Uzinduzi wa kisima .... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uzinduzi wa kisima ....

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Kelvin Joseph, Mar 31, 2011.

  1. Kelvin Joseph

    Kelvin Joseph Member

    #1
    Mar 31, 2011
    Joined: Mar 22, 2011
    Messages: 11
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 0
    Katika kijiji cha **** wananchi walijengea kisima cha kijiji Wakati wa uzinduzi wa kisima hicho Mh:Mizengo Pinda akaalikwa kuwa mgeni rasmi. Wakati akionyeshwa mandhari ya kijiji hicho akapelekwa kwenye kisima chenyewe. Wakakifunua ili akione. Ghafla Mheshimiwa akashtuka na kurudi nyuma. Wananchi Wakamuuliza: Mheshimiwa vipi Mbona umeshtuka hivyo kunanini? Akawauliza: hivi huku kijijini kwenu mnafuga mamba? Wakamuuliza: kwanini? Akasema nimeona kitu kama mamba akarudi kuangalia vizuri akagundua ilikua sura yake.
     
  2. MAMMAMIA

    MAMMAMIA JF-Expert Member

    #2
    Mar 31, 2011
    Joined: Feb 26, 2008
    Messages: 3,823
    Likes Received: 16
    Trophy Points: 0
    Ha, ha, ha!
     
  3. Joseph

    Joseph JF-Expert Member

    #3
    Mar 31, 2011
    Joined: Aug 3, 2007
    Messages: 3,522
    Likes Received: 87
    Trophy Points: 145
    Unajipenda ndugu yangu na utani huo?Wenzio wana kesi za kujibu,kuwa makini.
     
  4. c

    cc_africa Senior Member

    #4
    Apr 2, 2011
    Joined: May 30, 2010
    Messages: 121
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 0
    Unauliza makofi police
     
  5. Mshume Kiyate

    Mshume Kiyate JF-Expert Member

    #5
    Apr 2, 2011
    Joined: Feb 27, 2011
    Messages: 6,774
    Likes Received: 20
    Trophy Points: 135
    Hiyo kesi kaka unatania serikali
     
  6. Horseshoe Arch

    Horseshoe Arch JF-Expert Member

    #6
    Apr 2, 2011
    Joined: Aug 10, 2009
    Messages: 9,854
    Likes Received: 3,127
    Trophy Points: 280
    insult...wote tumeumbwa kwa mfano wa Mwenyezi Mungu
     
  7. s

    seniorita JF-Expert Member

    #7
    Apr 2, 2011
    Joined: Nov 1, 2010
    Messages: 674
    Likes Received: 4
    Trophy Points: 0
    Very true, kila binadamu anaumbwa kwa mfano na sura ya Mungu...na hakuna anayechagua taswira yake, we are born without our choices as how we shall look like....kama tungepewa uchaguzi of course kila mtu angeji design vile atakuwa...so stop this nonsense, unamtukana Mungu na unatukana uumbaji wa Mungu. Kwani wewe unajiona mzuri sana? Pengine na wewe uko kama nyani anacheka wenziwe kwa vile they cannnot see how they look like behind....be careful and next time think before you write a joke....tena unamtukana kiongozi wa nchi kwa sura yake...that is so pathetic of you. I am glad I dont know you personally otherwise I will be even more disgusted with your behavior....
     
  8. n

    nyuki dume JF-Expert Member

    #8
    Apr 2, 2011
    Joined: Oct 8, 2010
    Messages: 438
    Likes Received: 2
    Trophy Points: 35
    Masihala hayo sio mazuri
     
  9. s

    sugi JF-Expert Member

    #9
    Apr 2, 2011
    Joined: Feb 12, 2011
    Messages: 1,315
    Likes Received: 74
    Trophy Points: 145
    heri mie sijasema.....
     
  10. Jaluo_Nyeupe

    Jaluo_Nyeupe JF-Expert Member

    #10
    Apr 2, 2011
    Joined: Dec 21, 2010
    Messages: 2,248
    Likes Received: 314
    Trophy Points: 180
    mmmh! Hata cjaipenda.
     
  11. donlucchese

    donlucchese JF-Expert Member

    #11
    Apr 3, 2011
    Joined: Mar 23, 2011
    Messages: 6,187
    Likes Received: 968
    Trophy Points: 280
    jamani mnaocomplain hamjui sense of humour?
     
  12. Jaluo_Nyeupe

    Jaluo_Nyeupe JF-Expert Member

    #12
    Apr 3, 2011
    Joined: Dec 21, 2010
    Messages: 2,248
    Likes Received: 314
    Trophy Points: 180
    huo ni udhalilishaji. Utani wa kweli unaohusu maumbile haupendezi. Sasa hapo kuna tofauti gani na kumtania mlemavu kwamba una mguu kama .......... au mikono kama.........?
     
  13. P

    Pascal Mayalla JF-Expert Member

    #13
    Apr 3, 2011
    Joined: Sep 22, 2008
    Messages: 22,183
    Likes Received: 10,223
    Trophy Points: 280
    Mode p'se itendee haki thread hii, hata kama ni jukwaa la jokes kuna utani unaokubalika kama itani lakini hii ni dhihaka, kebehi na udhalilishaji wa viongozi wa kitaifa.
     
  14. komedi

    komedi JF-Expert Member

    #14
    Apr 4, 2011
    Joined: Mar 6, 2011
    Messages: 204
    Likes Received: 1
    Trophy Points: 0
    Kelvin Joseph siku nyingine jaribu kuandika kwa mtindo huu....

    Katika kijiji cha mkongojomwitu wananchi walijengea kisima cha kijiji Wakati wa uzinduzi wa kisima hicho Mh:waziri mkuu akaalikwa kuwa mgeni rasmi. Wakati akionyeshwa mandhari ya kijiji hicho akapelekwa kwenye kisima chenyewe. Wakakifunua ili akione. Ghafla Mheshimiwa akashtuka na kurudi nyuma. Wananchi Wakamuuliza: Mheshimiwa vipi Mbona umeshtuka hivyo kunanini? Akawauliza: hivi huku kijijini kwenu mnafuga mamba? Wakamuuliza: kwanini? Akasema nimeona kitu kama mamba. Wanakijiji wakasogea kuangalia vizuri kisha wakamwambia ''mkuu maji kama kioo tu...mambo ya taswira mheshimiwa''
     
Loading...