Cheka: Sina hamu jamani maisha ya JELA sio mchezo

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,074
42,852
bondia maarufu nchini, Francis cheka SMG mkali ambaye amewahi kushikilia mataji kadhaa ya dunia kwa kuwachakaza mabondia wa ndani na nje ya Tanzania ameanika mkasa wake wa kutupwa jela na namna ambavyo mpaka leo bado haamini kilichomkuta. Kivipi? Hebu endelea naye upata uhondo...!

ISHU ILIANZIA HIVI

Ilikuwa Februari 2, 2015, Cheka alipohukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela, siku hiyo hakulala nyumbani kwake kama alivyozoea, kwa mara ya kwanza alilala kwenye gereza la Morogoro.

Asubuhi ya siku hiyo kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Morogoro, Cheka alikutwa na hatia ya kumjeruhi meneja wa baa yake iliyopo mjini Morogoro, kosa alilolifanya Julai 2, 2014 na kuhukumiwa siku hiyo.

“Siku ya hukumu niliondoka nyumbani nikiwa tofauti, niligombana sana na mke wangu siku hiyo, nikamwambia sitaki nikuone mahakamani, nikaondoka, ila baadae mke wangu alinifuata nyuma.

“Nilisomewa mashtaka yangu, hakimu akaniambia jitetee, siku hiyo sijui nilikuwaje, nikamjibu hakimu fanya uamuzi wowote ambao mahakama inaona.

“Nilijibu kwa hasira, nadhani sababu niliona kama mimi ndiye nilikuwa nastahili kushtaki, kwani huyo aliyedai nimempiga ndiye alinifanyia mambo ya ajabu.

“Nilichukua fedha yangu ya pambano la Phil Williams nikampa na nyingine nilikopa benki ili tufanye biashara, siku nakwenda hakuna chochote kinachofanyika, hakuna pesa, nilipomuuliza akanijibu vibaya.

“Kiukweli nilikasirika, ukizingatia namna ninavyopata fedha kiugumu, sio siri nilimpiga ngumi mbili tatu, lakini hazikuwa na thamani ya fedha yangu, sema ndivyo hivyo sheria, nilivyomwambia hakimu aamue anavyooona inafaa ndipo akanipiga miaka mitatu jela na faini ya Sh 1 Milioni.

SIKU YA KWANZA GEREZANI HAKULALA

Cheka anasema kuna wakati alihisi yuko ndotoni na kuna wakati alikuwa akijifinya akidhani labda anaota, lakini ulibaki kuwa kweli kwamba anakwenda gerezani.

“Mke wangu na mwanangu Historia walilia sana, hawakutarajia, lakini ndivyo hivyo imeshatokea mimi nakwenda jela, ndugu zangu waliumia, nilikuwa nawaza namna mama yangu atakavyopokea taarifa.

Bahati mbaya hata WBF walitangaza kunivua ubingwa wao sababu nimekuwa mfungwa, niliumia mno, sikuwahi kufikiria kama ipo siku nitafungwa.

“Siku hiyo nilikuta wafungwa wenzangu wakinisubiri kwa hamu kwani walikuwa wakifuatilia kesi yangu, unajua mle gerezani kuna muda wa kuangalia taarifa ya habari, kuna tv hivyo walikuwa wakifuatilia kesi yangu kwenye tv.

“Bwana Jela aliniita akaniambia, Cheka tunajua kilichokuleta, lakini sisi sio tunaoleta watu gerezani, sisi tunapokea tu, hivyo jipe moyo ipo siku utatoka.

Siku hiyo hakuwa na godoro, lakini kutokana na umaarufu wake kwenye ngumi kuna mfungwa mmoja alikuja kuwa rafiki yake anaitwa Mahina ambaye alikuwa amefungwa miaka mitano, alimkaribisha kwenye godoro lake kabla ya Cheka kupewa lake.

“Nilikaa kama siku 14 ndipo nikapewa nguo za gerezani, niliambiwa nisubiri nguo zangu, zilikuwepo nyingine, lakini zilikuwa zimevaliwa, naona walinionea huruma kuniepusha na magonjwa ya ngozi.

“Nilikuwa maarufu ndani ya muda mfupi, wafungwa karibu wote walikuwa marafiki zangu, walipenda niwafundishe ngumi, nikiwa na wiki moja gerezani, nilipewa kitengo cha kufanya kazi jikoni.

Anasema hata askari Magereza walimpenda, kila waliposimuliwa kilichompeleka jela waliumia, lakini ndivyo hivyo, ili asiteseke wakamuweka jikoni ambako alikuwa anakula vizuri tofauti na wafungwa wengine.

Kule jikoni tulikuwa tunapata maziwa ya askari, mabosi wakipikiwa kuku, sisi tunakinga damu, tunaikaanga tunalia ugali, jela kumenifunza hadi kula ugali na damu ya kuku tulikuwa tukiita hanjamu, hata mboga yetu ilikuwa inaungwa,” anasimulia Cheka.

Anasema mbali na jikoni alikuwa anapenda kusomba maji kujaza mapipa ya gerezani, alifanya hivyo si kama alipangiwa, lakini alikuwa akiamini ni sehemu ya mazoezi yake akiwa gerezani.

