahitaji waweza kunicheki pm.
Mungu akubariki na kukupa ushindi wa kuushinda mwili na tamaa zake, through him we are more than the conquerors.
Injili kwa mataifa yote Mkuu.
 
Tumia akili yako kujua kama usinzi ni dhambi. Eva aliletwa kwa Adam, wakazaana na kuijaza Dunia. Ninachojua kubaka ni kosa, unalazimisha. Hiyo starehe kaweka Mungu. Mme au mke wa mtu ni kosa, nimemaliza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umesema hujasoma uzi wote halafu umesha-conclude! Huenda jibu la swali lako lipo kwenye content ya uzi wangu.

Now I have come to a conclusion that EVEN COMMON SENSE IS NOT COMMON.
Hilo neno la mwisho kuna ticha wetu moja wa majengo sec moshi alikuwa anapend sana kulitumia..... any way tupo hapa kupeana challenge tu ....
 
Back
Top Bottom