Uzi wa kufundishana maisha ya Jela na selo

Superbug

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
12,417
30,928
Makamarade nimeona nianzishe huu Uzi ili kupeana uzoefu wa maisha ya Jela. Sisi wote ni wafungwa watarajiwa alijisemeaga magufuli.

Sasa hebu tupeane mbinu maisha misamiati tamaduni taratibu za Jela ili siku ukienda kule unakuwa Mwenyeji. Pia tuambiane mabosi wanakaa maeneo gani kule Jela? Wanavyumba vyao?

Majitu yaliyouwa je Kila mtu anachumba chake? Au yamelundikwa? Je chumba gani ni hatari zaidi kule Jela na mfungwa gani ni hatari zaidi? Je kuna mfungwa yupo Jela toka mwaka 1977 ccm inazaliwa mpaka leo hajatoka?

Je wafungwa wanapata msongo gani wa mawazo akijua fika mke wake lazima agegedwe wakati yeye yupo Jela? Je wafungwa wakike Wana life la kibabe? La kindava kama wakiume?

Je, wafungwa wakike wanapashanaje joto kimapenzi? Nk
 
Nakumbuka 2019,nilikua mahabusu pale ISISI gerezani,sasa wakati tunasubiri kupewa jezi(zile za orange) na kukaguliwa,TV ilikua imewashwa tunaangali kuna jamaa alikuja dirishani akasema.

"rasta rasta huo umeme wa magufuli rasta haaya,mtaulipia rastaa"
aliongea kwa uchungu na tuliulipia kweli dadeki..
 
Nakumbuka 2019,nilikua mahabusu pale ISISI gerezani,sasa wakati tunasubiri kupewa jezi(zile za orange) na kukaguliwa,TV ilikua imewashwa tunaangali kuna jamaa alikuja dirishani akasema.....

"rasta rasta huo umeme wa magufuli rasta haaya,mtaulipia rastaa"
aliongea kwa uchungu na tuliulipia kweli dadeki..
Kwamba mliulipiaje mkuu!? Duuuuh
 
Jera ukipenda kulakula na wewe ni mwanaume unavuliwa ubigwa haraka sana, yani unatauliwa marinda so usiendekeze njaa ukiwa jera
Pia ukitaka usalama kiasi,kama unavisitor wengi wanaokuletea mazaga,mtafute nyapara mmoja mpe awe anakutunzia....

Bila hivyo utalima sana jembe la mbele na viboko vingi.....
Kuna watu wanazikimbilia nyoka ziwang`ate ila nazo zinakimbia dah...

Usiombe uwe unaumwa HIV halafu ulijichanganya ukaacha kadi,huchukui round utakufa labda uhonge...
 
Nakumbuka 2019,nilikua mahabusu pale ISISI gerezani,sasa wakati tunasubiri kupewa jezi(zile za orange) na kukaguliwa,TV ilikua imewashwa tunaangali kuna jamaa alikuja dirishani akasema.....

"rasta rasta huo umeme wa magufuli rasta haaya,mtaulipia rastaa"
aliongea kwa uchungu na tuliulipia kweli dadeki..
Fafanua mkuu.. kuna maelezo umeyaacha tunahisi yana umuhimu.
 
Kwamba mliulipiaje mkuu!? Duuuuh
Kazi ngumu bro,
Nakumbuka siku moja kuna gogo tulienda kubeba kuleta jikoni,umbali kama mt 50 tu, tulikua 15 tukashindwa kuliweka begani.

Nyapara tuliekua nae akaenda kwa mkuu akamwambia "niongezee nguvu wale jamaa wameshindwa"
Alitandikwa vibao, halafu akaja yeye na wenzie kama wa3 hivi.

Mkuu hukuwepo ila niamini tulibeba gogo likakaa begani na akaanza kupunguza mmoja mmoja mpaka tukabaki 8.

Hapa siongelei magereza yenu ya town(kazi kubwa kumwagilia maua na kufyeka majani). NGWALA,SONGWE,KISONGO,MAWENI,MPECHI na ISISI usiombe ukaingia hizi ngome....

ROHO YAKO MWILI WAKWETU
Na wanautumia kweli
 
Nimeshawahi kumwangushia mti wa miba mshkaji wangu wa home kabisa na sijui kama alipona,nahisi alifia hospital...
Alikua shoga tena aliolewa na cleaner,roho iliniuma sana..

Siku moja tunakata ile miti ya miiba(alikua mlaini mlaini hivi halafu hapendi kazi ngumu)..."nkamwambia kinega (nlikua namwita ivo) ondoka upande huo mti unaangukia huko,nenda kachukue panga zile pale chini"
Alipoenda ndio nkamalizia kukata mti ukampigiza mpaka chini na kumfunika kabisa....(MUNGU ANISAMEHE KWA DHAMBI HII)

Ila nilipigwa sana mpaka nkagoma kupigwa na nlipiga kelele nyingi mikwara kibao...na hela walizokuwa wanapewa na bro ili wasinitese,basi MP akanipa mkanda nikawa KIHEREHERE
 
Ukienda jela jitahidi usiende kwa makosa ya kise"**.. uwe na kosa atleast lina mafuta( uzito)...uwe na watu...jela kinachoumiza kazi ngumu na upweke kiasi..ukiwa na network hizo kazi ngumu utazisikia....usiwe pia mkaidi..uwe na hela na sabuni za kutosha..most of cells hela haziruhurusiwi..sabuni ndio mode of exchange ukitaka msosi mzuri...huko huko jela unaeza fanya biashara ya bangi na ugoro 😂😂😂...,

Ukienda na njaa njaa usipokua makini watu watafunua kitabu chako(ingawa hii maafande wakikufuma mtapigwa mchakae maana ni ushenzi)..
 
Makamarade nimeona nianzishe huu Uzi ili kupeana uzoefu wa maisha ya Jela. Sisi wote ni wafungwa watarajiwa alijisemeaga magufuli...

Nilienda jela bila sababu au kutegemea, maisha ya jela ni mabaya mno mara 10,0000 ya nilivyowaza,

1. Tupige sala sana.
2. Tuache tamaa na pupa.
3. Wivu wa mapenzi na wanawake.
4. Hasira za kupitiliza.
5. Kusamehe na kuachilia.

Hakuna sababu ya kujiandaa kwenda jela, kama wewe unakaribia kwenda huko, piga sala, sio mwisho wa kila kitu.
 
Picha linaanzia tuko site tunavuta bangi msituni huko, miongoni mwa wavuta bangi walikuepo maaskari tulikua tunanyonga nao.

Sasa yule pusha ilikua lazima awape kodi ya meza ili wamlinde wasimchome, naona alizingua aise lilitimba pila Hilo tulichukuliwa tukashuka central😬

Sasa ishu ikawa mtu wa kumcheki Kwa ishu kama io ya kisenge ya kuvuta bangi😀😀 nikasema nitakaa hapa adi mnitoe wenyewe mimi Sina ndugu yoyote hapa mjini🤣

Na kweli nimekaa mahabusu siku 3 wale jamaa kumbe target Yao ilikua pesa tu mwisho waliamua kuniachia tu
Yaani sikukuu imenikutia mahabusu. Nilacha bangi tangu hapo😬😂

Mahabusu kubaya sana sipati picha huko jela Kuna jamaa alikua analia tu aliletewa chakula Hali watu ambao hatuna ndugu tunabonda tu. Mahabusu unaweza kua huna ndugu ukala ukashiba Kuna watu wako so frustrated aise
 
Back
Top Bottom