RATIBA ILIVYOKUWA GEREZANI

Cheka anasema walikuwa wakilala saa 1 usiku, lakini saa 10:00 jioni wote wanakuwa ndani ya gereza milango inafungwa.

“Mle ndani kuna kama ukumbi kuna televisheni, tulikuwa tunaangalia tv hadi saa moja tunatakiwa kulala na muda wa kutoka kila mmoja kuelekea kwenye kazi yake ni saa moja asubuhi baada ya gwaride.

“Gerezani mlo ni mara moja, huwa kuna ratiba ya uji, lakini hadi uupate umefanya kazi, tunakula ugali mchana pekee, hivyo ukiweza kuutunza huo ugali ule usiku unahifadhi na ndivyo tulikuwa tunafanya.

Kuoga napo kuna muda maalumu, sio muda unaotaka wewe kuoga unaenda, ikifika wakati wa kujisaidia ni foleni, unakuta labda katika selo moja tuko wafungwa 150, choo ni kimoja, utake usitake lazima upange foleni.

“Kuna watu walikuwa wakija kunitembelea gerezani, wengine walikuja kinafiki, lakini yote nilimshukuru Mungu, mke wangu alihangaika mno ili nitoke na kuna watu walitumia matatizo yangu kama njia ya kujipatia kipato, walichangisha fedha wakidai za kunisaidia, lakini zikaishia kuliwa, wakati huo mke wangu alikuwa mjamzito, niliumia lakini sikuwa na namna.

SIKU YA KUTOKA HAKUAMINI

Akiwa gerezani Cheka anasema alitembelewa na watu wa Ustawi wa Jamii mara kwa mara ambao kila walipomtembelea walikuwa wakimuuliza maswali mengi sana.

“Alikuwa anakuja dada Upendo na Ponela, walikuja kama mara tatu, siku moja asubuhi niko jikoni nakoroga uji, niliambiwa nijiandae natakiwa kwenda mahakamani, sikuwa hata na viatu.

“Rafiki yangu anaitwa Kisoda yeye alikuwa amehukumiwa miaka 10 akanipa raba zake fasta fasta nikajiandaa tukatoka kwenda mahakamani.

“Sikuamini, nilipoitwa nikaambiwa kuanzia siku ile nitakuwa natumikia kifungo cha nje na nitakuwa nafanya kazi ambazo nitapangiwa na watu wa Ustawi wa Jamii, nililia machozi,” anasimulia.

Anasema hadi siku anapewa kifungo cha nje alikuwa amekaa gerezani siku 42.

“Niliondoka kwenda kuungana na familia yangu, japo sitaki kuyakumbuka maisha ya jela, lakini ni maisha fulani magumu ila basi ni Mungu tu.

Je, Cheka alipotolewa gerezani ili kutumikia kifungo cha nje, alifanya kazi zipi na vipi kuhusu kuzipiga kwenye fani yake ya ngumi? Endelea naye kesho katika hitimisho la simulizi la bondia huyo ambaye ametangaza kuihama nchini.
 
Kashakuwa Tapelii huyoo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inakuwaje huko tupe simulizi

Sent using Jamii Forums mobile app

Hayo yote ni magereza ya kilimo hivyo huko hakuna kudeka. Mkiamka asubuhi ni kwenda shama kulima kuanzia hadi mida ya mchana huku ukiwa umepata kikombe cha uji tu kabla ya kuondoka. Chakula kama kawa, ni mlo mmoja tu kwa siku saa 10 jioni. Huko watu hawadeki maana viherehere wanaweza kukuua kwa kipigo.
 
Hayo yote ni magereza ya kilimo. Mkiamka asubuhi ni kwenda shamba kulima kuanzia hiuo asubuhi hadi mida ya mchana huku ukiwa umepata kikombe cha uji tu kabla ya kuondoka. Chakula kama kawa, ni mlo mmoja tu kwa siku saa 10 jioni. Huko watu hawadeki maana viherehere wanaweza kukuua kwa kipigo.
Hahahaha panatishaa si mchezo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahaha panatishaa si mchezo

Sent using Jamii Forums mobile app

Hizo jela wakienda watoto wa mama huwa wanaishia kulia tu kama watoto wadogo. Wakati wanalima huwa wanapanga mstari wafungwa wote, sasa ukichelewa hata hatua moja tu nyuma ya wenzako, basi kuna wafungwa wanaoitwa viherehere, hao(wapo chini ya nyapala kimamlaka) watakutwanga fimbo hadi ujute kuzaliwa.

Lijualikali (mb)baada ya kuhukumiwa, alipelekwa gereza la Idete na kuishi siku chache sana kabla ya kuhamishiwa Ukonga. Bila shaka waligundua asingeweza kuishi pale mahali. Sasa Cheka alikua gereza la mkoa, kazi kubwa ni kuchota maji na kupasua kuni, full kuangali tv! anyway, sema tu hata ile hali ya mtu kukunyima uhuru wako, bado ni mateso na adhabu kubwa sana.
 
Ushawahi kwenda pale idete nini maana unapajua haswaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom